.

Alhamisi, 17 Oktoba 2013

Rapper Octopizzo Kwenye Collabo Na Msanii Mkubwa Wa Nigeria.


Octopizzo rapa anayefanya poa sana katika gemu Afrika Mashariki anazidi kuongeza idadi za kolabo na wasanii mbalimbali barani Africa na habari iliyopo ni kwamba rapa huyo amepiga kolabo na mwanamuziki mkongwe wa nchini Nigeria, King Sunny Ade.
Wawili hao tayari wamekwisha rekodi wimbo mmoja unaoitwa 'Tlongo' kupitia studio maarufu ya Coke Studio ambapo ameweka wazi kuwa kukutana na gwiji huyo wa Nigeria ni kama amekutana na rapa nyota wa Marekani Jay Z.
Aidha Octopizzo ameelezea kuwa yupo mbioni kufanya kolabo zingine zaidi na wanamuziki wakongwe katika gemu kwani nia na dhumuni lake haswa ni kutanua wigo wa muziki wake duniani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni