.

Jumapili, 23 Novemba 2014

Hatimaye Diamond Aongelea Kuhusu Kuachana na Wema na Mahusiano yake na Zari Boss Lady

Jana Nov 21, Diamond amesikika kwenye show ya XXL ambapo amezungumzia mambo mengi, baadhi ya yale aliyoyazungumzia ni pamoja na story zilizoenea mitandaoni kwamba mahusiano ya msanii huyo na Wema yameisha pamoja na story ambayo imetokana na kuenea kwa picha mitandaoni za msanii huyo na Zari the Boss Lady kutoka Uganda.
Hii ni sehemu ya mahojiano aliyofanya Diamond kwenye XXL:

Adam Mchomvu :”…Nataka kujua ile vibe ya Fiesta that day, story zilikuja ooh Diamond kazomewa.. kazomewa kazomewa..na vitu kama vile, sijapata chance ya kukusikia wewe una kipi cha kuzungumzia kuhusiana na that situation..?“

Diamond :- “… Siku zile kwangu ilikuwa kama mchezo, unajua muziki ushakuwa kama sio fani tena, ushakuwa kama siasa.. So, lazima uichukulie hivyo wewe mwenyewe kama msanii ujue una control vipi kwa sababu sio mara ya kwanza vitu kama hivyo vishatokea Maisha.. Maisha yalitupwa mpaka na mayai viza kabisa.. Ni vitu ambavyo vikitokea naonaga kama ni kawaida…“

B 12  :-“…Kwa hiyo ukweli uko wapi kati yako wewe na Wema Sepetu?…”

Diamond  :- “…Kuna vitu vitu fulani nadhani kuvizungumza sio vizuri… Lakini ikifikia kuvizungumzia vinazungumziwa… Uzuri wa mahusiano yetu ni kwamba kila mtu anafahamu… Haijafikia kuweka wazi ndio maana ninapoulizwa inakuwa ni swali gumu kulijibu.. “

B 12 :- “.. Ni gumu kwa upande wako lakini yeye yuko tayari kuzungumza kwamba it’s over kati yangu mi’ na Diamond…“

Diamond  :- “… Sijui…“

B 12  :- “…Hii ngoma kama umemzungumzia yeye direct hivi… watu wamekuza akili zao zikaenda mbali zaidi kimawazo lakini, kwamba inawezekana ile singo umemwimbia yeye hivi kwamba bado unamzimia japokuwa bado kama kakutosa hivi…“
wemadiamond

Diamond  : “.. Waswahili wanasema ‘A’ na ‘B’ yote majibu, halafu ukisikiliza ile nyimbo kama kweli mtu mwenye ufahamu wako, kweli kabisa hauwezi kuwa na maswali mengi …“
Kuhusiana na mahusiano yake na Zari the Boss Lady, Diamond amejibu hivi:

Diamond  :- “.. Zari ni rafiki yangu tu, alipokuja hapa mimi ndio nilikuwa mwenyeji wake Tanzania na kama mimi ndiyo mwenyeji sikutaka kuleta roho za kibaguzi, unajua hata alipokuja Davido pia ilibidi awe na mimi karibu ili hata kesho na kesho kutwa  mimi nikiwa Nigeria basi Davido anipokee hivyo hivyo…“

Ijumaa, 21 Novemba 2014

Hivi ndivyo Whatsapp imevunja ndoa ya wawili hawa…


whatsapp2Wiki chache baada ya WhatsApp kutambulisha mfumo mpya ambapo iwapo unamtumia message mtu inakuonyesha alama ya tick mbili za kijani na pia inaonyesha muda ambao mtu uliyemtumia message hiyo ameisoma, tayari kuna ndoa ambayo imeingia matatizoni kutokana na hilo.
Mwanaume mmoja Saudi Arabia ametoa talaka kwa mkewe kutokana na kitendo cha mwanamke huyo kutokujibu message aliyomtumia WhatsApp.
Mwanaume huyo amesema kitendo kilichomkasirisha zaidi ni pale aliporudi nyumbani na kumkuta mke wake akiwa busy anachat na marafiki zake kupitia mtandao huo wakati message aliyomtumia yeye hakuijibu.
dreamstime_s_36639295-600x399
Jamaa huyo ameona kama kitendo hicho ni dharau kubwa na hakuwa tayari kuendelea na ndoa hiyo ambayo imedumu kwa miaka miwili tangu ifungwe.

Ronaldo aosha vyombo baada ya kushindwa


Ronaldo aosha vyombo baada ya kushindwa katika karata na mchezaji wa Tenisi Rafa Nadal
Ronaldo aosha vyombo baada ya kushindwa katika karata na mchezaji wa Tenisi Rafa Nadal
Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Brazil Ronaldo alilazimika kuosha vyombo baada ya kushindwa katika mchezo wa karata na mchezaji wa tennisi Rafa Nadal,na kumfanya mchezaji huyo wa tenisi kupokea dola 50,000 za hazina yake ya kutoa msaada huku Ronaldo akiosha vyombo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 alikabiliana vilivyo na mwana tenisi huyo kutoka uhispania katika mechi kati ya wawili hao katika meza ya pokerstar, Casino ya Hippodrome mjini London ambapo Nadal alishinda fedha hizo.
Duru ziliarifu kwamba kiini cha nyota hao wawili kukutana katika chumba kimoja ni chakula kilichoandaliwa katika hafla hiyo.
Hatahivyo kitu kilichowafurahisha wengi kulingana na wageni ni hatua ya Ronaldo kukubali kushindwa na kupewa kazi ya kuviosha vyombo vya Nadal alivyotumia kula.

Binti asema hapana kuasiliwa na Kim kardashia

Pink

kim kardashia


Mtoto aliyekuwa akiishi katika mazingira ya umasikini katika Nyumba ya kulea Watoto yatima nchini Thailand amefanya uamuzi wa kushangaza alipokataa ombi la Nyota maarufu duniani Kim Kardashian kumuasili kuwa sehemu ya familia yake.
Taarifa zinasema binti huyo alifurahi sana aliposikia milionea huyo anataka kumuasili, lakini alisisitiza kuwa anataka kusoma nchini Thailand akimtaka Kim kuisaidia nchi yake na watoto wenzake wanaoishi pamoja katika nyumba ya watoto yatima.
Kim alivutiwa na binti huyu aitwae Pink mwenye umri wa miaka 13, alipotembelea nyumba ya watoto yatima katika Jimbo la Phang Nga,eneo ambalo zaidi ya watu 4,000 walipoteza maisha kutokana na Tsunami mwaka 2004.
Pink alipelekwa na mama yake katika nyumba ya kulelea watoto kwa kuwa hakuweza kumlea mtoto huyo na kugharamia elimu yake.
Binti huyu anasema yeye na Watoto wenzake walipokutana na Kim Kardashian hawakumfahamu yeye ni nani.
Pink ambaye jina lake halisi ni Laddawan Tong-Keaw, alifurahi kukutana na Nyota huyo, amesema na yeye anapenda sana kuonekana kwenye Televisheni.
Pink husafiri umbali wa Maili 100 kwa basi na Watoto wenzake wawili kwenda Shule inayoongoza jimboni humo inayomilikiwa na Serikali baada ya kufaulu mitihani yao kuingia shule hiyo.
Binti huyu huamka saa kumi na moja alfajiri na kurejea nyumbani saa kumi na mbili jioni.

Alhamisi, 20 Novemba 2014

AFARIKI AKIFANYA MAPENZI KWENYE GARI


Polisi mkoani Kagera inachunguza kifo cha mmiliki wa ukumbi wa klabu ya usiku ya Linas Night, Leonard Mtensa (50) ambaye inadaiwa alifariki dunia wakati akifanya mapenzi kwenye gari lake.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alisema Mtensa, ambaye alikuwa na mpenzi wake kwenye gari maeneo ya Buyekera, alifariki dunia kabla ya kufikishwa kituo cha afya cha ELCT Ndolage.

Alisema binti waliyekuwa naye kwenye gari anatokea mkoani Mara na kwamba tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana. Alisema baada ya gari lake kupekuliwa, vilikutwa vinywaji mbalimbali.

“Baada ya upekuzi ndani ya gari lake, vilikutwa vilevi vya aina mbalimbali, ikiwamo whisky aina ya Bond 7 aliyokuwa anakunywa, lakini chanzo cha kifo hicho hakijajulikana,” alisema Mwaibambe.

Kamanda Mwaibambe alisema polisi wanamshikilia mpenzi wake kwa ajili ya upelelezi kwa hatua zaidi. Kifo hicho kimeshtua wakazi wa Bukoba, kutokana na mazingira ya kifo cha mfanyabiashara huyo anayemiliki ukumbi pekee mjini hapa unaotoa burudani hadi asubuhi.
SOURCE:MWANANCHI