.

Alhamisi, 21 Novemba 2013

"Nimekuta Chupi ya kike kwenye chumba cha Boyfriend wangu, yeye anadai hajui ilipotokea, Nifanyeje?".....Mdau


Wadau hapa nilipo nimechanganyikiwa na nisijue cha kufanya, naombeni ushauri wenu, nilikwenda field huko Tabora, nikamwacha mchumba wangu Tanga(ndiko kwetu) tulikuwa tukiwasiliana kama kawaida, na niliondoka nikiwa nimeshavishwa pete.

Nilipigiwa simu baba yangu ni mgonjwa sana, watoto wake wote tulio mbali, tunatakiwa kurudi Tanga, basi nami nilirudi, na kukuta kweli hali ya baba si nzuri, nikampigia simu mchumba wangu kumuuliza yuko wapi, ili tukutane nae hospitali, akasema kwamba amesafiri kikazi gafla kwa siku moja tu then kesho yake angegeuza, nikamuuliza inakuwaje huniambii, akasema nimesafiri gafla, hata hivyo nilitaka nikujulishe maana nimeondoka leo.
Niliumia sana kwa alichokifanya, sasa kuna rafiki yangu mmoja akaniambia, mbona mimi nimemuona jana super market? Akiwa na msichana? Nilijisikia huzuni sana ila nilijipa moyo

nilikwenda moja kwa moja hadi kwake, nikamkuta mtoto wa mwenye nyumba, nikamuuliza kama kweli mchumba wangu amesafiri,(nikajua labda alikwenda supermarket kununua vitu vya safari) akasema mbona yupo? Na asubuhi nimemuona?, nikampigia simu kuwa nipo pale kwake, akasema atachelewa sana kurudi, hivyo nirudi nyumbani kesho ndio nije, nikamwambia namsubiri, ilifika saa sita mimi niko mlangoni nimekaa namsubiri, aliponikuta nimesinzia mlangoni alishtuka sna, na kuanza kunifokea kwanini nisingesubiri hadi kesho.

Ile naingia tu! Ndani, nikakutana na sandols za kike, na kwenye mto kuna chupi ya kike, niliumia na kuanzisha ugomvi mkubwa,

Kinachonishangaza eti anasema yeye mwenyewe hajui ni vya nani, itakuwa mama mwenye nyumba mchawi, maana alikuwa anamtaka, na bado anasisitiza eti ananipenda na anataka nifunge nae ndoa mwezo wa tisa.

Sasa mimi hata sijui nifanyaje, naombeni ushauri wenu?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni