.

Jumamosi, 28 Juni 2014

Hawa Ndiyo Washindi Wa Tuzo Za Watu Zilizotolewa Siku Ya Jana..!! Diamond, Salama Jabil Na Salim Kikeke Wang'ara...!!


Tuzo za watu za Tanzania au Tanzania People’s Choice Awards zimetolewa Ijumaa hii kwenye ukumbi uliopo Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Jumla ya vipengele 11 vilikuwa vinashindaniwa. Mshindi katika kila kipengele ameibuka na zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na trophy. Host wa tuzo hizo alikuwa mtangazaji mkongwe wa radio, Jimmy Kabwe.


WASHINDI
1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA
Millard Ayo – Clouds FM
2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA
Amplifaya – Clouds FM
3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA
Salim Kikeke – BBC Swahili
4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA
Mkasi – EATV
5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA
Juma Kaseja – Yanga
6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA
Nisher
7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME
My Number – Diamond
8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE
Yahaya – Lady Jaydee
09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
King Majuto
10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
Elizabeth ‘Lulu’ Michael
11. FILAMU INAYOPENDWA
Ndoa Yangu

HATIMAYE FLORA MBASHA A MUMEWE WAPATANA RASMI...HAWA HAPA WAKIFUNGUKA...!

  Mume wa Flora Mbasha, Bw. Emmanuel Mbasha.
HAKUNA neno zuri la kusema zaidi ya Mungu mkubwa! Ule mtafaruku ndani ya ndoa ya mwimba Injili mahiri Bongo, Flora na mumewe, Emmanuel Mbasha umedaiwa kumalizika kwa wawili hao kupatana, Risasi Jumamosi linakuwa nambari wani kukuhabarisha.

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, wawili hao walikalishwa kikao cha upatanishi mapema wiki hii kilichokuwa chini ya familia.



 MANENO YA CHANZO
“Kikao cha familia kilikaa, Mbasha aliitwa akafika, Flora naye aliitwa akatokea, mazungumzo yalikuwa marefu lakini kimsingi waliamua kuweka kando mtafaruku wao na kuijenga upya ndoa yao,” kilisema chanzo.
 

Chanzo kiliongeza kuwa katika kikao hicho cha mwanzoni mwa wiki hii, miongoni mwa adidu za rejea ilikuwa kutokumbushia vikao vilivyopita ambapo hakukupatikana muafaka. 

VIKAO VILIVYOPITA
Katika vikao vilivyopita, wahusika wakuu walikuwa wazazi wa Mbasha (mzee Maneno Mbasha, Zulfa Maneno), ndugu wa Flora na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.


Mwimbaji Injili mahiri Bongo, Flora Mbasha.
VIKAO VYA BAADAYE
Kwa mujibu wa chanzo, vikao vilivyofuata, wawili hao wakawa tayari kila mmoja ametema nyongo yake pembeni na kufikia makubaliano kwamba, ndoa yao isimame tena wakitumia maandiko kwenye Biblia kutoka kitabu cha Waebrania yanayosema:    Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
 

WAKORINTHO YAFUNGA KAZI
Kwa mujibu wa chanzo hicho, maneno mengine ya Biblia yaliyotumika kwenye kikao hicho mpaka wawili hao wakaamua kurudiana ni 1 Wakorintho 7:1-10 ambapo maandiko yanasema:
Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.


Flora Mbasha akiwa kwenye picha ya pamoja na mumewe, Emmanuel Mbasha.
Mke hana amri juu ya mwili wake bali mumewe vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake bali mkewe. Msinyimane, isipokuwa mmepatana kwa muda ili mpate faragha kwa kusali, mkajiane tena shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza, wala hapo si mimi, ila Bwana (Mungu), mke asiachane na mumewe, lakini ikiwa ameachana naye na akae asiolewe au apatane na mumewe, tena mume asimwache mkewe. 

KIKAO CHA JUMAMOSI KUMALIZIA
Chanzo kilisema kuwa, kikao cha mwisho ambacho kitamalizia kuweka mambo sawa ili wawili hao waanze ngwe ya pili ya ndoa yao ambayo inaaminika itakuwa ya mwisho mpaka kifo kiwatenganishe, kinatarajiwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam mahali ambapo hapakutajwa.


Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
MWANASHERIA ATAJWA
Mwanasheria wa Flora aliyejulikana kwa jina moja la Ado ametajwa kusimamia kikao hicho ili wawili hao waanze maisha mapya baada ya safari fupi ya mvurugano uliowafanya kuwa mbalimbali.
 

AONGEA NA RISASI JUMAMOSI
Juzi, Risasi Jumamosi lilimsaka mwanasheria huyo kwa njia ya simu yake ya mkononi ili kumsikia anasemaje kuhusu kutajwa kwenye usuluhishi wa ndoa hiyo ambapo alipopatikana alisema:
“Niko Arusha, Ijumaa nitarudi Dar. Kuhusu kikao cha usuluhishi siwezi kukwambia lakini suala la kuwapatanisha nalifahamu, nawaomba na ninyi msaidie kufanikisha jambo hilo zuri.”
 

VIPI KUHUSU KESI YA MADAI YA KUBAKA?
Hata hivyo, Wakili Ado hakutaka kugusia kuhusu kesi ya Mbasha iliyopo Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo anadaiwa kumbaka shemejiye mara mbili (jina tunalo) ambayo kwa mujibu wa mahakama, upelelezi umekamilika na itasikilizwa Julai 17, mwaka huu.
 

KWA UPANDE WAKE FLORA
Risasi Jumamosi lilimwendea hewani, Flora ili kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa upatanishi kati yake na mumewe, Emmanuel.

Huyu hapa: “Ongea na wakili wangu atakwambia kila kitu.” Ambapo majibu ya wakili yalikuwa: ”Ninachojua mimi ni kwamba Flora ameshamsamehe mumewe na yuko tayari kuanza ukurasa mpya.” 

MBASHA SASA
Kwa upande wake, Mbasha alipozungumza na gazeti hili juzi alisema kurejea upya kwa ndoa yake ni jambo la kuupendeza moyo wake.

“Mimi sina neno nipo tayari, nimeshasamehe yaliyotokea, Flora ni mke wangu jamani, nampenda sana kutoka moyoni.”

Ijumaa, 27 Juni 2014

WAKUBWA TUUU...!!! Angalia hapa picha za uchi za wanafunzi wa chuo maarufu hapa nchi hii ni aibu kubwa kwa taifa





Baadhi ya madenti wa vyuo vikuu mbalimbali jijini Dar es Salaam, wameoza kwa matukio machafu ya ngono.
Katika uchunguzi wa muda mrefu, Inaonyesha kuwa kuna kamtindo ka wanafunzi kufanya mapenzi ndani ya hostel zao huku wakijirekodi na kupiga picha chafu na za aibu na wengine hata kuuza miili yao ili kukidhi hali ngumu ya maisha iliyopo vyuoni

Data zilizokamilika zilionesha kuwa wanafunzi hao waliojulikana kwa jina mojamoja ni Maya mwenye umri wa miaka 19, anayesoma katika chuo maarufu cha mahesabu, Raya anayebukua masomo ya Information Technology (IT) na mwingine ambaye jina lake na chuo anachosoma havikupatikana.

Habari zilidai kuwa Raya na rafiki zake watatu wamekuwa wakijihusisha na vitendo haramu vya ngono rejareja na mwanaume mmoja wakiwa katika hosteli hiyo kwa kigezo cha mshiko ‘mnene’ wanaochuma kwa jamaa huyo.

Hata hivyo, ripoti ya uchunguzi wetu haikufanikiwa kuwanasa wakimhudumia mwanaume huyo kwa mpigo, isipokuwa ilifuma picha ambazo kila mmoja yuko na jamaa huyo kwa nyakati tofauti.
Baada ya kunasa picha hizo chafu kupita maelezo kwa jamii ya Kitanzania, wapekuzi wetu waliwatafuta wahusika ambapo walifanikiwa kumpata Raya ambaye pamoja na kuelezwa kuwa kuna ushahidi wa picha, alikana kuzifahamu.

Mbali na matukio hayo yaliyosheheni katika makabrasha yetu, uchunguzi ulibaini kuwa, siyo kila mwanachuo anayepata nafasi hiyo adimu ya kujiunga na elimu ya juu anafanya kile kilichokusudiwa, badala yake wanafanya kinyume kwa kujihusisha na vitendo haramu na hatarishi vya ngono.

Imebainika kuwa wanaoishi hosteli ndiyo wanaoongoza kwa uchafu huo kwa sababu wana uhuru wa kufanya hivyo bila kubanwa hivyo kugeuza vyumba vyao madanguro.

Katika uchunguzi wetu, ilibainika pia kuwa idadi kubwa ya wasichana wanaojiuza katika viunga mbalimbali jijini Dar ni wanafunzi wa vyuo vikuu wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili kwa wanaume ili kukidhi mahitaji ya kila siku kuendana na mfumuko wa bei.

Wakijitetea kwa sharti la kutotajwa , madenti wa vyuo walionaswa wakijiuza katika eneo la Sinza Afrika Sana, Dar hivi karibuni, walidai tatizo ni Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ambayo haiwapi fedha za kutosha.


UPDATE: Binti aliyeasi dini ya kiislamu Nchini SUDAN na kuolewa na Mkristo aachiwa huru tena…!


Mwanamke wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa madai ya kuasi dini ya kiislam ameachiliwa huru baada ya kushikiliwa kwa mara ya pili.
Meriam Ibrahimu alikwenda katika ubalozi wa Marekani uliopo mji Mkuu wa Khartoum. Mumewe ana asili ya Sudan Kusini lakini kwa sasa ni raia wa Marekani.
 
Mwanamke huyo aliachiliwa baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifo siku ya jumatatu lakini alishikiliwa tena na polisi kwa tuhuma za kughudhi hati za kusafiria ili aondoke nchini Sudan kwenda Marekani.
Meriam Yehya Ibrahim Ishag aliadhibiwa kwa makosa mawili, zinaa na kuasi dini
Meriam Yehya Ibrahim Ishag aliadhibiwa kwa makosa mawili, zinaa na kuasi dini
 
Kufuatia kuachiliwa huru kwa mara nyingine, Mke huyo wa Ibrahim ameiambia BBC kwamba ataendelea kuwa Mkristo.
Kesi yake ya kuasi dini imevuta hisia za watu wengi wakiwemo watetezi wa haki za binadamu pamoja na nchi za Magharibi

Amina Maige akana Shitaka la kumchoma Pasi na Kumng’ata Hausigeli wake


Mkazi wa Mwananyamala, Amina Maige(42) anayetuhumiwa kumng’ata mfanyakazi wake wa ndani,  amepandishwa kizimbani kusomewa maelezo ya awali baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.
 
Amina  alisomewa maelezo hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mbele ya Hakimu Yohana Yongolo.
 
Wakili wa Serikali Tumaini Msikwa alidai kati ya Januari na Juni mwaka huu, maeneo ya Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni, Maige alimng’ata Yusta Kashinde(20) sehemu  mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu.

Mshitakiwa alikana maelezo aliyosomewa na kwamba aliiomba mahakama kumpatia dhamana.
maige1
 
Wakili Msikwa aliiambia mahakama kuwa dhamana ya mshitakiwa imezuiliwa kama awali kwa kuwa bado  wananchi wana hasira hivyo kuhofia usalama wake.
maige Hakimu Yongolo alisema shauri hilo litaanza kusikilizwa  Julai 10 mwaka huu.

SASA UNAAMBIWA KITALE NA PENNY AKUNA SIRI TENA

KITALE

Msanii wa filamu za vichekesho, Kitale, ambae kwa sasa anatambulika zaidi kwa jina la ‘Mkude Simba’ amekanusha kuwa hajawai kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Vj Penny ambae aliwai kuwa mpenzi wa zamani wa Diamond.
PENNY
Kitale akizungumza Global TV
hivi karibuni ,amekanusha uvumi huo, ambao uliambatana na picha  zinazo muonyesha Penny   akimbusu Kitale.
KITALE
“Penny mimi sina mahusiano nae yoyote, siyo kweli sina mahusiano nae , mimi nina ndoa yangu na nina mke wangu na nina mtoto, naiheshimu ndoa yangu”Alisema Kitale.

MWANAFUNZI WA CHUO DODOMA ALIYEPIGA PICHA CHAFU ASEMA MBONA WEMA SEPETU NAE AMEPIGA PICHA UTATA NA WATU HAWASEMA SANA



Loveness Kaaya mwanafunzi wa chuo kimoja Mkoani Dodoma.
Mwanafunzi wa chuo mkoani Dodoma aliyefahamika kwa jina la Lovess Kaaya ambae anasoma chuo kimoja maarufu mkoani hume ameibuka na kusema picha yake  aliyovuja kwenye mtandao kwa bahati mbaya anashangaa wa2 wanatoa macho na kusema mengi wakati Wema Sepetu nae aliwahi kupiga picha za aina kama yake lakini watu hawakusema kivile....!
CREDIT XDEEJAYZ TANZANIA

MZEE WA KANISA AIBIKA, AKUTWA AKICHEPUKA NA KABINT KADOGO SANA KWENYE NYUMBA ZA WAGENI

Tumekwisha! Mzee wa kanisa la kiroho (jina linahifadhiwa kwa sasa), aliyetajwa kwa jina la Luca Pesa, mkazi wa Segerea, Dar, ameaibika baada ya kukurupushwa kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti) akidaiwa kutaka kuvunja amri ya sita na binti ambaye ni msanii chipukizi wa filamu za Kibongo,
Debora Jacob, Ijumaa lina kisanga cha aina yake.

Mzee wa kanisa la kiroho aliyetajwa kwa jina la Luca Pesa,
HABARI KAMILI
Tukio hilo ambalo kamwe Luca hawezi kulisahahu maishani mwake, lilijiri kwenye gesti hiyo iliyopo karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Segerea, Dar, Jumanne iliyopita huku mzee huyo akishushiwa tuhuma nzito ya rushwa ya ngono kwa vibinti chini ya miaka 18.

Katika tukio hilo, mzee huyo wa kanisa na msanii huyo wa Kundi la Maigizo la Vivif lenye maskani yake maeneo hayo walikuwa wamejichimbia kwenye gesti hiyo katika chumba ambacho mlangoni kilikuwa kimeandikwa Rombo kabla ya kuchomolewa na kufikishwa kanisani kisha polisi.
TUHUMA NZITO
Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, ikiwa kwenye mingo zake, ilipokea simu kutoka kwa dada aliyejitambulisha kwa jina moja la Diana na kujieleza kuwa anatoka kundi la sanaa za maigizo la Vivif lililopo Segerea jijini Dar.

OFM: Ndiyo hujakosea unazungumza na
OFM, tukusaidie nini?
Diana: Kuna mzee wa kanisa la kiroho la (anataja jina la kanisa hilo) lililopo maeneo ya Segerea, aliomba kuwa mfadhili wa kundi letu.

Akiwa kwenye geti la kanisa.
Tulimkubalia na baada ya muda alianza kutumia fedha zake vibaya kwa kufanya vitendo visivyofaa.
OFM: Vitendo gani visivyofaa?
Diana: Anawarubuni mabinti wadogo anawaweka kambini na kula nao tunda tamtam eti ndiyo tiketi ya kuchezeshwa kwenye maigizo.
OFM: Tiririka!

Diana: Yaani hadi muda huu ninapozungumza na ninyi mzee huyo wa kanisa anachati na msanii mwingine wa kundi hilo. Anaitwa Debora anataka waende kwenye gesti fulani wakanogeshane, wahini tayari mtego umewekwa utafyatuka muda wowote.
UDHALILISHWAJI?
Diana alisema baada ya Debora kuombwa ‘mambo’ ndipo akawataarifu wasanii wenzake na kuwataka wote kwa pamoja waungane kuikomesha tabia hiyo chafu ya Luca anayelichafua kanisa la kiroho na kulidhalilisha kundi lao la sanaa.

OFM MZIGONI
Baada ya kuseti kila kitu, Diana aliiomba OFM iambatane nao kwani muda huo tayari Debora alishatangulia kwenye gesti hiyo kumfuata mzee huyo wa kanisa ambaye alishachukua chumba.

.....akitaitiwa.
Taarifa hiyo ilipokelewa kwa mikono miwili na kiongozi wa OFM ambaye aliwaagiza vijana wake makini ambao walisitisha kazi nyingine za kiintelijensia kisha kuelekeza nguvu zao eneo la tukio.
Vijana hao walitumia pikipiki zao ziendazo kasi ambapo baada ya muda usiozidi dakika ishirini walikuwa wamefika kwenye gesti hiyo.

ENEO LA TUKIO
OFM walipofika eneo la tukio, walikuta kundi la wasanii hao wakimchomoa gesti mzee huyo wa kanisa ambaye aliruka ukuta na kudondokea kwenye matuta ya viazi.

Akiwa anajizoazoa kwenye matuta hayo, kundi la wasanii hao lilimuunganishia ambapo kabla ya kumnasa aliingia kwenye chumba cha nyumba iliyopo jirani na gesti hiyo ili kujisalimisha.
Hata hivyo, zoezi lake lilifeli baada ya wasanii hao kumtahadhalisha mwenye nyumba hiyo kuwa wanamtaka mtuhumiwa wao la sivyo wangeichoma moto.

Baada ya kuzingirwa na wasanii hao huku akihatarisha maisha yake kwa kuwa wasanii hao walikuwa na hasira, aliona yasiwe makuu akaamua kuwaruhusu wamtoe mtuhumiwa wao wakamalizane naye kanisani.
KABANG!
Alipotiwa mikononi, mzee huyo wa kanisa aliomba apelekwe kanisani ambapo hapakuwa mbali na eneo la tukio ili akahifadhi vitu vyake muhimu pamoja na kuomba ushauri.

APELEKWA MSOBEMSOBE KANISANI
Kundi hilo la wasanii lilimpeleka kanisani msobemsobe ambapo baada ya hatua kadhaa polisi walitokea na kuwadhibiti wananchi wenye hasira na wasanii waliotaka kumdhuru mzee huyo wa kanisa wakati akipelekwa kanisani.

Mtuhumiwa akitembezwa mtaani.
MTAANI WERAAA!
Wakiwa mitaani, njiani mabinti walikuwa wakipiga kelele ‘weraaa…ukomeee…’ huku wakifurahia kufunga mitaa kwa madai kwamba mzee huyo wa kanisa alizidi.
Katika sekeseke hilo, polisi hao walimtia pingu mzee huyo wa kanisa na kuongoza safari ya kuelekea kanisani.

Wakiwa kanisani hapo polisi walijitambulisha na kuwauliza wachungaji pamoja na waumini wa kanisa hilo kama walimfahamu mzee huyo wa kanisa.
BREKI YA KWANZA POLISI
Kundi la wazee pamoja na vijana wa kanisa hilo walikiri kuwa Luca ni mmoja wa wazee wa kanisa hilo ndipo polisi hao wakamruhusu kuwakabidhi baadhi ya vitu vyake ikiwemo simu na fedha kisha breki ya kwanza ikawa Kituo cha Polisi cha Tabata-Shule ambapo alifunguliwa jalada la kesi namba RB/3843/2014 -RUSHWA YA NGONO, KUWAWEKA KAMBI KINYUME CHA SHERIA WASICHANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 NA KUWADHALILISHA KIJINSIA.

Hadi OFM wanaanua jamvi kituoni hapo kanisa lilikuwa likihaha kumchomoa kwa dhamana akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.

MZEE WA KANISA AIBIKA, AKUTWA AKICHEPUKA NA KABINT KADOGO SANA KWENYE NYUMBA ZA WAGENI


Tumekwisha! Mzee wa kanisa la kiroho (jina linahifadhiwa kwa sasa), aliyetajwa kwa jina la Luca Pesa, mkazi wa Segerea, Dar, ameaibika baada ya kukurupushwa kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti) akidaiwa kutaka kuvunja amri ya sita na binti ambaye ni msanii chipukizi wa filamu za Kibongo, Debora Jacob, Ijumaa lina kisanga cha ai


Mzee wa kanisa la kiroho aliyetajwa kwa jina la Luca Pesa,
HABARI KAMILI
Tukio hilo ambalo kamwe Luca hawezi kulisahahu maishani mwake, lilijiri kwenye gesti hiyo iliyopo karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Segerea, Dar, Jumanne iliyopita huku mzee huyo akishushiwa tuhuma nzito ya rushwa ya ngono kwa vibinti chini ya miaka 18.

Katika tukio hilo, mzee huyo wa kanisa na msanii huyo wa Kundi la Maigizo la Vivif lenye maskani yake maeneo hayo walikuwa wamejichimbia kwenye gesti hiyo katika chumba ambacho mlangoni kilikuwa kimeandikwa Rombo kabla ya kuchomolewa na kufikishwa kanisani kisha polisi.
TUHUMA NZITO
Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, ikiwa kwenye mingo zake, ilipokea simu kutoka kwa dada aliyejitambulisha kwa jina moja la Diana na kujieleza kuwa anatoka kundi la sanaa za maigizo la Vivif lililopo Segerea jijini Dar.

OFM: Ndiyo hujakosea unazungumza na
OFM, tukusaidie nini?
Diana: Kuna mzee wa kanisa la kiroho la (anataja jina la kanisa hilo) lililopo maeneo ya Segerea, aliomba kuwa mfadhili wa kundi letu.

Akiwa kwenye geti la kanisa.
Tulimkubalia na baada ya muda alianza kutumia fedha zake vibaya kwa kufanya vitendo visivyofaa.
OFM: Vitendo gani visivyofaa?
Diana: Anawarubuni mabinti wadogo anawaweka kambini na kula nao tunda tamtam eti ndiyo tiketi ya kuchezeshwa kwenye maigizo.
OFM: Tiririka!

Diana: Yaani hadi muda huu ninapozungumza na ninyi mzee huyo wa kanisa anachati na msanii mwingine wa kundi hilo. Anaitwa Debora anataka waende kwenye gesti fulani wakanogeshane, wahini tayari mtego umewekwa utafyatuka muda wowote.
UDHALILISHWAJI?
Diana alisema baada ya Debora kuombwa ‘mambo’ ndipo akawataarifu wasanii wenzake na kuwataka wote kwa pamoja waungane kuikomesha tabia hiyo chafu ya Luca anayelichafua kanisa la kiroho na kulidhalilisha kundi lao la sanaa.

OFM MZIGONI
Baada ya kuseti kila kitu, Diana aliiomba OFM iambatane nao kwani muda huo tayari Debora alishatangulia kwenye gesti hiyo kumfuata mzee huyo wa kanisa ambaye alishachukua chumba.

.....akitaitiwa.
Taarifa hiyo ilipokelewa kwa mikono miwili na kiongozi wa OFM ambaye aliwaagiza vijana wake makini ambao walisitisha kazi nyingine za kiintelijensia kisha kuelekeza nguvu zao eneo la tukio.
Vijana hao walitumia pikipiki zao ziendazo kasi ambapo baada ya muda usiozidi dakika ishirini walikuwa wamefika kwenye gesti hiyo.

ENEO LA TUKIO
OFM walipofika eneo la tukio, walikuta kundi la wasanii hao wakimchomoa gesti mzee huyo wa kanisa ambaye aliruka ukuta na kudondokea kwenye matuta ya viazi.

Akiwa anajizoazoa kwenye matuta hayo, kundi la wasanii hao lilimuunganishia ambapo kabla ya kumnasa aliingia kwenye chumba cha nyumba iliyopo jirani na gesti hiyo ili kujisalimisha.
Hata hivyo, zoezi lake lilifeli baada ya wasanii hao kumtahadhalisha mwenye nyumba hiyo kuwa wanamtaka mtuhumiwa wao la sivyo wangeichoma moto.

Baada ya kuzingirwa na wasanii hao huku akihatarisha maisha yake kwa kuwa wasanii hao walikuwa na hasira, aliona yasiwe makuu akaamua kuwaruhusu wamtoe mtuhumiwa wao wakamalizane naye kanisani.
KABANG!
Alipotiwa mikononi, mzee huyo wa kanisa aliomba apelekwe kanisani ambapo hapakuwa mbali na eneo la tukio ili akahifadhi vitu vyake muhimu pamoja na kuomba ushauri.

APELEKWA MSOBEMSOBE KANISANI
Kundi hilo la wasanii lilimpeleka kanisani msobemsobe ambapo baada ya hatua kadhaa polisi walitokea na kuwadhibiti wananchi wenye hasira na wasanii waliotaka kumdhuru mzee huyo wa kanisa wakati akipelekwa kanisani.

Mtuhumiwa akitembezwa mtaani.
MTAANI WERAAA!
Wakiwa mitaani, njiani mabinti walikuwa wakipiga kelele ‘weraaa…ukomeee…’ huku wakifurahia kufunga mitaa kwa madai kwamba mzee huyo wa kanisa alizidi.
Katika sekeseke hilo, polisi hao walimtia pingu mzee huyo wa kanisa na kuongoza safari ya kuelekea kanisani.

Wakiwa kanisani hapo polisi walijitambulisha na kuwauliza wachungaji pamoja na waumini wa kanisa hilo kama walimfahamu mzee huyo wa kanisa.
BREKI YA KWANZA POLISI
Kundi la wazee pamoja na vijana wa kanisa hilo walikiri kuwa Luca ni mmoja wa wazee wa kanisa hilo ndipo polisi hao wakamruhusu kuwakabidhi baadhi ya vitu vyake ikiwemo simu na fedha kisha breki ya kwanza ikawa Kituo cha Polisi cha Tabata-Shule ambapo alifunguliwa jalada la kesi namba RB/3843/2014 -RUSHWA YA NGONO, KUWAWEKA KAMBI KINYUME CHA SHERIA WASICHANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 NA KUWADHALILISHA KIJINSIA.

Hadi OFM wanaanua jamvi kituoni hapo kanisa lilikuwa likihaha kumchomoa kwa dhamana akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.

WEMA SEPETU NA PENNY WAKUTANA USO KWA USO, NA HICHI NDICHO KILICHOTOKEA BAADA YA KUKUTANA


Katika hali isiyotarajiwa, mchumba wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Wema Sepetu na aliyewahi kuwa mchumba wa msanii huyo, Penniel Mungilwa ‘Penny’ walikutana studio na kila mmoja akamkwepa mwenzake.
 Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Posta, jijini Dar katika Studio za Amaya ambayo ni saluni inayotumika kurekodia vipindi mbalimbali vya Mkasi vinavyorushwa kupitia Runinga ya EATV.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mwigizaji Aunt Ezekiel alialikwa na mtangazaji wa kipindi hicho, Salama Jabir kwenda kufanya mahojiano, akaambatana na shosti wake Wema ndipo ghafla wakakutana na Penny ambaye naye alialikwa kwa wakati wake.
Chanzo kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya Aunt na Wema kufika studio hapo, Salama aliwakaribisha na wakaanza kurekodi kipindi hicho, lakini walipokuwa wakiendelea na mahojiano, Penny naye aliwasili bila kujua kama Wema alikuwepo.
“Penny alipofika alizama ndani na kukutana na Salama ambaye alimwambia kuwa kuna watu wanatoka ndani muda si mrefu hivyo wakati bado wanaongea, Wema na Aunt walitoka studio ambapo Penny alikimbilia kwenye gari lake kukwepa kuonana na Wema ambaye pia alionekana kutotaka kuonana na Penny,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Kwa kuwa Wema naye alimuona kwa mbali Penny, alimtaka Aunt waingie kwenye gari fastafasta na kuondoka eneo hilo.”
 Mapaparazi wetu baada ya kuunyaka mchongo huo, walimtafuta Penny ili kumsikia anazungumziaje ishu hiyo. Alipopatikana, alijibu hivi:
“Mimi sikumkimbia Wema na itambulike kuwa wakati naenda pale sikujua kama Wema alikuwepo hivyo nilifika na kusubiria muda wangu wa mahojiano nikiwa ndani ya gari, sikuwa na haja ya kujua Wema yupo ama la.”
Jitihada za kumpata Wema hazikuzaa matunda lakini alipotafutwa Aunt Ezekiel, alitiririka:
“Nilimuona Penny kweli pale studio ingawa mwanzo nilitahamaki maana sikujua kama naye alikuwa akisubiria tutoke aingie kwenye kipindi ila Salama alinishtua sana baada ya kusema kabla hatujatoka ndani tusubiri aandae uwanja wa ngumi, alitania.”
Wema na Penny wanadaiwa kuwa picha haziendi baada ya Wema kumtuhumu Penny ambaye alikuwa rafiki yake kuwa alimwibia Diamond wake kabla hawajamwagana na kurejea tena mikononi mwake

Ukraine,Georgia na Moldova watia sahihi


 
Rais Petro poroshenko katikati baada ya kutia sahih mkataba wa ushirikiano na ulaya.
Ukraine, Georgia na Moldova zimetia sahihi mikataba ya ushirikiano na muungano wa ulaya, swala ambalo Urusi inapinga vikali.
Makubaliano hayo ambayo yatayaunganisha pamoja mataifa hayo na kuyaegemeza Magharibi kiuchumi na kisiasa, haswa ndio msingi wa mgogoro ulioko Ukraine.
Urusi imesema kuwa hata ingawa kutia saini mkataba huo ni haki ya taifa lolote, kunaweza kuleta madhara mabaya baadaye.
Usitishaji wa vita kati ya vikosi vya serikali na waasi wanaounga mkono Urusi, mashariki mwa Ukraine, unakamilika Ijumaa hii.
Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko aliusifu mkataba huo akisema ni siku ya kihistoria katika taifa la Ukraine baada ya siku ya Uhuru wa taifa hilo mwaka 1991.
Ameutaja kuwa dalili ya imani na nia isiyoweza kuvunjwa.
Rais Poroshenko akitia sahihi makubaliano ya ushirikiano na ulaya.
Poroshenko pia amesema kuwa ameuona mkataba huo kama mwanzo wa mchakato wa kujiunga na Umoja wa bara Uropa,''Ukraine inadhibitisha chaguo lake la kitaifa, kujiunga na EU" alisema.
Kwengineko, rais wa Umoja wa bara Uropa, Herman va Rompuy ametaja kuwa "siku kuu kwa bara Uropa".
''Umoja wa bara Uropa unasimama pamoja nanyi, leo zaidi ya siku nyingine yoyote awali" aliwaambia viongozi wa nchi hizo tatu, akiongeza kuwa hakuna chochote katika mikataba hiyo ya makubaliano kitakachoiletea madhara Urusi kwa njia yoyote ile.
Naibu waziri wa maswala ya nje wa Urusi, Grigory Karasin ''ameliambia shirika la habari la Interfax kuwa hatua hiyo huenda ikazua madhara.
Kutiwa sahihi kwa mkataba huu muhimu, kwa hakika ni haki ya taifa lolote lile" alisema.
Ila tu matokeo ya Ukraine na Moldova kutia saini mkataba huu bila shaka yatakuwa mabaya".
Mapema, mshauri mkuu wa Kremlin, Sergei Glazyev alimtaja Poroshenko kuwa mwanachama wa Nazi na kuwa uchaguzi wake kuwa rais haukuwa wa haki kwani sehemu kubwa ya Ukraine haikupiga kura katika uchaguzi wa mwezi Mei.
Alizidi kusema kuwa Poroshenko hana haki kikatiba kutia sahihi mkataba huo, jambo ambalo litadhuru uchumi wa Ukraine

Iraq:Serikali mpya kushirikisha wasunni



Waziri mkuu nchini Iraq Nouri al Malik
Msemaji wa chama cha waziri mkuu nchini Iraq ameimbia BBC kwamba Nouri al Malik anajaribu kubuni serikali itakayoshirikisha kila mmoja ikiwemo watu wa dhehebu la kisunni walio na msimamo wa kadri.
Zuhair al Nahar amesema kuwa waziri mkuu alitaka kufungua awamu mpya katika siasa za iraq lakini akasistiza kuwa hatazungumza na kundi lolote lenye silaha ambalo linakabiliana na serikali.
Msemaji huyo ameongezea kuwa bwana Al Malik ana jukumu kubwa mbeleni na kwamba hatajiuzulu.
Kuhusu kampeni dhidi ya wanamgambo wa kisunni ,bwana Al Nahar amesema kuwa ana matumaini kuwa mashambulizi ya angani ya Marekani yatapunguza makali ya wapiganaji wa ISIS huku vikosi vya serikali vikiwakabili waasi hao.
Wapiganaji wa kisunni wa kundi la ISIS
Wakati huo huo, shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch, limesema kuwa kundi la wanamgambo wa kiislamu la ISIS huenda limewaua kati ya wanajeshi mia moja sitini na mia moja tisaini, wa Iraq, kufuatia hatua yao ya kuuteka mji wa Tikrit mapema mwezi huu.
Shirika hilo limesema haya kufuatia uchunguzi wao wa picha za satelaiti na pia picha za mitaro miwili iliyojaa miili ya binadamu.
Shirika hilo bado halijatembelea mji huo kuhakikisha madai hayo lakini limekubali kuwa idadi ya waathiriwa yaweza kuwa kubwa zaidi.
Kundi la ISIS liliweka picha hizo kwenye mtandao

Obama aomba pesa awasaidie waasi



Rais Barack Obama wa Marekani
Rais wa Marekani, Barrack Obama ameliomba Bunge la Congress kiasi cha dola milioni mia tano kwa ajili ya kugharamia mafunzo na kuwapatia silaha Waasi wa Syria.
Bado haijajuliakana ni aina gani ya msaada wa kijeshi ambao Marekani itautoa japo kulikuwa na maombi ya waasi hao wa Syria kuhusu kupewa makombora ya kubeba ya kutungulia ndege ambayo yalitupiliwa mbali kwa kuhofia silaha hizo zisiwaendee wanamgambo wa makundi ya kigaidi.
Ikiwa Bunge hilo litaridhia Ombi la Rais Obama,hii itakuwa mara ya kwanza kwa Jeshi la Marekani kujihusisha moja kwa moja kwenye mgogoro wa Syria, mashirika ya kiintelijensia ya Marekani tayari yanawasaidia waasi nchini Syria.
Waasi wa Syria wanapambana na wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa ISIS, ambalo ni kundi la waislamu ambao pia wameteka mpaka ndani ya nchi ya Iraq.

Alhamisi, 26 Juni 2014

CHUKU MUDA WAKO KUANGALIA PICHA ZA WATU WAWILI WANAOZANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WALIOUAWA JAN

Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha ya bunduki aina ya SMG na bastola waliokuwa wakitumia pikipiki aina ya sanlg yenye namba T460 CVQ wamevamia duka la mpesa na kumuua mfanyabiashara Gosbert Kulwa(59) mkazi wa tambukaleli mjini Geita. 

Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni katika eneo la benki ya NMB ambapo majambazi hao walimpiga risasi ya tumboni mfanyabiashara huyo wa mpesa na kufariki dunia wakati akipata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Geita.
Amesema mauaji hayo yalifanyika baada ya majambazi hao kupora kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kutoka kwa mfanyabiashara huyo.

Kamanda ameongeza kuwa kabla hawajamuua Gosbert walianzia kwenye duka la mfanyabiashara wa vinywaji ndugu Ignas Athanas na walichukua pesa kiasi ambacho hakijafahamika na   kuchukua bastola aina ya H PIETRO BERRETA HO4788Y CAR 5808 ikiwa na risasi 12 mali ya mfanyabiashara huyo. 

Aidha majambazi hao waliokuwa na bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake na risasi 13 na simu ya mkononi aina ya TECNO huku wakiwa wamevalia makoti meusi na helment ili kuficha sura zao zisitambulike kwa urahisi.

Jeshi la polisi lilipata taarifa muda mfupi zilizotolewa na raia wema ambapo kamanda wa polisi akiongoza kuwafuatilia majambazi hao walifanikiwa kuwakuta katika pori lililopo jirani na kijiji cha Ibambila wilayani Nyangh’hwale zaidi ya km 50 kutoka mjini Geita walipofanya uharifu.

Wakiwa wanakimbizana majambazi hao walipowaona askari jambazi mmoja aliyekuwa na silaha aliruka kwenye pikipiki na kuanza  kuwashambulia askari kwa risasi lakini dereva wa porisi alimfuta moja kwa moja na kumgonga kwa gari jambazi huyo na kufariki hapo hapo.

 Baada ya hapo jambazi mwingine alikimbia kwa pikipiki na askari wakaanza kumfukuza wakishirikiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Nyang’hwale na kufanikiwa kumkamata na kuanza kumshambulia na alifariki wakati anakimbizwa kupelekwa hospitali.

Taharuki hiyo iliyokuwa imeikumba mji wa Geita kwa masaa takribani 3 kabala hawajakamatwa majira ya saa2 baadhi ya wananchi wamelipongeza jeshi la polisi kwa kazi waliyoifanya kwa mda mfupi mara baada ya tukio hilo huku kamanda Konyo akiendelea kuwaasa wananchi wazidi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuimarisha amani katika mkoa huo.

Rick Ross ameuchoka unene, aamua kuingia Gym tayari amepunguza kilo 45.


rozay Rick Ross kila mtu anamjua kuwa na mwili mkubwa lakini hivi sasa ameamua kupugua kabisa. Mwenyewe anasema kwamba ameamua kujiweka fit na bado anakula anachokitaka lakini huwa anaenda gym kufanya mazoezi na ameshapunguza kilo 45.
rozay2

Picha 11 za Mzee Majuto, Timoth Conrad na wengine kwenye movie mpya Kenya. Posted by: Millard Ayo June 24, 2014 Ent. 5 Sabby Angel na Mzee Majuto. Director Timoth Conrad ambae ujuzi wake umetumika kwenye movie kadhaa za Tanzania ikiwemo ‘Mdudiko’ amehusika tena kuidirect movie mpya inayofanywa Mombasa na kuwashirikisha waigizaji mbalimbali akiwemo mchekeshaji Mzee Majuto. Movie hii iitwayo ‘Riziki’ inawashirikisha pia wakali wengine kama Mwigizaji Tino Muya, Sabby Angel, Dude hao wakiwa ni Watanzania ambapo kwa upande wa Kenya watahusika Penelorp Immaculate, Julie, Elizabeth Bana, Lavinah Wanjiku na Dominick Leo huku assistant actor akiwa ni Hassan Faisal ambae pia ni diretor maarufu nchini Kenya. 4Stori ya movie inamuhusu msichana wa Kikenya aliyekua akiishi Uingereza na kukopi tabia na tamaduni za huko ambapo baadae akajikuta kwenye mazingira magumu aliporudi nyumbani Afrika. Inakua ngumu kwake kwenye mapenzi pia na hata wa kumuoa inakua tabu kupata kwa sababu ya kukosa heshima kwa Wanaume na kutaka kuwa juu yao kimaamuzi. 3Hii ni movie ya Sabby Angel mrembo Mkenya anaeonekana kwenye hizi picha ambae ni amekua akifanya kazi Tanzania pia na kama una kumbukumbu aliwahi kuonekana kwenye movie ya ‘Hard price’ ya Ray na sasa ameanza kufanya kazi zake mwenyewe. 2 1 6 7 8 11 9 10 Director Timoth Conrad akiwa na waigizaji Tinno na Mzee Majuto. Kila kinachonifikia ni halali yako kukipata mtu wangu! ili niwe nakutumia moja kwa moja kwenye ukurasa wako wa twitter instagram na facebook jiunge na mimi kwa kubonyeza hapa

Picha 11 za Mzee Majuto, Timoth Conrad na wengine kwenye movie mpya Kenya.

5
Sabby Angel na Mzee Majuto.
Director Timoth Conrad ambae ujuzi wake umetumika kwenye movie kadhaa za Tanzania ikiwemo ‘Mdudiko’ amehusika tena kuidirect movie mpya inayofanywa Mombasa na kuwashirikisha waigizaji mbalimbali akiwemo mchekeshaji Mzee Majuto.
Movie hii iitwayo ‘Riziki’ inawashirikisha pia wakali wengine kama Mwigizaji Tino Muya, Sabby Angel, Dude hao wakiwa ni Watanzania ambapo kwa upande wa Kenya watahusika Penelorp Immaculate, Julie, Elizabeth Bana, Lavinah Wanjiku na Dominick Leo huku assistant actor akiwa ni Hassan Faisal ambae pia ni diretor maarufu nchini Kenya.
4Stori ya movie inamuhusu msichana wa Kikenya aliyekua akiishi Uingereza na kukopi tabia na tamaduni za huko ambapo baadae akajikuta kwenye mazingira magumu aliporudi nyumbani Afrika.
Inakua ngumu kwake kwenye mapenzi pia na hata wa kumuoa inakua tabu kupata kwa sababu ya kukosa heshima kwa Wanaume na kutaka kuwa juu yao kimaamuzi.
3Hii ni movie ya Sabby Angel mrembo Mkenya anaeonekana kwenye hizi picha ambae ni amekua akifanya kazi Tanzania pia na kama una kumbukumbu aliwahi kuonekana kwenye movie ya ‘Hard price’ ya Ray na sasa ameanza kufanya kazi zake mwenyewe.
2
1
6
7
8
11
9
10
Director Timoth Conrad akiwa na waigizaji Tinno na Mzee Majuto.
Kila kinachonifikia ni halali yako kukipata mtu wangu! ili niwe nakutumia moja kwa moja kwenye ukurasa wako wa twitter instagram na facebook jiunge na mimi kwa kubonyeza hapa

Bow Wow abadilisha jina tena…lijue jina na sababu ya kubadilisha.


bow
Mwaka 1993 alipewa jina la Lil Bow Wow na Snoop Dogg, ikafika mwaka 2002 akabadilisha jina kujiita Bow Wow kwa sababu aliyosema amekuwa mkubwa na sio Lil tena.
Hivi sasa amesema ikipita BET awards ataacha kutumia jina la Bow Wow na kutumia jina lake halisi la Shad Moss.
Kupitia video ya instagram alisema,”After BET awards I will no longer go by Bow Wow. Im going by my real name Shad Moss we made a lot of history as bow wow. Now its time for the next chapter and challenge.”
Aliendelea kutoa sababu ya kubadilisha hilo jina alisema,“Bow wow does not fit who i am today. Ima father, business man, TV host, Actor, and rapper! Time for MR Moss to take over!”
Bow Wow hivi sasa ana miaka 27 na BET awards zitafanyika June 29 na baada ya hapo ataanza kuitwa Shad Moss

Hukumu iliyotolewa na Mahakama moja Misri dhidi ya Wanahabari watatu wa shirika la Televisheni Aljazeera yakosolewa kimataifa


Waandishi wa Habari wa Kituo cha Al Jazeera
Waandishi wa Habari wa Kituo cha Al Jazeera
AFP/Khaled Desouki
Na Ruben Kakule Lukumbuka
hii leo Katka Mjadala wa Wiki tunazungumzia hukumu iliyotolewa na mahakama moja ya Misri dhidi ya waandishi watatu wa Al Jazeera kifungo cha miaka saba jela kwa mashitaka ya kuwaunga mkono Muslim Brotherhood chama kilichopigwa marufuku nchini Humo, kesi ambayo imelaaniwa kimataifa.
Nikumbushe tu kwamba Waandishi hao watatu waliohukumiwa mjini Cairo ni pamoja na raia wa Australia Peter Greste , raia wa Canada mwenye asili ya Misri Mohamed Fahmy na raia wa Misri Baher Mohamed ambaye alihukumiwa miaka mitatu zaidi kwa makosa mengine.
Ungana nami Reuben Lukumbuka, kusikiliza Makala haya,...............

Gavana wa Kaunti ya Lamu nchini Kenya akamatwa kutokana na mauaji ya Mpeketoni

Issa Timamy Gavana wa Kauti ya Lamu
Issa Timamy Gavana wa Kauti ya Lamu
Daily Nation

Na Victor Melkizedeck Abuso
Polisi nchini Kenya wamemkamata na kumzuia Gavana wa Kauti ya Lamu Issa Timamy kwa tuhma za kuhusishwa na mauaji ya zaidi ya watu 60 katika mji wa Mpeketoni na vitongoji vyake Juma lililopita.

Mkuu wa idaya ya makosa ya Jinai nchini humo Ndegwa Muhoro amethibitisha kukamatwa kwa Gavana huyo siku ya Jumatano na anatarajiwa kufikishwa Mahakamani siku ya Alhamisi.
Haijafahamika vema ni makosa gani Gavana huyo anatuhumiwa kuyafanya.
Juma hili watu wengine 11 waliuliwa na watu wasiojulikana katika Kaunti hiyo ya Lamu, juma moja tu baada ya mauaji ya zaidi ya watu sitini katika eneo la Mpeketoni.
Kundi la kigaidi la Al-Shabab nchini Somalia limekiri kutekeleza mauaji haya yote kutokana na jeshi la Kenya kuwa Somalia lakini serikali ya Kenya imesema mauaji hayo yalipangwa na kuchochewa kisiasa.
Rais Uhuru Kenyatta ameonya kuwa watu wote wanaoshukiwa kupanga na kutekeleza mauaji hayo yaliyolenga jamii ya Kabila moja iliyohamia katika eneo hiyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Watu waliopoteza maisha Mpeketoni
Reuters
Upinzani nchini Kenya umekuwa ukiishinikiza wakuu wa usalama nchini humo kujiuzulu kwa kushindwa kuwalinda wakenya na kuwahakikishia usalama wao katika siku za hivi karibuni.
Inspekta wa Polisi David Kimaiyo alinukuliwa juma hili akisema hawezi kujiuzulu kwa kile alichokisema kuwa mauaji hayo yangezuiliwa kama sio kupangwa na kochechewa kisiasa.
Maeneo mengi ya Pwani nchini Kenya yamekuwa yakishuhudia mzozo wa ardhi kutokana na wenyeji wa eneo hilo kudai kuwa ardhi yao imenyakuliwa na wageni.

Benki ya Equity iliyochomwa moto katika mji wa Mpeketoni
REUTERS/Joseph Okanga
Kuzorota kwa usalama Pwani ya Kenya tangu mashambulizi ya kigaidi ya Al Shabab yalipoanza nchini humo umesababisha nchi ya Uingereza kufunga Ubalozi wake mdogo mjini Mombasa na kuwawaomba raia wake kutozuru Pwani ya Kenya.
Mataifa mengine ambayo pia yamewarai raia wake kuwa makini wanapozuru Pwani ya Kenya ni pamoja na Ufaransa na Marekani.

tags: Kenya - Uhuru Kenyatta - Kundi la Wanamgambo la Al Shabab