.

Jumamosi, 12 Oktoba 2013

VIDEO ya Majibu ya maswali aliyoulizwa Ney wa Mitego nakuhusu kufunguliwa kesi mahakamani


ney mitegoNey wa Mitego ameongea na AyoTV kuhusu aina ya nyimbo anazoimba zenye utata na kuwasema watu mbalimbali.
Cheki video au unaweza kusoma interview yote hapa ambayo Ney kazungumzia athari na kwanini hupendelea aina hiyo ya uandishi wa nyimbo zake.

Mara nyingi umekuwa mtu wa kutoa nyimbo za kuwasema watu, athari gani unazipata baada ya hizo nyimbo kutoka?
Ney : Athari ni pale ambapo wale watu ambao nimewazungumzia wanapanic, kila mtu anakuwa na maamuzi yake lakini kwangu mimi inakuwa sio athari kubwa kwasababu ninacholenga ni ujumbe ufike ndiyo muziki wa hiphop ulivyo, hiphop ni ukweli na kama unataka kutoa kitu ambacho kipo moyoni unataka ujumbe ufike.
Kuna faida kubwa sana kwa hiki ninachokifanya kwa sababu kuna mashabiki wengi nawapata hadi mimi mwenyewe napagawa.
AyoTV: Kuna vitisho gani unapata baada ya kutoa nyimbo zikiwasema watu na kuwaingilia kwenye maisha yao?
Ney: Vitisho vipo hasa muda huu ambao nimetoa wimbo wa salam zao, nyimbo za nyuma ilikuwa kawaida ila ‘salam zao’ umeniletea mambo mengi sana, watu wengi walikuwa wakinitumia sms wakinitishia maisha kwamba umetuingilia huku tutafanya hiki, wengine walisema watafungua kesi.
AyoTV: Ni nani ambaye amesema atafungua kesi?
Ney: Kwasasa hivi siwezi kumtaja lakini ni kwamba wakili aliyemfuata yeye ni rafiki wa wakili wangu, so wakili wangu ameniambia muda wowote nitatumiwa barua kwenda mahakamani so watu wajue kuna watu wameshaenda Mahakamani na watu wajue muda wowote nitaitwa mahakamani kwa ajili ya wimbo wa salam zao.
AyoTV: Unajiamini kiasi gani kwa kusema maneno hayo kuhusu watu au kuzungumzia maisha ya watu?
Ney: Mimi sijamini sana, lakini naheshimu maamuzi yangu.Ninapoamua kufanya kitu fulani basi lazima nifanye. Kuna watu wanasema mimi najiamini sana, lakini sio kweli naheshimu tu maamuzi yangu. Nikiamua kufanya kitu fulani ambacho kipo kwenye jamii na watu wata-support,huu muziki unaniruhusu,katiba ya nchi inaniruhusu na pia media ita-support kitu hicho basi lazima nifanye
AyoTV:Huwa unatumia vielelezo gani vya ushahidi ili kuzungumzia mambo mbalimbali ya watu hasa unapowakosoa?
Ney: Kwanza kabisa huwa nazungumza kitu ambacho watu wanakiona kipo ila wanashindwa kuzungumzia So point ya msingi ni kwamba kitu ninachozungumza kiko wazi sio nimekitoa kichwani hata mtu akiniuliza kwanini umeimba hivyo, hata wananchi wanaweza kunisaidia kujibu.
AyoTV: Hivyo vitisho unavyopata kwenye sms unawajua watu wanaokutumia?
Ney: Kwenye wimbo wa Salam zao wawili nawafahamu, nilipost kipande cha sehemu ya sms alizonitumia mwingine alinitumia sms na kuongea vitu ambavyo havistahili kabisa, wengine watatu siwafahamu kabisa.
AyoTV:Hii inakupa nafasi ya kuacha kufanya nyimbo za namna hii?
Ney: Sometimes kufuatana na watu wanaonizunguka wananiambia nistop kufanya hiki ambacho nakifanya nao mashabiki wanasema huo ndio muziki ambao tunaupenda na ndio maana tunaku-support, maamuzi yangu na akili yangu kuhusu kuacha kama nilivyosema naheshimu maamuzi yangu So siwezi kusema naacha au la, mimi ni mwanamuziki ambaye ni mfanyabiashara na ninaekwenda na wakati.
AyoTV:Uko tayari kwenda mahakamani?
Ney: Niko tayari, kwa mara ya kwanza naongea kwamba kuna mtu ameshaenda Mahakamani mimi nipo tayari.
AyoTV: Baba Levo aliku-diss kwenye stage ya Serengeti Fiesta 89.3 Kigoma kwa mtu ambaye hakuwepo alisema nini?
Ney: Kwanza watu wanafahamu kwamba mimi ni mwanamuziki mwenye nguvu kubwa so kwa mtu ambaye anataka attention atafanya hivyo alivyofanya Baba Levo,  Baba Levo alinifata na kunambia kwamba anataka kufanya kitu hiki japokuwa hakunambia ataenda kuongea maneno gani ndio maana mwisho wa siku nilipanda tukapiga show pamoja.
AyoTV : Alisema maneno gani pale kwenye stage Baba Levo?
Ney: Alikuwa anawaambia watu nikisema Ney mnasema shoga, Ney watu wanaitikia…… mimi hakikuniuma coz show niliyofanya Kigoma ni kubwa sana, watu walisema ukiimba Salam zao umemzungumzia Zitto Kabwe itakuwa sio poa, lakini salute kwa watu wa Kigoma.

Mtete Focus Blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni