.

Alhamisi, 23 Januari 2014

DR.SLAA:BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LIMECHOKA KABLA HALIJAANZA FANYA KAZI


Katibu mkuu wa Chadema Dr. Willbrod Slaa amesema kwamba baraza jipya la mawaziri lililoteuliwa na kutangazwa jana na katibu mkuu kiongozi limechoka kabla halijaanza kufanya kazi.

Aidha Dr. Slaa amesema kuwa uteuzi wa Mwigulu Nchemba kama naibu waziri wa fedha (sera) ni mkakati wa CCM kujichotea fedha za uchaguzi mkuu ujao hivyo tutarajie EPA nyingine.

Uteuzi wa Mwigulu Nchemba, Dr. Asharose Migiro, Adam Malima, Saada Mkuya, Jenista Mhagama na kurejeshwa kwa Dr. Shukuru Kawambwa kumezua manung'uniko mengi huku wengi wakihoji uwezo wao kiutendaji.

Dr Migiro anakuwa waziri wa katiba na sharia huku akielezwa kama miongoni mwa waliobeba maslahi ya CCM kwenye mchakato wa katiba mpya hususan kwenye madaraka ya rais na muundo wa muungano. Saada, Nchemba na Malima wamekabidhiwa wizara nyeti ya fedha na uchumi ambapo imedaiwa kuwa uwezo wao kiutendaji hauwezi kuiletea ufanisi wizara hiyo huku wengi wakitilia shaka uteuzi wa Nchemba kiuadilifu ambapo amekuwa akionyesha chuki za wazi kwa Chadema na viongozi wake na kukosa kabisa staha pale anapochangia bungeni.

Kawambwa na Jenista wamepewa jukumu la kuongoza elimu ambapo Kawambwa alionyesha dhahiri kushindwa vibaya kuongoza sekta hiyo nyeti kabla ya uteuzi mwingine wa jana.

Jumatano, 22 Januari 2014

MTANDAO WA KUMTOA JACK PATRICK WAUNDWA




FAMILIA ya modo wa Bongo, Jacqueline Patrick aliyenaswa kwa msala wa madawa ya kulevya Macau- China inadaiwa kuunda mtandao kwa ajili ya kufanikisha zoezi la kumchomoa mrembo huyo mikononi mwa vyombo vya sheria.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na familia hiyo (jina lipo), familia hiyo imeanza mchakato huo hivi karibuni hasa baada ya kudadisi kuhusiana na sheria za eneo alilokamatiwa (Macau) kutokuwa kali kisheria tofauti na maeneo mengine ya nchi hiyo kama Hong Kong.

“Wameandaa mikakati thabiti kwani wamegundua Macau ni tofauti na maeneo mengine ya China ambayo ukikamatwa na madawa ya kulevya na kuthibitika kuwa na hatia, hakuna msalie mtume, ni kitanzi tu. Macau sheria zao si kali sana, wanaweza wakafanikiwa kumchomoa hata kwa njia za panya,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Kinara wa mtandao huo ni Jux yule wanayesema ni mpenzi wake Jack ambaye kwa sasa yupo China. Ndiye ambaye juzijuzi hapa aliposti picha mpya za Jack na kusababisha watu wajue mrembo huyo kaachiwa huru.”

Paparazi wetu alimtafuta dada yake Jack ambaye hakupenda kutaja jina lake  ambapo alisema inawauma kutojua hatima ya ndugu yao hivyo wameona bora wajipange kwenda kufuatilia sakata hilo kupitia kwa Jux waliyemtaja kama ni rafiki wa Jack.

“Tunasikia maneno mengi tofautitofauti, inatuuma sisi kama ndugu hivyo tutajichanga na tutawatuma ndugu wawili ili waweze kwenda kushughulikia suala la ndugu yetu. Katika mkakati huu tumepata na baadhi ya marafiki wa Jack ambao kwa sasa sitawataja,” alisema dada huyo.

Hata hivyo, imeelezwa ndugu hao wametahadharishwa kuwa makini kwani licha ya kusikia sheria za Macau si kali sana wasidharau kwani huenda wakawekewa mtego na kujikuta wameingia katika matatizo kama watajaribu kutumia mlango wa ‘uani’ kumtoa Jack.

Kampeni Mpya za CHADEMA kutikisa Nchi Nzima….Helikopta tatu kurushwa Angani Siku 14 Mfululizo.


MBOWE
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuanzia leo, kinarusha helkopta tatu kwa siku 14 mfululizo, katika  kutekeleza kampeni iliyopewa jina la Operesheni Pamoja Daima (ODB) itakayoendeshwa katika mikoa yote nchini.
Ziara hiyo inaanzia katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Ruvuma, huku viongozi wa chama hicho wakijigawa katika makundi sita; matatu yakitumia helkopta na matatu yatawafikia wananchi kwa kutumia usafiri wa magari.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, lengo la operesheni hiyo ni kukiimarisha chama hicho na kuwafumbua macho wananchi kuhusu mchakato wa Katiba Mpya.
“Tumejigawa katika makundi sita na makundi matatu kati ya hayo yatatumia helikopta kila moja, makundi mengine yatawafikia wananchi kwa misafara ya ardhini,” alisema Mbowe na kuongeza;
“Viongozi wakuu wa chama, wabunge, wenyeviti wa mikoa, wilaya, majimbo na kanda kila mmoja atashiriki kwa nafasi yake katika operesheni hii. Tutafanya mikutano kwa wiki mbili, ila tunaweza kuongeza wiki nyingine moja.”
Alisema chama hicho kimejipanga kuwafikia wananchi wengi kadri itakavyowezekana, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wake wa ndani kuanzia ngazi ya mashina, uchaguzi mdogo wa madiwani katika Kata 27 nchini utakaofanyika Februari 9, mwaka huu pamoja na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
chadema
“Naomba tueleweke, katika hili hatufanyi kampeni hata kidogo, huu ni mwendelezo wa maandalizi ya chaguzi mbalimbali. Kama mnakumbuka tulianza kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2015 baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010,” alisema Mbowe na kuongeza;
“Kwa sasa tunachokifanya ni kuongeza nguvu na umakini zaidi. Makundi yataanzia katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Ruvuma, tutapita kila Kata ambazo utafanyika uchaguzi wa madiwani.”
Mbowe alisema operesheni hiyo itapiga kambi katika Jimbo la Kalenga ambalo kwa sasa lipo wazi baada ya mbunge wake ambaye pia alikuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa kufariki dunia Januari 1, mwaka huu nchini Afrika Kusini.
“Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) haijatangaza kufanyika uchaguzi katika jimbo hilo, Chadema tutafika Kalenga na tutafanya mkutano maalumu na kutoa pole kwa wakazi wa jimbo hilo kutokana na msiba mkubwa wa mbunge wao,” alisema Mbowe.
Operesheni hiyo inafanyika siku chache tangu chama hicho kikuu cha upinzani nchini kipite katika mgogoro ambao ulisababisha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe kukimbilia mahakamani ili kunusuru uanachama wake.
Wakati Zitto akinusurika kufukuzwa kutokana na zuio la mahakama, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo walifukuzwa uanachama, likiwa ni hitimisho la mchakato ulioanza kwa kuwavua nyadhifa zao pamoja na Zitto.

SOURCE: Mwananchi

Picha 7 za kitakachoonekana ktk video mpya ya Weusi ‘nje ya box’ magari na yule manka wa kichaga sasa


Screen Shot 2014-01-22 at 9.38.51 PMUnaambiwa Ijumaa hii ya January 24 2014 ndio video hii itawafikia mamilioni ya Watanzania manake ndio siku ya kuachiwa kwake ikiwa imefanywa na mkali kutoka 87.9 Arusha >> Nisher.
Mwezi wa kwanza wa 2014 tayari umemilikiwa na video za wasanii kama Diamond, Chege, Madee, Makomando na sasa wanafata Weusi na ‘nje ya box’ ambayo hizi ni baadhi tu ya picha za kitakachoonekana ndani yake.
Hizi hapa ni picha na kipisi cha video hiyo.

5
4
3
2
1

Magazeti ya leo January 23 2014 na stori kubwa za Udaku, Michezo na Hardnews


.
.


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
..
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
..
.
..
.
.
.
.
.
.
.
..
.
.
.
.
.
.
.
.


Jumamosi, 18 Januari 2014

Mwanamke aliyetapeli kwa Airtel Money Atupwa jela miezi 6..!!


court.hammer
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imemhukumu mkazi wa hapa kwenda jela miezi sita, kwa kosa la utapeli wa fedha kwa njia ya mtandao wa Airtel Money kwa mawakala mbalimbali wilayani humo.
Akitoa hukumu hiyo, Hakim Mkazi Mfawidhi, Joseph Ngomelo, alisema mshitakiwa Helena Alexandria, atakwenda jela miezi sita baada ya kukiri kufanya utapeli huo.
Mshitakiwa huyo alikiri kutapeli mawakala mbalimbali wa Airtel Money waliopo Nzega mjini kwa njia ya mtandao na kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.
Alisema kifungo cha mama huyo kitakuwa fundisho kwa wanawake wangine wenye tamaa, kwani makosa kama hayo yakiachiwa yanaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii.
Awali Mwendesha Mashitaka wa Polisi Mkaguzi Msaidizi, Melito Ukongoji, aliiambia Mahakama hiyo kuwa Januari mosi mwaka 2014, mshitakiwa ambaye ni mkazi wa Nzega mjini, aliiba kwa kutumia mtandao wa Kampuni ya Airtel Money.
Alidai kuwa Hellena alikuwa akitumia ujumbe mfupi wa maneno wenye muamala wa kutoa pesa Sh 40,000 Airtel Money na kujipatia Sh 40,000 kwa kila wakala kwa nyakati tofauti.
 court-hammer
Akijitetea, mshitakiwa alikiri kuhusika na tuhuma hizo kwa nyakati tofauti na kuongeza kuwa lengo lilikuwa ni kutafuta fedha za kujikimu kimaisha kutokana ugumu wa maisha.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo Mwendesha Mashitaka aliiomba Mahakama hiyo itoe adhabu kwa mshitakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo za wizi wa utapeli kwa njia ya mtandao.
Chanzo: Habari Leo