.

Jumamosi, 8 Februari 2014

Msanii wa Project fame alieingia kwenye vita ya nchi, anasema Rais akiuwawa amani ndio itakuja.



Screen Shot 2014-02-08 at 12.35.39 PMUnaweza kujaribu kutengeneza picha, pale ambapo msanii anaamua kushika bunduki na kuingia kwenye vita ya nchi yake kisa hajapendezwa na upande mmoja kati ya mbili zinazopingana.
Imeripotiwa kwamba huenda aliewahi kuwa mshiriki wa shindano la Tusker Project fame Kuonck ‘K-Denk’ Deng na kuiwakilisha nchi yake ya Sudan ya Kusini, ameamua kushika silaha na kuingia vitani.
Screen Shot 2014-02-08 at 11.50.50 AM
Screen Shot 2014-02-08 at 12.20.59 PMKwenye page yake ya facebook, K Denk amepost status kadhaa zenye utata ambazo mapokezi yake hayajawa mazuri… na hii imeonekana toka vita ianze December 2013 nyumbani kwao Sudan.
Updates zinaonyesha msanii huyu alieamua kuingia vitani, amehama kutoka Juba hadi sehemu ya kaskazini ambayo inashikiliwa na Waasi.
Screen Shot 2014-02-08 at 12.25.01 PMK Denk ameonekana kuwa upande wa Waasi wanaopigana na Serikali huku akisisitiza kwamba amani itapatikana baada ya Rais Salva Kiir kuuwawa.
Baadhi ya mashabiki zake ambao ni sehemu ya waliopoteza ndugu zao kwenye vita hii hawajasita kumuandikia ya moyoni.
Screen Shot 2014-02-08 at 12.25.28 PMSource: gazeti la Daily Nation.

MWANAMKE MUIMBA KWAYA MSOMI WA CHUO KIKUU ANASWA AKIJIUZA, AHAHA MCHUNGAJI ASIJUE:



Ni aibu iliyoje? Mwanadada ambaye amejitambulisha kuwa ni msomi wa chuo kikuu (jina lipo) ambaye pia ni mwanakwaya chuoni hapo aliyejitaja kwa jina moja la Rei ameaibika baada ya kunaswa usiku mnene akijiuza, Risasi Jumamosi linaifumua.


Mwanakwaya,msomi wa chuo kikuu (katikati), aliyejitaja kwa jina moja la Rei.
Rei alikamatwa katika msako wa polisi katikati ya Jiji la Dar (City Center) hivi karibuni akiwa na kundi la warembo wa vyuo mbalimbali wakifanya biashara haramu ya kuuza miili.
Mrembo huyo ambaye Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilimshuhudia, kabla ya kupelekwa kituo kikuu  cha polisi, Wilaya ya Ilala (Central),  alijitetea kuwa yeye ni denti wa chuo kikuu hivyo kitendo cha kupigwa picha alijua kabisa kuwa zitasambaa mitandaoni hivyo itakuwa ni aibu kubwa.
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers wakichukua picha.
“Kaka naomba usinitoe gazetini au mitandaoni, haya ni maisha tu, itakuwa aibu kwa wanachuo wenzangu,” alijitetea.
Mbali na hayo, mrembo huyo wa haja alikuwa akihaha kuwa kama ishu hiyo itamfikia mchungaji wake, basi hatakuwa na sehemu ya kuficha uso wake.
Pia Rei alijitetea kuwa huwa hajiuzi kila siku na hiyo ilitokea tu kwa bahati mbaya kwani ana biashara zake binafsi.
Alipoulizwa na ‘kachero’ wetu juu ya kanisa au kwaya anayoitumikia alikataa kutaja kwa madai kuwa atalichafua kanisa.
“Wewe ujue tu mimi ni mwanakwaya, hayo mambo ya kwaya na kanisa sitaki kulichafua jina la Mungu,” alisema.
Mwanakwaya,msomi wa chuo kikuu (katikati).
Kwa mujibu wa polisi wa doria waliowanasa warembo hao walidai kuwa Jumatano iliyopita watafikishwa katika Mahakama ya Jiji la Dar (Sokoine Drive) chini ya Hakimu Mkazi, Timothy Lyon kwa kosa la uzururaji kwa kuwa hakuna sheria ya moja kwa moja juu ya ukahaba.

PICHA MBALI MBALI ZA NICK MINAJ AKIWA BILA WIGI...SHE IS CUTE I LIKE HER LIKE THIS


 Jionee Mwenye Mtoto Alivyo Bomba ...Hapo kaweka Usela wote pembeni na yale mawigi yake ya kishetani pembeni ...mtoto unywele Anao ...Dahhhh She is Cute ......
Check picha alafu ucomment





AY AKANUSHA KUMTUNGIA NYIMBO JAGUAR...APINGA KUWA DIAMOND NI TISHIO KWAKE


Msanii wa HipHop kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya amekanusha uvumi uliokuwa umezagaa nchini Kenya wa kumuandikia baadhi ya nyimbo mkali wa Kioo kutoka Kenya, Jaguar.

Katika mahojiano aliyofanyiwa nchini Kenya alikokuwa ameenda hivi karibuni, AY amesema hajawai kumuandikia wimbo wowote Jaguar na hata wimbo wao ‘Nimetoka Mbali’ kila mtu aliandika mashairi yake.

“Jaguar ni mmoja wa marafiki zangu. Tumefanya kazi pamoja na hakuna ukweli wowote kuhusiana na tetesi za mimi kumuandikia mashairi ukizingatia amekuwepo kwa muda mrefu kwenye gemu ya muziki hivyo kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii wenye uzoefu wa kutosha na kufanya vizuri hata ukitazama ngoma niliyowahi kufanya nae ya Nimetoka Mbali, kila mmoja wetu aliandika mashairi yake kivyake hivyo huna haja ya kubisha kwa uwezo mkubwa alionao na naamini ni ushahidi tosha,” alisema.

Pia AY amepinga muziki wake kuathiriwa na Diamond kwakuwa kila mtu ana malengo yake katika muziki wake.

“Kila msanii ana mipango na mikakati yake ya kufikia malengo aliyojiwekea, sipo kujilinganisha na mtu yoyote, ushindani wangu ni kwa yule anayetaka kujaribu kutengeneza mkwanja mkubwa kushinda wangu, huo ndio ushindani wa kweli, hata hivyo siwezi kuwa juu milele.”

Source:Bongo5

Hawa ndio walioteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge maalum la Katiba.


wajumbeJioni ya February 07 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Mh.Florence Turuka alitangaza majina ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,ambalo bunge hilo litakutana kwa siku 70 na kuongezewa 20 kama hawatoafikiana.
Bunge hilo la Katiba litakuwa na jumla ya wajumbe 640 kujadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Desemba 30 2013 majina hayo yalitangazwa kupitia ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam.
IKULU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
UTANGULIZI
1. Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.
  1. Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
    (i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
    (ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
    (iii) Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.
  2. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-
(i) Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii) Taasisi za Kidini (20)
(iii) Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv) Taasisi za Elimu (20);
(v) Watu wenye Ulemavu (20);
(vi) Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii) Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii) Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix) Vyama vya Wakulima (20); na
(x) Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).
  1. Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.
  2. Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  • Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874. Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118 walijipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.
  • Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo:
  • Na.
    Kundi/Taasisi
    Taasisi zilizoleta mapendekezo
    Idadi ya Watu Waliopendekezwa
    Idadi ya Wajumbe Wanaotakiwa
    Idadi ya Walioteuliwa
    Tanzania Bara
    Zanzibar
    Tanzania Bara
    Zanzibar
    Tanzania Bara
    Zanzibar



    1. Taasisi zisizokuwa za Kiserikali 246 98 1,203 444 20 13 7
    2. Taasisi za Kidini 55 17 344 85 20 13 7
    3. Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu 21 14 129 69 42 28 14
    4. Taasisi za Elimu 9 9 84 46 20 13 7
    5. Makundi ya Walemavu 24 6 97 43 20 13 7
    6. Vyama vya Wafanyakazi 20 1 89 13 19 13 6
    7. Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji 8 1 43 4 10 7 3
    8. Vyama vinavyowakilisha Wavuvi 7 3 45 12 10 7 3
    9. Vyama vya Wakulima 22 8 115 44 20 13 7
    10. Makundi yenye Malengo Yanayofanana 142 21 613 114 20 14 6

    Mapendekezo Binafsi - - 118 -



    Jumla 672 178 2,880 874 201 134 67

    Jumla Kuu 850 3,754


    1. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba. Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja wanatakiwa kutoka Zanzibar na theluthi mbili kutoka Tanzania Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe 201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar na wajumbe 134 watatoka Tanzania Bara. Aidha, mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe 201 halikuwa rahisi hata kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.
    2. Kama nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar, majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu 1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13 tu. Kwa upande Zanzibar, taasisi zisizokuwa za kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.
    WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
    10. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:
    (a) Uteuzi umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijana, watu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati miaka 22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
    (b) Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.
    (c) Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika kila chama.
    Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya wajumbe 201 wa Bunge Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:
    TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI- (WAJUMBE 20)
    TANZANIA BARA (13)
    1. Magdalena Rwebangira 2. Kingunge Ngombale Mwiru
    3. Asha D. Mtwangi 4. Maria Sarungi Tsehai
    5. Paul Kimiti 6. Valerie N. Msoka
    7. Fortunate Moses Kabeja 8. Sixtus Raphael Mapunda
    9. Elizabeth Maro Minde 10. Happiness Samson Sengi
    11. Evod Herman Mmanda 12. Godfrey Simbeye
    13. Mary Paul Daffa
    TANZANIA ZANZIBAR (7)
    1. Idrissa Kitwana Mustafa 2. Siti Abbas Ali
    3. Abdalla Abass Omar 4. Salama Aboud Talib
    5. Juma Bakari Alawi 6. Salma Hamoud Said
    7. Adila Hilali Vuai


    TAASISI ZA KIDINI- (WAJUMBE 20)
    TANZANIA BARA (13)
    1. Tamrina Manzi 2. Olive Damian Luwena
    3. Shamim Khan 4. Mchg. Ernest Kadiva
    5. Sheikh Hamid Masoud Jongo 6. Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela
    7. Magdalena Songora 8. Hamisi Ally Togwa
    9. Askofu Amos J. Muhagachi 10. Easter Msambazi
    11. Mussa Yusuf Kundecha 12. Respa Adam Miguma
    13. Prof. Costa Ricky Mahalu
    TANZANIA ZANZIBAR (7)
    1. Sheikh Thabit Nouman Jongo 2. Suzana Peter Kunambi
    3. Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu 4. Fatma Mohammed Hassan
    5. Louis Majaliwa 6. Yasmin Yusufali E. H alloo
    7. Thuwein Issa Thuwein


    VYAMA VYOTE VYA SIASA
    VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE 42)
    TANZANIA BARA (28)
    1. Hashim Rungwe Spunda 2. Thomas Magnus Mgoli
    3. Rashid Hashim Mtuta 4. Shamsa Mwangunga
    5. Yusuf S. Manyanga 6. Christopher Mtikila
    7. Bertha Ng’angompata 8. Suzan Marwa
    9. Dominick Abraham Lyamchai 10. Mbwana Salum Kibanda
    11. Peter Kuga Mziray 12. Isaac Manjoba Cheyo
    13. Dr. Emmanuel John Makaidi 14. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
    15. Modesta Kizito Ponera 16. Prof. Abdallah Safari
    17. Salumu Seleman Ally 18. James Kabalo Mapalala
    19. Mary Oswald Mpangala 20. Mwaka Lameck Mgimwa
    21. Nancy S. Mrikaria 22. Nakazael Lukio Tenga
    23. Fahmi Nasoro Dovutwa 24. Costantine Benjamini Akitanda
    25. Mary Moses Daudi 26. Magdalena Likwina
    27. John Dustan Lifa Chipaka 28. Rashid Mohamed Ligania Rai
    TANZANIA ZANZIBAR (14)
    1. Ally Omar Juma 2. Vuai Ali Vuai
    3. Mwanaidi Othman Twahir 4. Jamila Abeid Saleh
    5. Mwanamrisho Juma Ahmed 6. Juma Hamis Faki
    7. Tatu Mabrouk Haji 8. Fat –Hiya Zahran Salum
    9. Hussein Juma 10. Zeudi Mvano Abdullahi
    11. Juma Ally Khatibu 12. Haji Ambar Khamis
    13. Khadija Abdallah Ahmed 14. Rashid Yussuf Mchenga

    TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)
    TANZANIA BARA
    1. Dr. Suzan Kolimba 2. Prof. Esther Daniel Mwaikambo
    3. Dr. Natujwa Mvungi 4. Prof. Romuald Haule
    5. Dr. Domitila A.R. Bashemera 6. Dr. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa
    7. Prof. Bernadeta Kilian 8. Teddy Ladislaus Patrick
    9. Dr. Francis Michael 10. Prof. Remmy J. Assey
    11. Dr. Tulia Ackson 12. Dr. Ave Maria Emilius Semakafu
    13. Hamza Mustafa Njozi
    TANZANIA ZANZIBAR (7)
    1. Makame Omar Makame 2. Fatma Hamid Saleh
    3. Dr. Aley Soud Nassor 4. Layla Ali Salum
    5. Dkt. Mwinyi Talib Haji 6. Zeyana Mohamed Haji
    7. Ali Ahmed Uki


    WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20)
    TANZANIA BARA (13)
    1. Zuhura Musa Lusonge 2. Frederick Msigala
    3. Amon Anastaz Mpanju 4. Bure Zahran
    5. Edith Aron Dosha 6. Vincent Venance Mzena
    7. Shida Salum Mohamed 8. Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi.
    9. Elias Msiba Masamaki 10. Faustina Jonathan Urassa
    11. Doroth Stephano Malelela 12. John Josephat Ndumbaro
    13. Ernest Njama Kimaya
    TANZANIA ZANZIBAR (7)
    1. Haidar Hashim Madeweyya 2. Alli Omar Makame
    3. Adil Mohammed Ali 4. Mwandawa Khamis Mohammed
    5. Salim Abdalla Salim 6. Salma Haji Saadat
    7. Mwantatu Mbarak Khamis
    VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19)
    TANZANIA BARA (13)
    1. Honorata Chitanda 2. Dr. Angelika Semike
    3. Ezekiah Tom Oluoch 4. Adelgunda Michael Mgaya
    5. Dotto M. Biteko 6. Mary Gaspar Makondo
    7. Halfani Shabani Muhogo 8. Yusufu Omari Singo
    9. Joyce Mwasha 10. Amina Mweta
    11. Mbaraka Hussein Igangula 12. Aina Shadrack Massawe
    13. Lucas Charles Malunde
    TANZANIA ZANZIBAR (6)
    1. Khamis Mwinyi Mohamed 2. Jina Hassan Silima
    3. Makame Launi Makame 4. Asmahany Juma Ali
    5. Mwatoum Khamis Othman 6. Rihi Haji Ali


    VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE 10)
    TANZANIA BARA (7)
    1. William Tate Olenasha 2. Makeresia Pawa
    3. Mabagda Gesura Mwataghu 4. Doreen Maro
    5. Magret Nyaga 6. Hamis Mnondwa
    7. Ester Milimba Juma
    TANZANIA ZANZIBAR (3)
    1. Said Abdalla Bakari 2. Mashavu Yahya
    3. Zubeir Sufiani Mkanga


    VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI –(WAJUMBE 10)
    TANZANIA BARA (7)
    1. Hawa A. Mchafu 2. Rebecca Masato
    3. Thomas Juma Minyaro 4. Timtoza Bagambise
    5. Tedy Malulu 6. Rebecca Bugingo
    7. Omary S. Husseni
    TANZANIA ZANZIBAR (3)
    1. Waziri Rajab 2. Issa Ameir Suleiman
    3. Mohamed Abdallah Ahmed
    VYAMA VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20)
    TANZANIA BARA (13)
    1. Agatha Harun Senyagwa 2. Veronica Sophu
    3. Shaban Suleman Muyombo 4. Catherine Gabriel Sisuti
    5. Hamisi Hassani Dambaya 6. Suzy Samson Laizer
    7. Dr. Maselle Zingura Maziku 8. Abdallah Mashausi
    9. Hadijah Milawo Kondo 10. Rehema Madusa
    11. Reuben R. Matango 12. Happy Suma
    13. Zainab Bakari Dihenga
    TANZANIA ZANZIBAR (7)
    1. Saleh Moh’d Saleh 2. Biubwa Yahya Othman
    3. Khamis Mohammed Salum 4. Khadija Nassor Abdi
    5. Fatma Haji Khamis 6. Asha Makungu Othman
    7. Asya Filfil Thani


    WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)
    TANZANIA BARA (14)
    1. Dr. Christina Mnzava 2. Paulo Christian Makonda
    3. Jesca Msambatavangu 4. Julius Mtatiro
    5. Katherin Saruni 6. Abdallah Majura Bulembo
    7. Hemedi Abdallah Panzi 8. Dr. Zainab Amir Gama
    9. Hassan Mohamed Wakasuvi 10. Paulynus Raymond Mtendah
    11. Almasi Athuman Maige 12. Pamela Simon Massay
    13. Kajubi Diocres Mukajangwa 14. Kadari Singo
    TANZANIA ZANZIBAR (6)
    1. Yussuf Omar Chunda 2. Fatma Mussa Juma
    3. Prof. Abdul Sheriff 4. Amina Abdulkadir Ali
    5. Shaka Hamdu Shaka 6. Rehema Said Shamte



    Imetolewa na:
    Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
    Ikulu.
    Dar es Salaam.
    7 Februari, 2014

    Jumatano, 5 Februari 2014

    TAARIFA YA KUKATIKA KWA MAWASILIANO YA VODACOM‏


    Dar es Salaam, 5 Februari, 2014.Tunapenda kuwaomba radhi wateja wetu wote kwa kushindwa kutoa huduma za mawasiliano kuanzia asubuhi ya Februari  5, 2014. Hii imetokana na kukatika kwa mkonga wa mawasiliano ulioko barabara ya Morogoro na  nyingine mbili za ziada zilizoko Mlalakuwa na Mayfair plaza barabara ya Mwai kibaki jijini Dar es Salaam.
    Kukatika kwa Mkonga huo kumesababisha vituo vyetu vya kutoa huduma za mawasiliano vilivyopo Oysterbay na mbezi juu kushindwa kufanya kazi kutokana na vituo hivyo kutegemeana kumesababisha kushindwa kutoa huduma za mawasiliano.
    Kutokana na hilo wateja hawakuwa na uwezo wa kupiga simu, kutumia intaneti na hata  huduma za kifedha. Tunatambua usumbufu ambao umetokea kwa kukosa mawasiliano, kwa mara nyingine tena tunaomba radhi na tunashukuru kwa uvumilivu wao katika kipindi chote ambacho huduma zilikosekana. 
    Mafundi wetu wameweza kurekebisha uharibifu uliotokea barabara ya Mwai kibaki ambao uliotokana na shughuli za ujenzi  wa barabara zinazoendelea. Uharibifu mwingine uliotokea katika Barabara ya Mlalakuwa ulichukua muda kurekebisha kutokana na nyaya zilizo katika mkonga wa mawasiliano kuungua kulikosababishwa na zoezi la uchomaji taka lililokuwa linaendelea katika sehemu ambayo mkongo umepita na kusababisha uharibifu huo. 
    Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa, Tumejidhatiti katika kuendelea kutoa huduma bora na za kipekee  wakati wote watakapokuwa wanautumia mtandao wa Vodacom, Tunawashukuru kwa namna ambavyo wameendelea kutuunga mkono na kutuvumilia pale matatizo yanapojitokeza. 
    Rene Meza 
    Mkurugenzi Mtendaji – Vodacom Tanzania

    Kilichosemwa na Basata kuhusu kufungiwa kwa video kadhaa hapa Bongo ikiwemo ya Snura.


    godSiku kadhaa zilizopita kupitia millardayo.com kuna taarifa ziliztoka kuhusu kufungiwa kwa video ya Nimevurugwa ya Snura,taaarifa hizi alizi-amplify meneja wake Snura ‘Hk’ akidai kuwa sababu maalum bado hawajazipata ingawa kila kituo anachoenda wanampa sababu tofauti.
    Millardayo.com haikuishia hapo ilienda moja kwa moja kwenye Baraza la Sanaa la Taifa(Basata)ili kuujua undani wa sakata hili ikiwemo pia kuulizia video ya Jux(uzuri wako)ambayo nayo ilitoka taarifa ya kufungiwa kwa video hiyo.
    Kutoka Basata huyu hapa Godfrey mungeleza ni kaimu katibu mtendaji  anataarifa zaidi>>Unaposema kufungia video moja kwa moja kuna chombo kingine cha serikali kinashughulikia hilo ambao ni bodi ya filamu Tanzania’
    ‘Bodi ya filamu wanaangalia video zote suala zima la filamu wanapoona hii haikidhi au haifai kwa jamii za Kitanzania basi wanaisimamisha kidogo wanamshauri aweze kuirekebisha ili iweze kulingana na maadili ya kitanzania’
    ‘Sisi tunaangalia Audio kabla haijaingia sokoni katika urasimishaji tunakaa tunausikiliza muziki wake tunashauriana kwamba akarekebishe hapa na tunaangalia mambo mengi ikiwemo ubunifu wake mwenyewe’
    ‘Suala la kufungiwa kwa Snura najua kabisa linaenda kwenye suala la maadili na limeandikwa sana na sisi Baraza kama Baraza tunaangalia sana suala la maadili tukisema tunamfungia hatufungii video tu tunamfungia msanii mwenyewe’

    BAADA YA BAADHI KUJIUNGA CCM-BONGO MOVIES VIPANDEVIPANDE!


    Stori: Waandishi Wetu
    MPASUKO mkubwa umeikumba tasnia ya filamu Bongo baada ya baadhi ya wasanii wanaong’ara kuchukua kadi rasmi za kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.

    Tukio hilo lilitokea juzi, Jumapili jijini Mbeya kulipokuwa na sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais Jakaya Kikwete.

    Mashabiki mbalimbali wa sinema za Kibongo, waliingia kwenye mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii, mara baada ya wasanii hao kuonesha uamuzi wao, kila mmoja akieleza mtazamo wake.

    WASANII WENYEWE
    Baadhi ya wasanii waliochukua kadi za CCM ni pamoja na Jacob Steven ‘JB’, Single Mtambalike ‘Richie’, Irene Uwoya, Haji Salum ‘Mboto’, Tamrina Posh ‘Amanda’, Blandina Chagula ‘Johari’, Wastara Juma na Haji Adam ‘Baba Haji’.

    MIJADALA
    Watoa maoni walikuwa na mawazo tofauti kuhusiana na uamuzi wa wasanii hao wenye mashabiki wengi, wengine wakiwapongeza huku upande wa pili ukiwashutumu kwa maelezo kuwa wanawagawa mashabiki wao.

    Mtoa maoni aliyejitaja kwa jina la Mussa Juma aliandika: “Sijui hawa wasanii wetu watakua lini? Huwezi kuonesha itikadi yako ya kisiasa wakati una mashabiki wengi. Hapo wamechemka. Mfano mimi siyo CCM na siwezi kununua tena filamu za JB.”

    IPYANA LWIGA:
    “Hii ndiyo demokrasia, unawavuta watu wajiunge kwako kwa kuwapa usafiri na mahitaji yote muhimu! Wameona mbali sana, nawapongeza sana! Wajifunze kwa Marlaw!”

    BENATUS MARWA NYAMBORI:
    “Huo ni uamuzi wao. Hauhusiani na kazi zao. Kama umechukia, chukua kazi zao zote piga moto. Kiukweli Chadema mnafikiri watu wengi wanawasapoti? Hapana... huko vijijini wanakuja kuangalia helikopta maana hawajawahi kuiona.”

    JACOBS KING:
    “Sasa hivi ndiyo watakoma kabisa, najua hakuna wa kununua kazi zao, wataibiwa mpaka wakome, CCM wanataka kuwatumia kwenye kampeni mikoani ili wawavutie wananchi kwenye mikutano yao lakini kwa sasa Watanzania tunajielewa.”


    COCU BATENGA: 
    “Wasanii wana haki ya kuchagua chama chochote wakipendacho. Wakati wa kazi ni kazi, siasa ni siasa. Mbona Sugu (Joseph Mbilinyi – Mbunge wa Mbeya Mjini) yupo bungeni? Mbona Afande Sele (Seleman Msindi) ametangaza kujiunga Chadema, mbona hayasemwi? Hakuna mantiki hapa.”

    JB BUNGENI
    Hivi karibuni, JB alitangaza nia yake ya kugombea ubunge ingawa bado hajataja jimbo, kitendawili cha atagombea kwa tiketi ya chama gani, kimeshateguka baada ya kuchukua kadi ya CCM.

    Hata hivyo, minong’ono inasema kwamba, JB huenda atagombea Jimbo la Kinondoni (kwa sababu ndiyo eneo analoishi) au Same (kwa sababu ni mzaliwa wa huko).

    TUNDU LISSU:WABUNGE WENGI BONGO HAWAJUI KINGEREZA



    Mbunge wa Singida Mashariki, mnadhimu wa upinzani na mwanasheria mkuu wa CHADEMA mh. Tundu Lissu, amesema kuwa wabunge wengi wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hawajui lugha ya kiingereza kitendo kinachowafanya wakose ufanisi katika kazi zao za kibunge hususani mijadala mbalimbali bungeni na nje ya bunge. 

    Mwanasheria huyo amekiita kitendo hicho kuwa ni janga la taifa ambapo ameshauri suala hilo litazamwe upya ili tuwe na wabunge wanaoweza kuwa tija kwa taifa.

    Ikumbukwe kuwa wabunge wengi wa bunge hili wamekuwa wakituhumiwa kuwa na elimu za kidato cha nne (iv) au chini ya hapo na wengine kidato cha sita chenye matokeo mabaya.

    source; cluods fm na star tv.

    Taarifa kuhusu hukumu ya Chris Brown na kesi ya kumshambulia mtu.


    2
    Chris Brown akiambatana na girlfriend wake Karrueche Tran pamoja na wakili wake wameingia kwenye chumba cha mahakama huko L.A baada ya ushahidi wa kesi inayomkabili kupitiwa.
    Kesi hiyo ilikuwa inasema kwamba Chris Brown alimshambulia mtu mmoja huko D.C na waendesha kesi hiyo walisisitiza kwamba tabia ya Chris Brown ya kufanya fujo na kushambulia watu inaendelea kukua na kutokea mara nyingi na inaongeza hatari kwa jamii.
    Licha ya mambo yote kusikilizwa na jaji James Brandlin hakukubaliana na hayo mawazo ambayo yalitaka C Brown afungwe jela. Mwisho wa kesi jaji alisema ni bora Chris Brown aendelee na siku tisini za rehab for anger management kuliko kumuweka jela.
    3
    4
    1