.

Alhamisi, 17 Oktoba 2013

Ndoa Ya Producer Timbaland Hatarini

 Mke wa mtayarishaji muziki Timberland, Monique ameripotiwa kuanzisha mchakato wa kuachana na producer huyu na hii ikiwa ni baada ya miaka 5 ya kuishi pamoja kama mke na mume.
Katika nyaraka za talaka ambazo amezifile mwanamama huyu, madai ya Monique baada ya kutengana na Timberland ambaye utajiri wake ni zaidi ya dola milioni 80, ni malipo ya gharama zote za malezi ya watoto pamoja na gharama za kesi hii ambayo amedai kuwa amemkopa rafiki yake pesa za kumlipa mwanasheria anayesimamia madai haya.
Kimbembe kikubwa katika madai ya Monique ni juu ya malezi ya moja ya watoto wake ambaye Timberland siye baba yake halisi, ambapo mama wa mtoto amedai kuwa ni jukumu la Timberland kumlea vile alishamkubali kama mtoto wake wakati walikuwa wakiishi pamoja.
Mtete Focus Blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni