.

Jumanne, 28 Oktoba 2014

Unafahamu kilichoandikwa kwenye mitandao ya kijamii Nigeria kuhusiana na msanii Wizkid? Kisome hapa.

Wiz & Vicky


Taarifa zilizoenea mitandao mbali mbali ya Nigeria saa chache zilizopita zinazungumzia tukio kutoka Kenya linalohusiana na kukamatwa kwa msanii wa Nigeria Wizkid ambaye alishikiliwa na na jeshi la Polisi nchini humo saa chache kabla ya kupanda ndege kurejea Nigeria.
Taarifa iliyoandikwa na Standard Digital Kenya imesema, Wizkid alikamatwa hotelini Nairobi Crown Plaza ambapo amekaa kwa takribani wiki moja baada ya kufanya onesho lake.
Kwa mujibu wa habari kutoka chanzo hicho, Wizkid alikamatwa kwa kosa la kuvuta bangi hotelini hapo na baada ya mzozo wa muda mrefu baina yake na mhudumu wa hoteli hiyo, mhudumu wa hoteli alitoa taarifa polisi ambao walimkamata na kumfikisha kituo cha Capital Hill ambapo alipigwa faini ya sh. 50,000 za Kenya kwa kosa hilo na baadaye kuachiwa huru.
Wizkid alikamatwa hotelini hapo siku ya jumamosi kwa kosa hilo, ambapo Victoria Kimani, msanii wa Kenya ambaye wamefanya kolabo hivi karibuni ametajwa kuhusika kumtoa Wizkid kutoka kituo cha Polisi.

Jumatatu, 27 Oktoba 2014

CCM YAFUNIKA MJINI UNGUJA, ZANZIBAR



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia Wananchi na Wanachama wa CCM katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja leo.
 Wananchi na WanaCCM waliofirika katika viwanja vyaDemokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja wakiwa katika Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein leo ambao umeweka bayana na kufanya uchambuzi baadhi ya vifungu vya katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba

 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais Mama Pili Balozi wakiwa katika Mkutano wa Hadhara katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja leo uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyeekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  .[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyeekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Borafya Silima,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakifuatana katika mkutano hadhara uliofanyika leo katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja,.Picha na IKULU-Zanzibar
 

Huyu ndiye Rais mwanamke aliyeshinda kiti cha Urais kwa mara ya pili.

DilmaMwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa urais nchini Brazil 2011, Diana Rousseff amechaguliwa tena kushika wadhifa huo katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili Oktoba 25 nchini humo.
Baada ya kutangazwa kushinda katika kinyang’anyiro hicho, Rousseff mwenye umri wa miaka 66 amesema anahitaji kufanya vizuri katika awamu hii ya uongozi wake huku akisifia jitihada zake na rais aliyemtangulia Luiz Inacaio Da Silva kuwa katika vipindi vyao vya uongozi wametatua tatizo la ajira kwa kiasi kikubwa.
Rousseff ameshinda kwa 51.59% ambapo mpinzani wake Aecio Neves amepata kura 48.41%.

Jumapili, 26 Oktoba 2014

Msichana asimulia ya Boko Haram


Baadhi ya wasichana waliotekwa nyara
Ni miezi sita sasa baada ya wanamgambo wa kiislam wa kundi la Boko Haram kuwateka wanafunzi wasichana Zaidi ya 200 kaskazini mashariki mwa Nigeria, wasichana watatu ambao wametoroka wamezungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC.
Tukio hili linakuja wakati serikali ya Nigeria ikiwa katika makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram hatua itakayo saidia kuwaachilia huru wasichana waliotekwa na kundi hilo .
'' nilikuwa nataka kurukia nje wakati msichana mwenzangu aliponikamata kwa nyuma na kusema watakupiga risasi kama utafanya hivyo. Nikasema, nini utofauti wataniua mimi hapa na kuacha maiti yangu ikusachukuliwa nilikuwa nalia na kuomba mpaka tulipoifikia kambini" Anasimulia msichana mmoja alitoroka mikononi mwa Boko Haram
Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC, Msichana huyu anakumbuka jinsi alivyokuwa nyuma ya Lori wakati wanapinaji wa Boko Haramu walipomteka yeye na wasichana wengine.
Zaidi ya wasichana 200 kati miongoni mwao walikuwa walitekwa lakini wale waliokimbia walibahatika kutoingia katika hofu kubwa kwenye mikono ya watekaji.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadam la Human Rights Watch limesema wanawake wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haramu wamekuwa wakinyanyaswa, kubakwa na hata kulazimishwa kuolewa.
Katika ripoti mpya ya shirika hilo inasema Wanamgambo hao wa Kiislam wamewawateka wanawake Zaidi ya 500 na wasichana tangu mwaka 2009.
Serikali ya Nigeria hivi karibuni imetangaza makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram ambayo hatua itakayawafanya wanamgambo ho kuachilia huru wasichana wa hao waliotekwa huko Chibok.
Lakini Boko Haram wenyewe hawajawahi kuthibitisha makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano na hakuna dalili zozote za kuachiwa kwa wasichana haohivi karibuni.
Lakini kwa wale waliobahatika kutoroka, matatizo ya kisaikolojia bado yanawasumbua..

AY KUACHIA NYIMBO MPYA NA MSANII TOKA MAREKANI SEAN KING STON




Mama yake na Sean Kingston, Janice Turner maarufu kama Mama Kingston, ameipa promo ngoma mpya ya AY aliyomshirikisha mwanae. Tayari AY na Kingston wameshoot video ya wimbo huo nchini Marekani.
Africa get ready for the SMASH HIT VIDEO@aytanzania ft seankingston!!!!
mdash; Janice Turner (@mamakingston)
October 17, 2014 AY amesema kuwa ukaribu alionao na msanii Mjamaica-Mmarekani, Sean Kingston ni zaidi ya urafiki wa kikazi kiasi ambacho wanachkuliana kama  familia.
AY-and-Sean
AY and Sean”Hivi karibuni AY aliiambia Bongo5 kuwa mama yake Sean humchukulia kama mtoto wake na wanawasiliana mara kwa mara.“Yaani huyu jamaa ananipa support asilimia 100 huwezi kuamini ni mtu ambaye si yeye tu hadi mama yake mwenyewe  tunawasiliana, kwahiyo ni

family yaani” Alisema Ambwene“Mama yake ananichukulia kama mtoto wake, hata kwenye Instagram yangu ana comment, halafu hii yote ni family ambayo mi nikienda L.A ndo watu wangu ambao hua nahang nao”Collabo ya AY na Sean Kingston iitwayo ‘Touch me Touch Me’ inatarajiwa kutoka November.

TAZAMA PICHA ZA MSICHANA MWENYE SURA YA KIUME, ASEMA WANAUME WANAMKIMBIA KUTOKANA NA HALI YAKE


Queen ni mtoto wa 4 kati yya familia ya watoto 5. Ni msichana mzuri na mrembo kimtazamo, lakni tatizo kubwa linalomkabili maishani mwake ni nywele ambazo zimekuwa zikimfanya aonekane kama mwanaume,Akiongea kwa njia ya mtandao, Queen amesimulia kuhusu changamoto anazokumbana nazo kutokana na tatizo hilo.
“Nimerithi hizi nywele toka kwa mama yangu na zilinianza nikiwa na miaka 21. Kadri miaka ilivyozidi kusonga mbele, tatizo hili lilizidi kusambaa mwili mzima.
“Mwanzo nilikuwa najisikia vibaya sana maana watu walikuwa wakiniona ni kiumbe wa ajabu, lakini baadae nilizoea na ikanilazimu nikubaliane na ukweli….
Akiongelea kuhusu changamoto za kimahusiano anazozipata ,Queen alikuwa na haya ya kusema:
“Sijabahatika kuwa na mwanaume wa kudumu, wengu hunikimbia kutokana na hali hii”




25Oc

. Picha Za Sherehe Ya Siku Ya Msanii Ilivyoadhimishwa Tanzania.

Siku ya msanii duniani imeadhimishwa Tanzania 25/October/2014 Mlimani City kwenye sherehe iliyohudhuriwa na Wasanii na wadau wa sanaa Tanzania. Mgeni rasmi wa sherehe hii alikuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. 
Hizi picha za sherehe yote na wasanii waliofanya show.