.

Jumapili, 5 Januari 2014

MCHINA ASHITAKIWA KWA KUCHANA NOTI YA SHILINGI ELFU 10


Raia wa China ambaye ni meneja uzalishaji katika kampuni ya ujenzi  Shen Hai,46, amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuchana noti ya shilingi 10,000 ambayo ni mali ya Serikali ya Tanzania.

Akisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mkoa Janeth Masesa, Mwendesha Mashtaka wa Serikali,   Castus Ndamugobas alidai kuwa Mchina huyo alitenda kosa hilo mnamo Desemba 3 mwaka jana katika maeneo ya uwanja wa ndege Wilaya ya Ilemela majira ya saa 10:30 jioni ambapo kwa makusudi aliichana noti hiyo  yenye namba AY3748043, ambayo  thamani yake ni Sh10,000 mali ya Serikali ya Tanzania.

Mshtakiwa huyo ambaye ni meneja mzalishaji aliyeajiriwa na Serikali ya Tanzania ili kufanya ukarabati katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza, alikana mashtaka yote na alirudishwa rumande baada ya kutokidhi masharti ya dhamana na hakimu Masesa aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 8 mwaka huu ambapo itafikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa tena.

Kitendo  hicho cha raia huyo wa China kuchana noti kilionyesha dharau kwa nchi ya Tanzania na raia wake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni