.

Alhamisi, 14 Novemba 2013

MWIMBAJI MKONGWE SQUEEZER AZILAUMU REDIO KUDIDIMIZA WASANII WAKONGWE


Squeezer ametoa wimbo mpya unaoitwa ‘Mtemi Pesa’ aliomshirikisha Belle 9, kama jina linavyojieleza wimbo huo unazungumzia jinsi pesa inavyotawala kila kitu.

Akizungumza na kipindi cha Planet Base cha Planet FM Morogoro, Squeezer ambaye pia ni kaka wa rapper wa kike Dataz amesema baadhi ya vyombo vya habari vinachangia katika kuwadidimiza wasanii wakongwe kutokana na baadhi yao kuwabeba wasanii wapya kutokana na kuwa na masilahi nao.

“Mi nafikiri kuna baadhi ya media zinadidimiza wakongwe kwa makusudi kwa sababu wanajua wana nguvu hiyo na wanaweza, na hiyo yote ni kwasababu ya kuweza kuwamiliki ambao wanaweza kuwalipa kile kidogo walichonacho”.

Rapper huyo wa ameongeza kuwa wasanii wapya hawajui thamani yao tofauti na wasanii wakongwe kama yeye wanaojitambua.
-Bongo5.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni