.

Jumapili, 5 Januari 2014

BEAT YA PROFESA JAY NIKUSAIDIAJE YAWAUNGANISHA TENA JOSE CHAMELEONE NA MDOGO WAKE WEASEL

Unaikumbuka beat ya wimbo wa Profesa Jay ‘Nikusaidiaje’ aliomshirikisha Ferooz? Ni beat kali iliyopigwa na Godfather wa Bongo Flava, P-Funk Majani aka Kinywele Kimoja. Beat hiyo ilitumiwa tena miaka saba ijayo na ndugu wa Uganda, Jose Chameleone na Weasel katika wimbo wao uliohit, Bomboklat.

Hata hivyo kwa muda mrefu ndugu hao walikuwa hawaelewani wala kuzungumza. Habari njema ni kuwa mwaka mpya 2014 umekuja na baraka zake ambapo mafahari hao waliamua kuweka tofauti zao pembeni kwenye show ya ‘UG Dance Mix End of Year Party’ iliyofanyika kwenye hoteli ya Sheraton jijini Kampala.

Baada ya kundi la Goodlfye linaloundwa na Radio na Weasel kutumbuiza,  Chameleone alipanda jukwaani akiwa amevalia nguo nyeupe. Aliimba huku fataki zikipigwa hewani kuukaribisha mwaka 2014. Kisha alisimama na kuwaambia mashabiki amewaandalia surprise ya mwaka.

Chameleone na Weasel wakatumbuiza kwa pamoja wimbo wao, Bomboklat na kuufanya umati uliokuwa ukishuhudia ukulipuka kwa shangwe. Baadaye Chameleone alimuita Radio na watatu hao wakaahidi kuyaacha yaliyopita ili wagange yajayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni