.

Jumatano, 15 Januari 2014

Huyu Ndio Mtoto Wa Rapper Octopizzo, Atasikika Kwenye Wimbo Wake Mpya



Akifata nyayo za wasanii kama Will Smith, Jay Z, Eminem na 50 Cent waliohusisha watoto wao kwenye kazi zao za sanaa rapper Octopizzo kutoka Kenya ametangaza kuwa mtoto wake wa kike Tracy atashirikishwa kwenye wimbo wake mpya.


Octopizzo, anayeonekana na Tracy sehemu nyingi mjini Nairobi amekuwa busy sana toka mwaka uanze akijipanga kudondosha wimbo mpya anaotaka ufanye maajabu mwaka 2014. 

Tracy mtoto wa Mr Kibera aka Namba Nane atakuwa amepata zali la colabo wakati anazurura na Baba yake tu, Mashabiki wa Octopizzo wanasema rapper huyu kuwa na ubunifu wa kazi mpya ndio kitu kinachomfanya abaki juu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni