.

Jumanne, 7 Januari 2014

JINSI MBWA 120 WALIVYOMTAFUNA MJOMBA WA KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI


Walimvua nguo na kumtupa kwenye ngome ya Mbwa wenye njaa 120

.Rais Kim Jong Un alikataa mjomba wake kunyongwa bali kuliwa na mbwa akiwa uchi wa mnyama

.kiongozi huyo na viongozi wengine 300 walishuhudia ukatili huo wa kutisha

.Adhabu hiyo iitwayo ‘Quan jue’ ilidumu kwa saa moja

.Mjomba wake alishtakiwa kwa hila na rushwa na matumizi mabaya ya madaraka

Na Damas Makangale, kwa Msaada wa Mtandao

Taarifa zilizovuja kutoka mashirika mbalimbali ya habari duniani ni kwamba Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un alishuhudia jinsi mjomba wake Jang Thaek akiliwa na mbwa karibu 120 akiwa uchi wa mnyama kama adhabu mbadala badala ya kunyongwa.

Taarifa zinasema kuwa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini aliamuru mjomba wake avuliwe nguo zote na kubaki uchi wa mnyama na kisha mbwa kumtafuna akiwa hai mpaka kifo chake, watetezi wa haki za binadamu wanasema ni adhabu ya kikatili ambayo dunia haijawahi kushuhudia kwa miongo kadhaa.

Watu wa karibu na wanafamilia wanasema Mjomba wake huyo alipelekwa kwenye ngome hiyo na wasaidizi wake watano na kuachiwa kwa mbwa wenye njaa ya siku tatu ili waweze kumshughulikia.

Maelezo ya kutisha yaliojitokeza katika ripoti katika gazeti la Straits Times la Singapore , ambayo lilisema kitendo hicho ni cha  kutisha na kinajulikana kama ‘ Quan jue ‘, au ‘ utekelezaji wa adhabu kwa kutumia mbwa wenye njaa.

Thaek , alivaa suti ya bluu na pingu akisindikizwa katika mahakama ya Desemba 12, aliuawa na mbwa mwitu , kulingana na ripoti kutoka China.

Taarifa zinaongeza kiongozi huyo wa Korea ya Kaskazini Kim Jong- Un alikuwa anatoa ujumbe katika sikukuu ya mwaka mpya kwa wakorea wote nchini humo.

Wachambuzi wanasema kiongozi huyo jeuri alikuwa na ujumbe maalum kwa viongozi walioalikwa kwenye sherehe ya kifo cha mjomba wake kama onyo kwamba wanapaswa kufuata taratibu na endapo kiongozi yeyote atakiuka taratibu adhabu kali itachukuliwa dhidi yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni