.

Jumapili, 5 Januari 2014

Picha za mwanzo za uthibitisho kuhusu tukio la watu waliorushwa baharini kutoka kwenye boti wakitokea Pemba

Naambiwa hii picha ni wakati alipookolewa mmoja wa watu waliorushwa kwenye maji kutokana na dhuruba iliyoipata boti hiyo.
Naambiwa hii picha ni wakati alipookolewa mmoja wa watu waliorushwa kwenye maji kutokana na dhuruba iliyoipata boti hiyo.
Suleiman Masoud ambae yuko msibani Zanzibar kwa sasa amethibitisha kwamba ndugu zake watatu ambao ni watoto wa shangazi yake wamepotea saa kadhaa tu baada ya kutoka Pemba safarini kuelekea Unguja.
Anasema ‘katika waliokwenda kutambua miili kaka mtu baada ya kuona maiti ya mdogo wake amezimia, watoto wa Shangazi ni watatu wamepotea ili mpaka sasa maiti ya pili imeonekana’
Suleiman Masoud akiwa msibani Mwanakwerekwe Zanzibar leo baada ya kupata taarifa za watoto watatu wa shangazi yake kupotea.
Suleiman Masoud akiwa msibani Mwanakwerekwe Zanzibar leo baada ya kupata taarifa za watoto watatu wa shangazi yake kupotea.
‘Jinsi ilivyotokea kwa watoto hawa watatu, walikabidhiwa kwa mama mmoja Pemba ili awatizame kwenye meli ambapo kabla ya boti kufika Nungwi ndani ya boti joto lilizidi hivyo mmoja akawa kapakatwa na huyu mama na wawili ndio wakatoka nje kwenda kupunga upepo ndio wakakutana na hiyo dhoruba wakazolewa na hakuwaona tena kuanzia hapo’
Wakati naipandisha hii stori Suleiman ameniandikia msg inayosema ‘mwili wa mtoto wa pili kati ya watatu waliopotea, umeonekana pia’

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni