.

Alhamisi, 23 Januari 2014

DR.SLAA:BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LIMECHOKA KABLA HALIJAANZA FANYA KAZI


Katibu mkuu wa Chadema Dr. Willbrod Slaa amesema kwamba baraza jipya la mawaziri lililoteuliwa na kutangazwa jana na katibu mkuu kiongozi limechoka kabla halijaanza kufanya kazi.

Aidha Dr. Slaa amesema kuwa uteuzi wa Mwigulu Nchemba kama naibu waziri wa fedha (sera) ni mkakati wa CCM kujichotea fedha za uchaguzi mkuu ujao hivyo tutarajie EPA nyingine.

Uteuzi wa Mwigulu Nchemba, Dr. Asharose Migiro, Adam Malima, Saada Mkuya, Jenista Mhagama na kurejeshwa kwa Dr. Shukuru Kawambwa kumezua manung'uniko mengi huku wengi wakihoji uwezo wao kiutendaji.

Dr Migiro anakuwa waziri wa katiba na sharia huku akielezwa kama miongoni mwa waliobeba maslahi ya CCM kwenye mchakato wa katiba mpya hususan kwenye madaraka ya rais na muundo wa muungano. Saada, Nchemba na Malima wamekabidhiwa wizara nyeti ya fedha na uchumi ambapo imedaiwa kuwa uwezo wao kiutendaji hauwezi kuiletea ufanisi wizara hiyo huku wengi wakitilia shaka uteuzi wa Nchemba kiuadilifu ambapo amekuwa akionyesha chuki za wazi kwa Chadema na viongozi wake na kukosa kabisa staha pale anapochangia bungeni.

Kawambwa na Jenista wamepewa jukumu la kuongoza elimu ambapo Kawambwa alionyesha dhahiri kushindwa vibaya kuongoza sekta hiyo nyeti kabla ya uteuzi mwingine wa jana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni