.

Jumapili, 5 Januari 2014

Jik, Maji ya betri, na Dawa ya Malaria 'Metakelfin' zatumika Kurefusha na Kurembesha Nywele....!!


Tabia ya kutumia vitu vyenye kemikali bila ya ushauri wa kitaalamu imeendelea kujijenga miongoni mwa Watanzania, ambapo sasa dawa ya malaria aina ya Metakelfin  inatumika kutengeneza kipodozi cha kurembesha nywele.
 
Matumizi hayo hatari ya Metakelfin yamegundulika huku kukiwa na taarifa za maji ya betri za magari, kutumika kama malighafi ya kutengeneza mkorogo unaotumiwa na baadhi ya wanawake kuchubua ngozi zao.


Utafiti uliofanywa hivi karibuni na shirika lisilo la kiserikali la Envirocare linalojihusisha na mpango wa  kupunguza madhara yatokanayo na bidhaa za vipodozi kwa binadamu na mazingira, umebaini dawa ya malaria aina ya  Metakelfin ni mojawapo ya kemikali inayotumika kienyeji  katika kutengeneza kipodozi cha kurembesha nywele.

Kwa mujibu wa mtafiti  Issai Sen’genge, Metakelfin ni miongoni mwa kemikali inayotumika kutengeneza mchanganyiko wa kulainisha na kurefusha nywele.

Alisema idadi kubwa ya waliohojiwa, waliitaja dawa hiyo ya malaria kuchanganywa  ndani ya dawa nyingine za nywele ili kupata mchanganyiko ambao husaidia kurembesha nywele.

Swali lilikuwa kama kuna vitu vinavyotumika katika kutengeneza mchanganyiko wa kupaka kwenye ngozi au nywele, waliohojiwa walikiri kuchanganya, Metakelfin, Jik, maji ya betri na kemikali nyingine,” anasema Seng’enge.

Kwa upande wake, Maria Kimiro ambaye ni mmiliki wa saluni ya wanawake iliyopo  Makongo jijini Dar es Salaam, alikiri kusikia matumizi ya vidonge katika vipodozi lakini hana uhakika wa aina ya dawa hizo.

Nakumbuka kuna mtu nimeshawahi kumsikia anazungumzia vidonge katika masuala ya vipodozi, lakini sina uhakika kama ndiyo hiyo Metakelfin au vidonge vingine,”anasema Kimiro.

Asha Rashidi mkazi wa Tabata jijini Dar es salaam, alikiri kuwa katika kutafuta urembo wanawake wanatumia vitu mbalimbali hata vinavyohatarisha maisha ili mradi kutimiza azma yao.

Anasema kuwa hali hiyo mara kwa mara imekuwa ikisababishwa na kuiga au kusikia kutoka kwa wengine bila kufikiria madhara ya ambacho anatarajia kukifanya.

“Binafsi sijawahi kutumia hiyo Metakelfin kwa kuwa  nafahamu ni dawa ya malaria lakini naamini kuna watu ambao wanaweza kuichakachua kwa namna wanavyoweza wakidhani kwamba  inaweza kuwa na matokeo mazuri kwenye ngozi au nywele,” alisema.

Wataalamu wa afya wanazungumziaje

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni