.

Jumatatu, 30 Desemba 2013

Hizi ndizo sababu zilizofanya Haruna Moshi’Boban’ kutoongezewa mkataba


images2Makamu Mwenyekiti wa Coastal  Union Steven Mnguto timu yenye makao yake makuu pale 96.o Tanga ame-amplify taarifa zinazomhusu mwanasoka Haruna Moshi’Boban’ kuhusu mkataba wao na Boban.
imagesCoastal Union wamesema hawatomuongezea mkataba mshambuliaji Haruna Moshi ‘Boban’ kutokana na kuwa na utovu wa nidhamu.Steven Mnguto alisema mpaka sasa mshambuliaji huyo hajaripoti kambini kuanza mazoezi na wenzake na hajatoa taarifa yoyote.
LOGOSMnguto ameongeza kwa kusema kuwa kwa tabia aliyoionyesha ni ngumu kumuongeza mkataba mshambuliaji huyo aliyebakiza miezi sita tu katika mkataba wake unaomalizika mwishoni mwa msimu huu.Kutokana na kutojiunga na kikosi hicho mpaka sasa.
Boban atakatwa mshahara wake wa mwezi huu kwa kuwa hajaufanyia kazi yoyote tokea alipotakiwa kujiunga na wenzake  tarehe 1 Desemba mwaka huu,mbali na Boban adhabu ya namna hiyo pia itamkuta kiungo Jerry Santo ambaye ni raia wa Kenya kutokana na kutotoa sababu zozote za kuchelewa kujiunga na wenzake kambini.
‘Ni bora tukapandisha vijana wetu wa U20 kwa kuwa tunajua watatusaidia na wana nidhamu ya hali ya juu kuliko hawa ambao ni wazoefu lakini wanatusumbua upande huo’.
‘Hatuwezi kumuongeza mkataba mtu ambaye tunaona kabisa nidhamu yake haituridhishi kama timu na hajatoa hata taarifa yoyote.  Wa nini mtu kama huyo?  Sisi tunaangalia maslahi ya timu ili ifanye vizuri’. .
Kwenye kumbukumbu Boban aliwahi kuondolewa  kwenye kikosi cha timu ya Simba ambacho alikuwa amekitumikia kwa muda mrefu kutokana sababu za kiutovu wa nidhamu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni