.

Jumanne, 19 Novemba 2013

Picha na taarifa za mauaji yaliyotokea ilala tar 19nov 2013



IMG_0691 Jumanne ya tarehe 19nov2013 asubuhi kupitia power breakfast ya Clouds Fm wakati kipindi kikiendelea nilisikia taarifa ya mtu kushambulia kwa risasi kisha nae kujidhuru kwa kujiua kwa kutumia bastola.
IMG_0699                   Club ya wazee-ilala.
Tukio hilo ambalo kupitia shuhuda aliyekua akiripoti alisema limetokea asubuhi majira ya saa moja nyumba jirani na club ya wazee maeneo ya ilala.
Niliamua kulifatilia kwa undani ili kujua sababu na kupata maelezo ya mashuhuda ana kwa ana,Nilifika eneo la tukio lilipotokea mkabala na club ya wazee ilala,ambapo nilianza kufanya interview na mtu anaefanya usafi pale club ya wazee na pia ni shoe shine wa mitaa ile ambaye alikuepo mwanzo hadi mwisho wa tukio.
IMG_0703                                                                 Shuhuda.
Maelezo ya shuhuda huyu ni haya ‘ilikua ni sa 1 na nusu,wakati tunamalizia kufanya usafi wakati ndo tunatoka nje tukasikia milio ya risasi yani,baada ya kusikia milio ya risasi ikabidi tutoke nje,tuliposogea tukaona mshkaji[muuaji]anazunguka upande wa pili wa mwanamke kwa sababu ile gari ilikua na watu wanne ndani aina ya toyota surf rangi nyeupe baada ya hapo ikabidi tuangalie kinachoendelea ni nini tukaona mshkaji[muuaji] anaingia ndani,akatoka akarudi tena kwenye gari akaanza kupiga risasi kwa abiria waliokua ndani ya gari.
Ndani ya gari kulikua na abiria watatu na dereva mmoja jumla ya watu waliokua kwenye gari walikua wanne tukaona jamaa ameanza kufyatua risasi kwa yule dada aliekua amekaa mbele,baadae akafyatua tena kwa kaka aliyekua pia mbele,kisha akafyatua kwa abiria mmoja aliyekuia ndani ya gari’.Hayo maelezo mafupi ya shuhuda huyo wa kwanza.
IMG_0696            Nyumba yenye gheti jeusi ndo nyumba waliyokua wakitokea watu walioshambuliwa kwa risasi.
Sikuishia hapo nikaenda myumba ya tatu kutoka nyumba yaliyotokea mauaji haya,ambapo nilimkuta mama aliepiga simu polisi kuwapa taarifa juu ya mauaji na ndiye aliyekua wa kwanza kusambaza habari kwenye vyombo vya habari.
IMG_0697    vipande vya vioo vilivyovunjika kutoka kwenye toyota surf iliyoshambuliwa.
Maelezo ya mama yalikua hivi ‘siweze kukumbuka ilikua ni asubuhi ya sa ngapi lakini ni kati ya sa 12 na nusu asubuh na sa 1 na nusu asubuhi,mimi nikiwa nyumbani kwangu nyumba kama ya tatu kutoka kwenye nyumba ya tukio nuilisikia milio ya mlipuko wa risasi ni zaidi ya milipuko mitatu,nikaweza kupiga simu kwa askari polisi bahati nzuri  namba yake ninayo kwenye simu na akaniomba nidrop simu yangu haraka ili aweze kufanya mawasiliano ya radio ya polisi,na baada ya hapo mimi nikateremka chini kwenda kuangalia hali halisi ni nini.
Nikakuta kuna gari aina toyota hilux surf ya rangi nafikiri ya Gold mettalic ikiwa na majeruhi watatu-wawili samahani ndani kuna kaka mmoja na dada mmoja kaka akiwa anapumua na dada nae akiwa anapumua,na majeruhi watatu alikua kalala kwenye geti ya nyumba ya jirani na nyumba ya tukio nae akiwa anapumua.
IMG-20131119-00050

Aliyekua dereva kwenye gari iliyopigwa risasi.
Hali halisi ni kwamba aaah majeruhi hawa watatu tulipowakuta bado wanapumua mimi nikapiga tena simu polisi kuuliza kama tunaweza kubeba hiyo miili kwa sababu hatujui taratibu za kipolisi zikoje,kwa hiyo tulifanikiwa kumobilise pale watu ambao tulikuepo,tukachukua ile miili bahati nzuri tunaanza kuitoa kwenye magari polisi walifika mara moja’.
IMG-20131119-00045           Muuaji aliyeamua kujiua.
Taarifa kamili juu ya mauaji haya ya kusikitisha zitaendelea,ambapo utasikia alichokizungumza kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi ilala.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni