.

Ijumaa, 22 Novemba 2013

MUONEKANO WA JUKWAA LA P~ SQUARE LIVE IN DAR HATUA ZA MWANZO HATARIIIIIIIIIIII!!!!!!!!!!! TAZAMA MAPICHA HAPA







Ikiwa imebaki siku moja tu kabla ya show ya kihistoria inayosubiriwa na wengi kufanyika ndani ya viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam, tayari jukwaa litakalotumiwa na wasanii wanne kutoka hapa nyumbani na wale wakali wa kulishambulia jukwaa barani Afrika P~Square lipo katika maandalizi ya mwisho mwisho pamoja na kufunga mziki.
Jukwaa lina sehemu tatu za kupandia juu yaani ngazi na vijukwaa vidogo viwili kama winchi vilivyopo katikati ya stage. Imefungwa sound yenye mjumuiko wa spika zaidi ya sitini ambapo ufungaji wa sound unaendelea sambamba na kufunga stage ambayo inaweza kukamilika siku ya kesho. Kumbuka kuwa wasanii watakao-perform jukwaa moja na P` Square ni Malkia wa Bongo fleva mwenye miaka kumi na tatu kwenye gemu Lady Jay Dee a.k.a Anaconda, King wa R&B Ben Paul, mwamba wa kaskazini Joh Makini na MC shupavu au Heavy weight Mc au Daddy Joseph Haule wa Mitulinga Mchawi wa Rhymes. Hii si ya kukosa kwasababu kwa mara ya kwanza utashuhudia show nzima ikidondoshwa kwa style ya kupiga live band.
Na hizi ni baadhi ya picha zikionesha jukwaa hilo likiwa liknaendelea kutengenezwa


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni