.

Jumanne, 19 Novemba 2013

Wafanyabiashara Kariakoo Warudi Kazini.



IMG_0714Wafanyabiashara wa soko la Kariakoo,Kwa pamoja wamekubaliana leo tarehe 20nov2013 kufungua maduka yao na kuendelea na shughuli zao za kila siku.
IMG_0723Wafanyabiashara eneo la Mtaa wa Kongo

Wakizungumza na Millardayo.com wafanyabiashara hao wamekubali kufungua maduka yao kufuatia kauli ya mkuu wa mkoa wa Dsm Said Meck Sadiki kuwataka wafanyabiashara hao kuendelea na biashara zao kwani suala lao litaenda kujadiliwa upya bungeni
IMG_0707                                                                              Mitaa ya Big Bon
Wafanyabiashara hawa wameingia kwenye mgomo wa siku mbili kuishinikiza serikali kupunguza bei ya uuzwaji wa mashine zitolewazo na TRA kwa ajili ya kutoa risiti.
Ambapo mbali na uuzwaji wa bei kubwa kwa hizi mashine pia wameomba kupunguzwa kwa asilimia 18% ikatwayo na Mamlaka Ya Mapato Tanzania[TRA].

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni