.

Alhamisi, 21 Novemba 2013

Unajua kama Pesa ya Blue ilitoka kwa Natorious Big??


BL Ukizungumzia wasanii walioanza Game ya muziki wa bongo fleva wakiwa na umri mdogo huwezi kosa jina la mr.blue katika list hiyo.
Blue ambaye ni baba wa mtoto mmoja,ni miongoni mwa wasanii wachache walio kwenye GAME muda mrefu na bado wameendelea kufanya vizuri,millardayo.com imepiga story na BLUE kufahamu idea ya ngoma ilipotoka na mafanikio yake mpaka sasa juu ya kazi hiyo pekee inayofanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya radio.
BLUE
‘Dah idea ilikuja tu ilikuja kutokana na siku hiyo nakumbuka  nilikua natembea na gari nikiisikiliza ile beat,nakumbuka siku hiyo pia nilikua nikizisikiliza sana nyimbo za Notorious Big ndo nakumbuka nikaanza kufatilia historia yake ghafla namimi nikaanza kujifikiria nilipotokea na nilipokuepo nikajikuta nikianza kuandika nyimbo ya pesa taratibu.
Nyimbo ya pesa niliandika allmost mwezi mmoja na nusu,nilikua nikiandika verse moja baadae verse nyingne kwa sababu muda ulikua mchache na ilikua nikiingia kwenye gari ndo naanza kuiandika.
Nyimbo ya pesa pekeake mpaka sasa inaenda kunipa show ya ishirini na kuhusu call back tone saiv ndo nimeiandikisha hivyo bado sijaanza kupokea malipo rasmi.kwa haraka haraka pesa kwa sasa iv inaweza kufikia zaidi ya milion 10 chapu chapu na bado tunaendelea kula pesa.
Video ya pesa nilipanga niifungie mwaka hivyo sijajua mwenyezi nae kunja kitu kingine amepanga au mbele itakuaje  ila nimepanga kufanya video ambayo itakua kali maana ndo soko la muziki wangu lilipo pia.
Nimeongea na Ogopa na pia nafatilia kwa Adam Juma japokuwa nimesikia amesimamisha kushoot video lakini nimeongea na watu flani wa karibu na kwamba naweza nikafanya nae kama itakua vizuri’
Jipange kwa ajili ya kushuhudia video ya pesa ambayo ameahidi itatoka ndani ya miezi miwili kutoka sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni