.

Jumanne, 19 Novemba 2013

Taarifa za Ismail Aden Rage kusimamishwa Uenyekiti wa Simba na sasa anaeongoza ni huyu.



RageSimbaKamati ya  utendaji ya klabu ya Simba iliyokutana jana usiku imempiga stop Ismail Aden Rage kuendelea na ubosi katika klabu ya Simba na kulibadilisha benchi la ufundi isipokuwa nafasi ya meneja Madaktari wa timu ambapo pia kwa sasa wanamtarajia ZDRAVOK LOGARUSIC kutoka Croatia.
 Akizungumza kwa niaba ya kamati ya utendaji, mjumbe wa kamati ya utendaji Joseph Itangare amesema wamemsimamisha mwenyekiti kutokana na kufanya maamuzi yake binafsi bila kushirikisha kamati ya utendaji ikiwemo kutoitisha vikao vya kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara ya 31 (1)ya katiba ya simba.
Kingine alichosema Itangare ni ‘vilevile mwenyekiti huyo amesaini mkataba wa kukiuuza kipindi cha Simba tv bila kushirikisha kamati ya utendaji’
Mzee Kinesi
Hii picha hapa juu ni Mzee Kinesi ambae namkariri akisema ‘kwa sasa lazima twende kikatiba, Mwenyekiti kama hayupo ngazi inayofatia inapanda juu na tunachagua Mjumbe mwingine ili kukaa kwenye nafasi iliyobakia, kwa muda huu wa matayarisho ya mkutano mkuu ujao mimi nitakaimu kama Mwenyekiti wa Simba na Swed atakaimu kama makamu Mwenyekiti’ (picha kutoka kwa salehjembe.blogspot.com)
Kwenye sentensi nyingine, Kinesi amesema ‘Mwenyekiti tumemsimamisha lakini tusubiri maamuzi ya mkutano mkuu ambao utafanyika kwa ajili ya marekebisho ya katiba, kuna mengine yamekiukwa hivyo yatawasilishwa kwenye mkutano mkuu tarehe 1 December’
‘Kutokana na timu yetu kutofanya vizuri, tumeamua kwamba benchi la ufundi tulifumue ili tulijenge upya, sasa litaongozwa na kocha aliekua na Gor Mahia ZDRAVOK LOGARUSIC amekubali kuja na ataanza mazoezi tarehe 2 December na kwa pamoja tumekubaliana ndie atakua kocha mkuu, pia tumekubaliana Matola ndio awe msaidizi wake kwa muda, hatumuondoi Simba B moja kwa moja kuhofia kutetereka’

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni