.

Jumanne, 4 Novemba 2014

Ukimya wa kiongozi mpya wa al-Shabaab waibua dhana

Punguza OngezaKaribia miezi miwili baada ya al-Shabaab Ahmed Omar kuchukua nafasi ya kiongozi muuaji Ahmed Abdi Godane, bado ni mambo machache yanajulikana juu yake, kusudio lake na uwezo wake wa kuongoza kikundi kilichojitenga cha al-Shabaab.

  • Mambo machache yanajulikiana kuhusu kiongozi mpya wa al-Shabaab Ahmed Omar, anayejulikana pia kama Abu Ubaida. Wapiganaji wa al-Shabaab walio katika picha hapo juu nchini Somalia katika picha isiyo na tarehe. [AFP]
    Mambo machache yanajulikiana kuhusu kiongozi mpya wa al-Shabaab Ahmed Omar, anayejulikana pia kama Abu Ubaida. Wapiganaji wa al-Shabaab walio katika picha hapo juu nchini Somalia katika picha isiyo na tarehe. [AFP]
  • Wakaazi wa Mogadishu wakiangalia habari tarehe 6 Septemba, siku ambayo al-Shabaab anayejulikana kama Ahmed Omar kuwa mrithi wa muuaji kiongozi wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane, katika skirini kulia. [Mohamed Abdiwahab/AFP]
    Wakaazi wa Mogadishu wakiangalia habari tarehe 6 Septemba, siku ambayo al-Shabaab anayejulikana kama Ahmed Omar kuwa mrithi wa muuaji kiongozi wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane, katika skirini kulia. [Mohamed Abdiwahab/AFP]
Baadhi ya wachambuzi wamesema kuendelea kw aOmar kuwa kimya kunaonyesha kwamba hana ujuzi wa uongozi kurejesha hamasa ya al-Shabaab kufuatia kifo cha Godane, hasara ya kijeshi ya mfulululizo na kuongezeka kwa idadi ya wanaoasi miongoni mwa wapiganaji wa al-Shabaab.
Wengine wanatahadhari, hata hivyo, kuwa bado ni mapema kueleza namna Omar alivyo, anayejulikana kama Abu Ubaidah, ataongozaje kikundi hiki na katika mwelekeo upi anaopanga.
Omar, aliyekuwa karibu na Godane, amekuwa akipigana na al-Shabaab kwa muda mrefu, lakini alibakia kuwa msiri hata katika kikundi hicho, alisema Mohamed Farah Ali al-Ansari, aliyekuwa kiongozi wa al-Shabaab aliyejisalimisha kwa serikali ya Somalia 2010 na sasa anaongoza vituo vya serikali vya urekebishaji wa wanamgambo hao.
"Abu Ubaidah anafikiriwa kuwa na kama miaka hamsini," al-Ansari aliiambia Sabahi. "Alizaliwa katika wilaya ya Luuq huko Gedo ambapo ndiko familia yake iliko."
Kabla ya kujiunga na al-Shabaab, kati ya 1997 na 2006, alikuwa sehemu ya kikundi cha al-Itihaad al-Islamiya na Brigedi ya Ras Kamboni ambayo ilikuwa inaongozwa na Hassan Abdullah Hersi al-Turki.
"Baadaye alikuwa mmoja wa maofisa wa ngazi ya chini katika Umoja wa Mahakama za Kiislamu," al-Ansari alisema. "Wakati Umoja wa Mahakama za Kiislamu ulipokuwa dhaifu kueleka mwishoni mwa [ 2006], alifanya kazi kwa karibu na [aliyekuwa kiongozi wa al-Shabaab] Aden Hashi Farah Ayro. Alifanya kazi kama makamu wa Godane baada ya kifo cha Ayro [2008] hadi sasa ."
Omar siyo mtu msomi, al-Ansari alisema. "Sifikirii kwamba hata alifikia ngazi ya elimu ya juu," alisema, akiongezea kwamba Omar alisoma masomo ya dini wakati akiwa sehemu ya Ras Kamboni na anazungumza na kuandika kwa Kisomali na Kiarabu.
Ingawaje Omar hajachukua hatua kwa lengo dhahiri la kujificha kwa umma, wapiganaji wa al-Shabaab hawamjui vizuri kwa sura au tabia, na kwa kiasi kikubwa hajulikani nje ya kikundi hicho anachoongoza sasa, al-Ansari alisema.
"Mwaka 2010, [Omar] kwa muda mfupi alikuwa gavana wa Bay na Bakol, lakini aliondolewa katika nafasi hiyo baada ya muda mfupi" alisema.

Kulinganisha viongozi wa zamani na wa sasa wa al-Shabaab

Omar kukosa elimu na uzoefu wa uongozi kunaonyesha kwamba pia anakosa uwezo wa msingi kuongoza kikundi kama al-Shabaab, alisema Abdirahman Isse Addow, aliyekuwa msemaji wa Umoja wa Mahakama za Kiislamu na sasa mkurugenzi wa Redio Mogadishu.
"Kiongozi mpya ni mtu asiye na elimu kubwa ambaye hana jina linalojulika vizuri [ndani ya vyeo vya al-Shabaab], hivyo itakuwa vigumu kwake kuunganisha pamoja kazi mbalimbali za kikundi hiki," aliiambia Sabahi.
Kinyume cha hayo, alisema, "Godane alikuwa mtu mwenye elimu, alimaliza chuo kikuu, alikuwa kwenye nchi za kigeni, alikuwa na mafungamano makubwa na alikuwa na uzoefu mkubwa."
"Godane alikuwa na uwezo mkubwa kwenye kundi hili," alisema, akiongeza kwamba kiongozi huyo wa zamani alikuwa hodari na aliutumia uongozi wake kuyadhibiti makundi mbalimbali kwenye himaya yake.
"Aliwatishia baadhi, kuua baadhi, kuwahonga baadhi na baadhi kuwafukuza, kama vile wageni ambao ushawishi wao anauzuia sana," Addow alisema. "Alikuwa mwangalifu sana kuhusu yeyote aliyekuwa anamzoea na kujua mengi kumhusu."
Kwa hiyo, Omar ni uchaguzi mbaya wa kuchukua nafasi ya kiongozi kama Godane, ambaye alichukua tahadhari nyingi na kujitayarisha kuwa kiongozi kutoka mwanzo, Addow alisema.
"Godane alikuwa anajitayarisha kuwa kiongozi [tokea siku za nyuma] mwaka 2005. Hakutoa nafasi kwa mtu yeyote kumfahamu, alikataa kupigwa picha, alikuwa mwangalifu kuhusu gari aliloendesha na kupunguza idadi ya watu aliokutana nao," Addow alisema, akiongeza kwamba Omar hajachukua tahadhari yoyote kama hiyo na aliishi kama mtu wa kawaida.

Mchakato wa kurithi hauko wazi

Bado haieleweki namna Omar alivyochaguliwa au kuteuliwa kuiongoza al-Shabaab. Baadhi ambao wanakifahamu kikundi wanasema alichaguliwa kwa kuzingatia uchaguzi wa mwisho wa Godane, wakati wengine wanasema alichaguliwa na watu wa ndani walioaminiwa na Godane, ambao walimuona Omar kama anayefaa zaidi.
"Kwa kuzingatia taarifa nilizonazo, Abu Ubaidah alikuwa wa kwanza katika orodha ya watu watano ambao Godane alisema wanapaswa kuchukua uongozi kwa mfuatano," Addow aliiambia Sabahi, akikataa kutaja wengine wowote katika orodha isipokuwa kwa Mahad Mohamed Ali "Karate", ambaye pia alikuwa miongoni mwa washirika wa karibu wa Godane.
"Abu Ubaidah alikuwa karibu sana na Godane," alisema. "Alihusika na kuratibu na kudhibiti majimbo. Alizoea kwenda katika vijiji vingi kukusanya taarifa zinazohusiana na al-Shabaab, hasa kuhusu watu wanavyowachukulia."
Hata hivyo, Al-Ansari alisema uteuzi wa Omar haukuja tu kutokana na uamuzi wa mwisho wa Godane. Bali, Omar alionekana kama muhimu kutokana na taarifa alizokuwa nazo kwa kuwa alikuwa karibu na Godane kuliko mtu yeyote yule.
"Huyu mtu ana uelewa kuhusu vyanzo vya fedha na taarifa za siri, kama vile uwezekano wa serikali kusaidia [al-Shabaab], mahali ambapo fedha na vifaa vinapitishwa, uhusiano na al-Qaeda, pamoja na [taarifa] kuhusu uhusiano wa ndani," alisema.
Licha ya siri alizonazo, Omar hana sifa nyingine za uongozi ambazo zilifanya achaguliwe, kwa mujibu wa al-Ansari, ambaye aliongeza kwamba inawezekana al-Shabaab itamteua kiongozi mwenye uzoefu zaidi katika miezi ijayo kuwaridhisha wanachama.
Kwa upande wake, Liban Abdi Ali, mwandishi wa habari anayefanya kazi na TV Alhurra iliyoko US aliyekuwa awali akifanya kazi na Redio Mogadishu inayoendeshwa na serikali ya Somalia, alisema uteuzi wa Omar ulikuwa ni matokeo ya mgogoro miongoni mwa watu wa ndani wa Godane.
"Kulikuwa na wanaume wengi ambao walitaka kazi ya uongozi na walimchagua [Omar] kuepuka mgogoro miongoni mwao," Ali aliiambia Sabahi.
Hata hivyo, Ali alisema ilikuwa ni mapema mno kuamua iwapo Omar atakuwa na stadi za haiba na ufasaha wa kuzungumza ambao Godane alifahamika kwa hilo, kwani hakuna hotuba zake za zamani zilizorekodiwa ambazo tunaweza kutathmini.
"Hotuba ya kwanza alinayoitoa itaonyesha kiwango cha uwezo wake," alisema.

Ukimya wa muda mrefu wa Omar

Wachambuzi wanaendelea kushangazwa kuhusu kwa nini Omar amekuwa kimya kwa muda mrefu. Aliteuliwa tarehe 6 Septemba, lakini bado hajatoa hotuba yoyote katika kundi au wafuasi wake, au kutoa tamko lolote kupitia vyombo vya habari.
Kufuatia kushindwa al-Shabaab wamepata shida kuwa chinii ya Jeshi la Taifa la Somalia na vikosi vinavyofungamana nalo, Omar hana ushindi wa kuripoti kwa wafuasi wa al-Shabaab na wapiganaji na anasubiri fursa nzuri, alisema Addow, mkurugenzi wa Redio Mogadishu.
"Abu Ubaidah alichukua nafasi yake wakati al-Shabaab walipokuwa katika kipindi chake kigumu katika historia," alisema. "Anakabiliwa na sababu kubwa kadhaa kama vile upandishwaji mkubwa wa ndani miongoni mwa wanachama wa kikundi, kifo cha kiongozi wake, kupoteza maeneo yake mengi ambayo yalidhibitiwa na kusambaa kwa matatizo ya fedha ambayo kundi limekabiliwa nayo."
Kwa kuwa sio mengi yanayofahamika kumhusu yeye, hotuba ya kwanza ya Omar itatakiwa kuacha alama kwa wafuasi wake, alisema Addow.
"Kwa mfano, anatakiwa kueleza kwa uwazi namna watakavyofanya kazi na al-Qaeda au vikundi vingine vya kigeni, namna watakavyosimamia mikoa [ya Somalia], na namna kundi litakavyoongozwa," alisema. "[Lakini] bado hajaweka wazi upi utakuwa mkakati wa kundi kwa siku zijazo. Inawezekana pia mkakati huo umeshawekwa nje ya nchi na anasubiri kuusikia kutoka katika vyombo vya nje."
Omar Dahir Sheikh Abdirahman, mkurugenzi wa Kituo cha Usuluhishi na Mazungumzo, alitupilia mbali uvumi huo, akisema tukio mbadala ni kwamba Omar ana kazi nyingi za kuandaa operesheni za al-Shabaab, na kutoa hotuba sio muhimu kwake.
"Inawezekana kwamba yeye ni mtekelezaji na sio mzungumzaji," aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba ukimya wa Omar unaweza kuwa sio dalili ya udhaifu na hapaswi kudharauliwa.
"Mtu ambaye alimbadili Godane maarufu, pamoja na kutofahamu sana kuhusu habari zake, anaweza kuwa ni mtu mwenye uwezo ambaye amefanya mengi kwa siri [kwa ajili ya al-Shabaab] na alichaguliwa kwa sababu hiyo," alisema Abdirahman. "Inawezekana kwamba yeye sio mzuri kwa kujieleza lakini ana utendaji thabiti."
"Inawezakana pia kwa sababu za kiusalama anaficha sauti yake na anataka kuzungumza kwa vikundi binafsi badala ya kutoa hotuba kwa umma," alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni