.

Jumatatu, 10 Novemba 2014

Eti Fid Q yuko tayari kumlipa msanii gani ili apige nae kolabo?


Screen Shot 2014-11-09 at 2.25.14 PMSiku hizi zimekuwepo stori kadhaa za mastaa wa muziki hasasa Afrika kuingia kwenye headlines za kulipa Wasanii wakubwa kimataifa sanasana kutoka Marekani ili kufanya nao kolabo, lengo ni kujiongeza au kujisogeza hatua nyingi mbele kwenye muziki wao.
Fid Q ameongea na mtangazaji Millard Ayo kwenye CloudsFM Top20 Jumapili November 9 2014 na kumtaja mwimbaji pekee ambae anaweza kukubali kumlipa pesa ili tu afanye nae wimbo.
Akiwa anatabasamu Fid alijibu >> ‘Kiukweli kabisa bado sijamuona msanii wa kufanya nae kolabo zaidi ya Lauryn Hill, ndio msanii pekee ninaweza kumlipa kufanya nae kolabo kwa sababu miziki yake yote nikiisikiliza huwa inanikosha, ni mshabiki wake kabisa wa damu labda akiniambia nimlipe nitamlipa lakini nauhakika nikikaa nae na kupiga stori kuhusu muziki wake atagundua kiasi gani namuelewa
Kwenye sentensi ya pili Fid Q akiwa na tabasamu kubwa alisema ‘niwe muwazi tu, ni Mwanamke ambae kazaa watoto watano lakini akisema kaachana na yule mtu na anataka aolewe na mimi, naweza nikamuoa pia.. fresh kabisa yani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni