.

Jumapili, 16 Novemba 2014

DJ TASS AWAFURAHISHA WABONGO KWA KUPROMOTE MUZIKI WA NYUMBANI NDANI YA BBA HOTSHOTS

Dj Tass wa Majic Fm na Maisha Magic ya DSTV Ijumaa (Nov. 14) alikuwa official Dj aliyetumbiza kwenye jumba la Big Brother Africa Hotshots jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Tass
Mashabiki wengi wameonekana kufurahishwa na uzalendo aliouonesha kwa kupromote zaidi ngoma nyingi za wasanii wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla katika platform ambayo inaonekana kwenye nchi nyingi za Afrika.
Dj Tass aliyekuwa amevalia T-shirt nyekundu yenye picha za Nyerere na Mandelea, ameiambia Bongo5 kuwa alipewa maelekezo ya kucheza nyimbo za Afrika tu.
“Wamekubali sana, baadhi ya watu wa Channel O nimeongea nao kuhusu muziki wa Bongo kwanini haupati airtime wanasema zingine hawafahamu. Lakini tumepata mawasiliano nao tuweze kuwa nawatumia labda muziki wanachambua ni muziki gani ambao wanaweza wakaucheza kwasababu hata mimi jana nimepewa limit nisicheze nyimbo za nje nicheze nyimbo za Afrika tu, kidogo kama walitaka kunipa wakati mgumu nikajipanga upya tena wakanipa hard disc yao nikaweka kwenye hard disc yao nilivyomaliza nikawaachia ili wabaki wanajua muziki gani ambao nimecheza kwa faida yao.“
Tass aliendelea,
“Vile vile nimehojiwa na Channel O ambayo itaweka kwenye website yao kuhusiana na awards za Channel O. Wameniuliza nani unaona anaweza akachukua, nikasema mi nadhani anaweza akachukua Diamond kwasasabu ni mtu wetu.”
Tass-2
Hizi ni baadhi ya nyimbo zilizokuwa kwenye playlist ya Dj Tass iliyowarusha House mates wa Hotshots jana:
1.Alikiba – Mwana
2. Diamond ft. Davido –Number 1 Remix,
3.Lady Jay dee- Joto Hasira
4. Nay Wa Mitego – Nakula Ujana
5.P-Unit – Una (Kenya)
6.Godzilla –Nataka
7.Juma Nature – Hakuna kulala
8.Yamoto Band – Niseme
9.Majirani – Ndo hivyo kunaendaga (Kenya)
Hizi ni baadhi ya comments za mashabiki kuhusu Dj Tass alivyoupromote muziki wa nyumbani kwenye BBA:
shilolekiuno-@djtass kaka wew ni nyoooookoo coz umejua kuipenda nchi yako na hizo ngoma zako kali!! @bigbrother africa oyooooooo
djebrah-Kila Mtu Anamwaga Sifa Kwako, Hiyo Inaonyesha Wazi Ulichokifanya Kimekubalika, Asie Mwaga Sifa Kwako Na Kukosoa Huyo Ni Mchawi, Baadhi Ya Waliodis Ni Wale Wabongo Wasiopenda Vya Home, Wanapenda Vya Nje Ya Home, Sio Wazalendo, Ki Ukweli Umepiga Kazi Nzuri Sana, Umeiwakilisha Vizuri Tanzania na East Africa Kwa Ujumla, Hadi Tshirt Uliyovaa Umeonyesha wazi wewe ni Mzalendo, hujaenda Kuuza Sura, umeenda Kuiwakilisha Nchi Yako, BIG UP SANA SANA SANAAAA DJ TASS.
sharogangstar_genius-Nilikipenda Sana alichokifanya Jana DJ TASS
ndani ya jumba la Big Brother Africa # Hotshots ,Alionyesha Uzalendo Uliotukuka,maana alicheza ngoma nyingi sana za kibongo. . huku akigusa na za Ki East Africa Kenya na Uganda I mean, Alizipa Muda kimtindo pia Zile Naija na Kwaito… Kuna Dj wa kibongo alishawahi kwenda akaishia kucheza ngoma za wenZetu tu, hakugusa ngoma ya bongo hata moja zaidi ya video ya aliyekuwa mshiriki wa humohumo akiwakilisha TZ, Feza kesi . iliniumaga sana kukosa uzalendo wa nyumbani …. Na ahsante waliomvalisha T-shirt iliyokuwa na picha mbili ya Nyerere na Mandela zilizoungana na kuchora ramani kama ya Africa , huku maandishi yakisomeka AFRICAN HEROES….. ulitishaaaaaaa DJ TASS. Moja kati ya status yangu niliyoiandika leo @djtass
foncethomas-Yeah salute kwake kairusha sana nchi
chichimishi-kanichekesha kweli jamani yani BBA leo kama Maisha Club. Hadi Yamoto Band.
abuujunior-Mwaka huu kweli wamepeleka #DJMtanzania
maryyarot-Kabisa yani ameutendea haki u Tanzania wake @abuujuniour
seycelela_msamba-akija wa nigeria watapiga zao wa south vilevile.. by the way aliekwambia utamu wa nyimbo mpaka uelewe maneno nani?? @ djtass umeuaa baba u nailee t.. @shilolekiuno huyu msambazie upendo naona kajisahau
dvjcon-@shilolekiuno dada umeongea umeonaeeee yaan @djtass kanikosha vilivyo kwa kuilitangaza soko la Tanzania kwa kupiga nyimbo za bongo big up @djtass
nurujw-Mbona si tunacheza makirikir kwan tunaelewa tayo kacheza mwanzo mwisho afu umeona nyimbo ya kiba ilivyowanyanyua kwan wanaelewa wabongo tuache mane no lol

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni