.

Jumanne, 4 Novemba 2014

Star gani atabadilishana jezi na Baloteli leo?



balo

Kipa wa Real Madrid Iker Cassillas amesema kuwa anatamani sana kubadilishana jezi na mshambuliaji wa Liverpool Mtaliano Mario Balotelli wakati timu zao zitakapocheza.
Casillas amesema hayo saa chache kabla ya mchezo kati ya Liverpool na Real Madrid ambao utachezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu katika mfululizo wa michezo ya ligi ya mabingwa .
Casillas ambaye ni nahodha wa Madrid amesema hayo huku akionya kuwa atafanya hivyo tu mara baada ya mchezo wao kumalizika na hawatabalishana jezi wakati wa mapumziko .
iker
Kauli hii inakuja zikiwa zimepita wiki mbili tangu Balotelli alipowaudhi mashabiki wa Liverpool kwa kitendo cha kubadilishana jezi na beki wa Real Madrid Pepe wakati wa mapumziko wakati timu hizo zilipokutana huko Anfield kwenye mchezo wa kwanza.
Liverpool na Real Madrid zinakutana kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa huku Madrid wakiwa kwenye kiwango cha juu tofauti na wapinzani wao ambao mambo hayajawaendea vizuri msimu huu .
Mario Baloteli alipobadilishana jezi na Pepep wakati wa mapumziko .
Mario Baloteli alipobadilishana jezi na Pepep wakati wa mapumziko .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni