.

Jumapili, 2 Novemba 2014

Ilivyokuwa mpaka nahodha wa Bafana Bafana akauwawa na Majambazi.



senzo 8Afrika Kusini ilishuhudia kwa masikitiko makubwa nahodha wa timu ya taifa Bafana Bafana na klabu ya Orlando Pirates Senzo Robert Meyiwa akifukiwa umbali wa futi sita kaburuni Jumamosi Novemba 1 zikiwa zimepita siku sita tangu alipouwawa kwa risasi baada ya majambazi kuvunja nyumba ya mama mzazi wa mpenzi wake ambae ni mzazi mwenzie ambaye pia ni star wa muziki wa Pop nchini Afrika Kusini Kelly Khumalo .
Huku raia wa Afrika Kusini wakiwa na hasira dhidi ya majambazi waliochukua roho ya marehemu Senzo, taarifa kamili ya kilichotokea dakika chache kabla ya tukio la kuuwawa kwa kipa huyo imetolewa.
Senzo alikuwa akijiandaa kutoka kwenye nyumba ya mama mzazi wa Kelly Khumalo wakati majambazi watatu walipovamia nyumba hiyo wakiwa na bastola ambapo walisikika wakiwaamuru waliomo ndani ya nyumba hiyo kutoa vitu vya thamani ikiwemo simu za mkononi na fedha taslimu.
Eneo la makaburini alikozikwa Senzo Meyiwa huko Kwazulu Natal , Afrika Kusini.
Eneo la makaburini alikozikwa Senzo Meyiwa huko Kwazulu Natal , Afrika Kusini.
Senzo ambaye alikuwa kwenye moja ya vyumba vya nyumba hiyo akicheza na mtoto wake wa kike ambaye amezaa na Kelly, aliwahi kuja sebuleni ambako alisikia kelele na kufahamu kuwa nyumba imevamiwa.
Mpenzi wa Senzo ambae Kelly Khumalo alikimbia chumbani kwa woga huku moja kati watu waliovamia akikimbia nyuma yake ambapo Kelly alifunga mlango na kuendelea kuzuia mlango huo huku jambazi akiwa anahangaika kuufungua.
Wakati mapmbano hayo yakiendelea jambazi mmoja alifyatua risasi chini kwa lengo la kuwatisha waliomo ndani ya nyumba hiyo na wakati huo rafiki wa Senzo ambaye alikuwa akimfuata jambazi huyo alikimbia na kutoka nje kwa hofu.
Umati wa watu waliojitokeza kushuhudia mazishi ya Senzo Meyiwa .
Umati wa watu waliojitokeza kushuhudia mazishi ya Senzo Meyiwa .
Senzo akiwa kwenye harakati za kutoka nje ya mlango kufukuzana na jambazi mwingine alipigwa risasi mgongoni na alikimbia huku damu zikiwa zinamtoka mpaka alipokutana na Kelly Khumalo na kuanguka mikononi mwake.
Harakati za kumkimbiza hospitalini hazikuweza kuwa na mafanikio yoyote kwani Kipa huyo tayari alikwishafariki kabla ya kufika hospitali.
Senzo Meyiwa alizikwa Jumamosi November 1 nyumbani kwao Kwazulu Natal baada ya shughuli ya mazishi iliyoanzia kwenye uwanja wa Moses Mabhida ambako watu wapatao elfu themanini waliujaza uwanja huo kumuaga staa huyu kipenzi cha mashabiki wa Olrando Pirates.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni