.

Ijumaa, 14 Novemba 2014

January Makamba kwenye Twitter baada ya kuandikwa na gazeti la Mtanzania


JayMakamba


Kibanda & J Makamba
Gazeti la Mtanzania leo Novemba 14 limeandikwa kichwa cha habari kinachosomeka hivi; “.. Utafiti watibua wagombea urais 2015.. January aupinga, Zitto amwambia aache siasa.. Keissy ashangaa Wasira kutosomeka katika ripoti..”
Kupitia mtandao wa Twitter, hiki ndicho kilichoandikwa na mhariri Absalom Kibanda na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba;
J. Makamba  : “ Unaelezeaje suala la gazeti lako kunukuu kinyume kabisa na mtu alivyosema? Umeambiwa.
A. Kibanda    : “ Nimeambiwa kaka. Badala ya kuandika JM kahoji wao wakaona umepinga utafiti.”
J. Makamba  : “ Si kweli. Na nimesema specifically sipingi. Heshima ndogo niliyobakiwa nayo na Mtanzania imeisha.”
A. Kibanda    : “ You judge the paper kwa kosa ambalo msingi wake ni kauli yako?! Worldwide media zinafanya makosa hayo ya tafsiri”
J. Makamba  : “ makosa yanatokea, ni kawaida na yanasameheka. Kupindisha makusudi kwa malengo mahsusi ni dhambi kwa wasomaji, tasnia na mhusika”
A. Kibanda    : “ Kaka unless silijui hilo. Siwezi kuruhusu gazeti naloongoza likuhujumu wewe au mwingine yeyote. Hata awe Membe anayenichukia”
JayMakamba IV
JayMaka Mwisho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni