.

Jumatano, 10 Septemba 2014

Mke Wa Mtu Atia AIBU baada ya kusaula nguo zote mbele ya Watoto wakati akicheza ngoma za Vigodoro


Wakati serikali ikipiga marufuku disko la mitaani maarufu kwa jina la ‘Vigodoro’ bado kuna baadhi ya mikoa inapuuza agizo hilo ambapo mwanamke mmoja ambaye mumewe anafanya kazi kwenye mgahawa uliopo ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Morogoro, aliyetajwa kwa jina la Mama Abdul (pichani), amejitoa fahamu kupitia Kigodoro na kujikuta akisaula nguo hadharani.
 
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri juzikati, majira ya mchana kwenye kigodoro mbele ya watoto waliopokea ekaristi takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Monica lililopo maeneo ya Kihonda mkoani hapa.
mke
Mke huyo wa mtu alimwaga ‘lazi’ hizo kwa kushirikiana na mdogo wake wa damu aliyefahamika kwa jina moja la Jacqueline wakati wakimpongeza mtoto wa rafiki yao aliyepokea ekaristi.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni