.

Jumanne, 30 Septemba 2014

Kesi dhidi ya Julius Malema yaahirishwa


Julius Malema
Kesi ya ufisadi inayomkabili kiongozi wa upinzani, nchini Afrika Kusini Julius Malema, imeahirishwa hadi Agosti mwaka ujao.
Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza hii leo lakini wakili mmoja muhimu hakuwepo.
Kiongozi huyo wa zamani wa kundi la vijana wa chama kinachotawala cha ANC anashtakiwa kwa kulaghai, matumizi mabaya ya fedha na kwa kuuza vitu kimagendo.
Bwana Malema amekanusha makosa yote na kusema kuwa madai dhidi yake yamechochewa kisiasa.
Wafuasi wa chama chake cha Economic Freedom Fighters, alichoanzisha baada ya kutimuliwa kutoka chama cha ANC mwaka 2012 - walikuwa wamekusanyika nje ya mahakama.
Bwana Malema amekuwa mstari wa mbele kushutumu ufisadi.
Bwana Malema mwenye umri wa miaka 33,ambae yuko nje kwa dhamana ya randi elfu 10 anakabiliwa na mashitaka manne ya Rushwa ,ufisadi ,kughushi nyaraka na kujipatia pesa kiasi cha randi million 4 kiujanja ujanja na kuzihaulisha katika shirika moja la Ratanang linalo semekana kumilikiwa na Malema mwenyewe .
Malema anayakanusha madai hayo yote na amekua akisema anafanyiwa njama na mahasimu wake kuweza kumuangusha kisiasa
Kama ilivo desturi yake Julius Malema aliandamana na wafuasi wake kwa wingi asubuhi ya leo kufika mahakama kuu ya Polokwane jimbo alikozaliwa mwenyewe.
Jitihada zake za kutaka kesi hiyo kutupiliwa mbali, mwaka jana hazikufua dafu.
                                                Malema akiandamana na wafuasi wake
Ikiwa atapatikana na hatia ya makosa yake, huenda akapoteza kiti chake bungeni.
Wakati wa kipindi cha maswali kwa Rais mnamo mwezi Agosti, Bwana Malema, alitatiza shughili hiyo kwa kumzomea Rais Jacob Zuma akimwambia alipe pesa alizopora kutoka kwa wananchi.
Alidai kuwa Zuma alitumia dola milioni 24 mali ya umma kukarabati nyumba yake ya kifahari.
Hata hivyo Malema ambaye alifurushwa kutoka kwa chama tawala mwenyewe anadaiwa dola milioni 1.6 ambazo alipaswa kulipa kama kodi kwa serikali.
Malema aliunda chama chake cha EFF baada ya kufurushwa kutoka kwa chama tawala, baada ya kutofautiana na Rais Zuma.
Tayari msemaji wa polisi wa mkoa wa Limpopo Brig Hangwani Mulaudzi amesema ulinzi utakua mkali. Barabara za mji wa Polokwane zinazoelekea kwenye korti kuu zitafungwa kuanzia saa 12 Alfajiri polisi ikipiga doria kupambana na uhalifu wowote utakaojitokeza mkiwemo eneo la Seshogo anakozaliwa Julius Malema

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni