.

Jumatatu, 1 Septemba 2014

Diamond aokolewa na Polisi Ujerumani kutokakwa washabiki wenye hasira


  • Kashindwa kuwika Stuttgart, kisa na mkasa?
  • Kafika ukumbini saa 10 alfajiri, washabiki wanasubiri show tangu saa 4 usiku
  • Promota Mnaijeria aingia mitini.
  • Dj apata kisago, eti vyombo vibovu. Aibu!

Stuttgart, Ujerumani - Usiku wa Jumamosi ya tarehe 30 Agosti 2014, majira ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa Bongo Flavor,  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.
Washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake.

Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki.

Ma-Djs walishambuliwa na wapo hosptalini kwa sasa. Mmoja wa Djs hao alipoteza laptop yake, mwanadada Dj Flor alipatwa shock (mstuko wa moyo) na kukimbizwa hosptali.
Washabiki hao walimpa kipigo Dj Drazee ambaye naye yupo hoi hospitalini. 
Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hili la aibu alijawahi kutokea. Kwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria, ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND" link:

http://www.stuttgarter-nachrichten.de/inhalt.blaulicht-aus-der-region-stuttgart-31-august-diamond-platnumz-zieht-aerger-der-fans-auf-sich.ca1f4b9d-599b-4c95-84c8-fe25d10b6ed9.html
---
Taarifa hii imewasilishwa kwa wavuti.com na mdau via email.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni