.

Jumapili, 20 Julai 2014

Uongozi YANGA wamchana Ridhiwani KIKWETE…wadai sio Mwanachama wao


Uongozi wa Yanga umesema Mwenyekiti wa Kamati ya ujezi wa jengo la Mafia, Ridhiwani Kikwete siyo mwanachama wa klabu hiyo kwa kuwa hajalipa ada yake kwa miezi sita mfululizo.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana kwa  vyombo vya habari na kusainiwa na Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto ilieleza kitendo cha Ridhiwani kupinga hatua ya Wajumbe wa Bodi ya Udhamini na wanachama wa Yanga kwa pamoja kumuongezea muda wa mwaka mmoja, mwenyekiti wao, Yusuf Manji hayana uzito kwa kuwa siyo mwanachama.
“Ridhwani Kikwete hajalipa ada zake za uanachama kwa miezi zaidi ya 6 mfululizo na kwa mujibu wa Katiba ya Yanga ibara ya 13 kipengele cha pili ambacho kinasema kuwa endapo mwanachama hajalipa ada yake kwa muda wa zaidi ya miezi sita mfululizo atakuwa amekoma kuwa mwanachama wa Yanga.”
“Maoni aliyoyatoa hayana uzito wa mwanachama wa Yanga, labda alikuwa akitimiza haki yake ya kutoa maoni kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaamini kama angekuwa ni Mwanachama hai wa Yanga angetoa maoni yake kwenye Mkutano wa dharura wa Wanachama  uliofanyika Juni Mosi. Pia angeweza kutoa  kwenye kitabu cha maoni ya kupinga maazimio ya Mkutano huo kilichowekwa hapa klabuni kuanzia Juni 23  hadi  27, hakuna aliyesaini zaidi ya mwenyekiti, Manji.
 Ridhiwani Kikwete
Ridhiwani Kikwete
“Niwakumbushe wanachama wa Yanga sehemu ya kuchangia maoni yao ni kwenye vikao vya Wanachama na siyo kwenye vyombo vya habari,  wasitafute umaarufu kwa njia za kubomoa kuliko kujenga wala wasiwadhalilishe waliojitosa kwa hali na mali kuisaidia Yanga kuwa bora kama Mama Fatma Karume wenye historia ndefu Yanga, tunaona ni sawa na udhalilishaji kwake, kwa kweli inasikitisha sana.
Taarifa hiyo ya Yanga imekuja ikiwa ni siku moja baadaya Ridhiwani kukaririwa na gazeti hili akisema haridhishwi na mambo ya migogoro ya kikatiba yanayoendelea ndani ya Yanga.
Tupe maoni yako hapo Chini..!!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni