.

Jumamosi, 26 Julai 2014

Aibu: MJOMBA Anaswa akila URODA na Mke wa MPWA wake Gesti huko MBEZI

Timbwili la aina yake lilifumuka ndani ya gesti moja iliyopo Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam (jina kapuni), kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina moja la Kelvin kumkuta chumbani mtu aliyedai ni mjomba wake, Joseph akiwa na mkewe wa ndoa, Emiliani.
 
Mkasa huo wa ajabu ulijiri usiku wa Jumamosi iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo Mbezi ya Afrikana jijini Dar es Salaam.
Mama mmoja aliyedai ni mpishi wa futari maeneo hayo, alipiga simu kwa mwandishi  na  kusema:
 
“Mimi ni mpishi wa futari hapa Mbezi Afrikana kuna baba mmoja na ndugu zake wanachakazana, kisa wamefumaniana kwenye gesti ya (akaitaja jina). Ipo hapahapa jirani njooni muwahi.”
 
Kufuatia taarifa hiyo, mwandishi  wetu  alifika  eneo  la  tukio  na kumkuta Kelvin amemvaa mjomba ‘ake chumbani ambapo timbwili zito lilitifuka. Walikuwa wakigaragazana huku mjomba mtu huyo akiwa kama alivyozaliwa na damu chapachapa jambo lililomtia aibu!
1
Mwandishi  bila kuzubaa alianza kuchukua picha za tukio  hatua kwa hatua. Wakati Timbwili likiendelea, Joseph alikuwa akipiga mayowe kumuomba mpwa wake huyo amsamehe ili wayamalize kimyakimya na kumsihi asisambaze habari hizo zikafika mpaka nyumbani kwa mke wake.
Katika hali ya kushangza, wakati wawili hao wakiendelea kuangushana chumbani, mke huyo alipata upenyo na kuchoropoka, akatimua mbio kwa kuhofia kipigo na kukwepa kamera.
2
 
Timbwili la wajomba hao lilitulizwa na mlinzi wa gesti hiyo (jina halikujulikana)  ambaye alitumia mabavu na kufanikiwa kuwadhibiti na kuwaweka kitako.
Baada ya kutulizwa, Kelvin aling’ang’ania waende polisi lakini mjomba mtu alikataa katakata akimbembeleza mpwa wake kwamba wayamalize na kuahidi kutorudia tena mchezo huo huku akisema mwanamke huyo alimuwekea mtego wa makusudi.
 
Baadhi ya waungwana waliofika kushuhudia tukio hilo walimsihi Kelvin kumsikiliza mjomba ‘ake na kupokea fidia kidogo kwani kuyasongesha mbele mambo hayo ni aibu kwa familia yao na kumtia matatani mjomba huyo kwa mkewe.
3
Kufuatia maombi ya watu, akiwemo mlinzi wa gesti hiyo, Kelvin alikubali kumsamehe mjomba wake ambaye naye ‘alijikomiti’ kimaandishi (kopi tunayo) kumlipa Kelvin fidia ya shilingi laki tano (500,000) na kuahidi kutorudia kummendea mke wake.
 
Katika barua hiyo aliyoaindika Joseph kwa mkono, alikiri kukutwa na mke wa Kelvin na kusema anatoa shilingi laki tatu (300,000) siku hiyo kisha kiasi kinachobaki atatoa siku inayofuata. 4
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni zinadai kuwa, Joseph alikwenda kituo cha polisi (jina halijajulikana) kumfungulia kesi mpwa wake Kelvin na mkewe Emiliani akidai walipanga kumfanyia fumanizi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni