.

Alhamisi, 26 Septemba 2013

Mastaa Waunga Mkono Sheria Ya Kutouza Watoto Wao




Mwigizaji Sandra Bullock ameweka wazi hisia zake kuhusu kitendo cha waigizaji wengi kutumia watoto wao kutengeneza pesa na kusema sio sawa na itadhalilisha watoto baadae.

Sandra ambaye ni mshindi wa tuzo kubwa ya Oscar amesema anaunga mkono kabisa sheria itakayozuia mapaparazi kusumbua watoto wao kwa sababu ya umaarufu wa wazazi wao. Sheria hii iliyopewa makali zaidi kwenye jimbo la california Inaruhusu watoto kuishi kama watoto na kutotumika kama mradi wa wazazi wao. Hii nikumanisha kuwa picha za watoto wa watu maarufu hazita uzwa kwa vyombo vya habari kwenye jimbo hilo. Gavana Wa California Jerry Brown ametia saini mswada huo jumanne iliyopita.



Sandra ni mmoja ya stars wakubwa anaye pigwa picha sana mjini hollywood akiwa na mtoto wake Louis Bardot mwenye miaka 3.
Waigizaji wengine kama Halle Berry na Jennifer Garner wameunga mkono sheria hio na kusema wao pia wamepitia wakati mgumu sana kutoka kwa paparazzi wakiwa na watoto wao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni