.

Jumamosi, 28 Septemba 2013

Fuatilia Hapa Kuhusu Rapper Young Jezzy Kubadilisha Jina Na Kurudi Studio


Rapper Young Jezzy Ametangaza Rasmi ujio wa cd yake mpya baada ya kutoa wimbo wa kwanza kutoka kwenye cd hio na kubadilisha Jina lake.


Wengi tuna mfahamu kama Young Jezzy Ila kwa sasa anatambulika zaidi kama "Jezzy" Tu na tayari rapper huyo kutoka Atlanta ametoa wimbo wa kwanza "In My Head," kutoka kwenye project yake mpya. Mpaka sasa imethibitishwa kuwa wasanii watakao husika kwenye project hii ni pamoja na Usher,Future, Ludacris,Dj Drama na Don cannon.

Kupitia jina lake Jezzy sasa rapper huyu anaweza kuwa balozi wa bidha nyingi zaidi ambazo zilishindwa kujihusisha na Young Jezzy wakati huo. Jezzy alishawahi kusema kuwa jina lake kubadilika haijamaanisha amebadilika kama rapper, ila amekuwa mtu bora zaidi na safari yake kwenye muziki imezaa matunda mazuri. Jezzy Amesema Alivyo anza muziki akiliyake ilikuwa ndogo kama jina lake ila sasa amekua na ni muda wa kuachana na jina 'Young'.

Fahamu kuwa Jezzy yupo kwenye orodha ya rappers duniani walioshawahi kuuza copi milioni moja kupitia album moja, Hii ilikuwa kwenye album ya Let's Get It na Thug Motivation 101 iliyotoka mwaka 2005 na watu kusema kuwa ilikuwa moja ya album bora ndani ya miaka 10.
Email This
BlogThis!
Share to Twitter
Share to Facebook

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni