Ujerumandiyo timu ya kwanza
kufuzu kwenye Fainali ya kombe la dunia Brazil 2014, baada ya kuinyeshea
wenyeji Brazil mabao 7-1 katika uwanja wa Estadio Mineirao ulioko Belo
Horizonte.
Umakini wa vijana wa Joachim Low ulikuwa wa
kupigiwa mfano walipoiadhibu Brazil na kuwa timu ya kwanza kuwahi
kushindwa kwa mabao mengi zaidi katika hatua hiyo ya nusu fainali ya
kombe la dunia.Kujeruhiwa kwa Neymar Ijumaa iliyopita ilimlazimu Scolari kubadili mfumo ambao sasa haukuwa na nyota huyo.
Je Scolari atasingizia nini ?
Na Baada ya nipe nikupe ya kufungua mechi Iliwachukuwa Wajerumani takriban dakika kumi tu za kwanza kupenya safu ya ulinzi ya Brazil iliyokuwa inakosa uzoefu wa Thiago Silva.
Klose kwa ushirikiano na Toni Kroos walifunga bao la tatu na la nne katika kipindi cha dakika moja.
Sami Kheidira alifunga la tano kunako dakika ya 29 kabla ya mchezaji wa akiba Andre Schurrle kufunga mabao ya 6 na ya 7 .
Bao la kufutia machozi la Brazil lilifungwa na Oscar kunako dakika ya mwisho ya mechi hiyo.
00:90 Oscar anaiifungia Brazil bao la kufutia machozi katika dakika ya mwisho ya mechi hii ya kihistoria .
00:70 Andre Schurrleanafanya mambo kuwa 6-0 kwa Ujerumani.
00:70 GOOOOOOOAL
00:59 Miroslav Klose anapumzishwa Andre Schurrle anaingia
00:57
00:54' Kipa Manuel Nuer anainyima brazil bao la kufutia machozi
23:35
23:30 Ujerumani 5-0 Brazil
23:26
23:24 GOOOOOOAL !Toni KROOOOS
23:20 Thomas Muller anafunga bao la pili la Ujerumani
23:20 GOOOOOOAL
23:20 Ujerumani 2-0 Brazil
23:18 Brazil wanaonekana wameduwazwa na bao hilo la Muller
23:15 Kona kuelekea upande wa Ujerumani
23:11 Ujerumani 1-0 Brazil
23:10 Thomas Muller anaiweka Ujerumani mbele 1-0
23:10 GOOOOOOOOOAL
23:09 David Luiz analazimika kufanya kazi ya ziada kufuatia mashambulizi ya mjerumani
23:05 Ujerumani inashambulia lango la Brazil lakini wapi inazimwa .
23:02 Ujerumani 0-0 Brazil
23:01 Ujerumani haina matatizo ya wachezaji ikilinganishwa na Scolari ambaye amelazimika kuchezesha kikosi bila ya Neymar
22:55 Wimbo wa taifa wa Brazil unapigwa hapa uwanjani ,,mashabiki wa Brazil wanaimba
22:54 Wimbo wa taifa wqa Ujerumani unachezwa hapa mbele ya uwanja uliofurika furifuri
22:52Mashabiki wa Brazil na wale wa Ujerumani wakishangilia timu zao kabla ya mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni