Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
amesema hatakatishwa tamaa na hatorudi nyuma katika harakati zake
anazoziita za fikra mpya na mawazo mapya za kushika dola na kwamba wazee
wakae kando.
Hata
hivyo, Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli (CCM) amewashukuru watu
wanaozungumzia nia yake ya kuwania urais mwaka 2015 na kutengeneza
mjadala unaoendelea nchini, jambo ambalo alisema linaashiria kuwa
dhamira yake imeeleweka.
Akiwa
London nchini Uingereza mapema mwezi huu, Makamba alitangaza nia hiyo
na kusema amefikia uamuzi huo kwa asilimia 90 lakini bado asilimia 10
katika baadhi ya mambo anayoendelea kuyatafakari, yakiwamo ya kuzungumza
na makundi mbalimbali ya wazee, viongozi wa dini na viongozi waliopita
ili apate ushauri wao kuhusu namna ya kufanya jambo hilo.
Julai
9, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, ambaye anamzidi januari kwa miaka
24, alisema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Soni, Bumbuli
mkoani Tanga kuwa Makamba anataka mambo makubwa, lakini hajamshirikisha.
Rais Kikwete alimtaka Makamba “asilazimishe” kwa kuwa wakati ukifika atapata kile anachokitaka. “Mie hajaniambia na mie nasikia,” alisema Kikwete.
Akizungumzia na gazeti la Mwananchi jana kuhusu kauli ya Rais Kikwete, Makamba alisema: “Ni
kweli sijamwambia. Siku itakapofika yeye ni mwamuzi na mwenyekiti wa
chama hivyo nitamweleza. Sitaki kumkwaza kwani na yeye ni wale waliopo
katika kundi la asilimia kumi,” alisema.
“Zama
za kizazi kipya za kutatua changamoto kwa kipindi cha miaka 30 hadi 50
ijayo zimewadia. Nitahakikisha mabadiliko ya haraka katika ardhi ya
Tanzania kwani inawezekana rasilimali za kutosha zipo kilichobaki ni
kuweka nidhamu katika nyanja zote.”
Aliwashangaa wanaombeza akisema kuwa hawamkatishi tamaa kwa hilo.
Tupe maoni yako hapo Chini..!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni