.

Jumatatu, 14 Julai 2014

TETESI ZA SOKA ULAYA


Mshambuliaji wa Uholanzi na Bayern Munich Arjen Robben, 30, amekataa 'ofa' ya kujiunga na meneja wake Louis van Gaal, Old Trafford (Daily Telegraph), Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ana matumaini ya kukamilisha usajili wa kipa wa Colombia David Ospina, 25, kutoka klabu ya Nice wiki hii (Daily Mirror), Chelsea wameanza mazungumzo kuhusu kumrejesha Didier Drogba, 'Darajani' kuwa mshambuliaji wa akiba na kocha (Daily Mail), mshambuliaji wa Liverpool Iago Aspas, 26, anajiandaa kujiunga na Sevilla kwa mkopo msimu wote ujao (Liverpool Echo), mipango ya uhamisho ya Tottenham imekwama kwa sababu kiungo Gylfi Sigurdsson, 24 na beki Michael Dawson, 30, hawataki kuondoka (Daily Mirror), wakala wa beki wa Spurs Jan Vertonghen, 27, amekiri kuwa mchezaji huyo huenda akaondoka White Hart Lane (Evening Standard), Liverpool wameanza tena kumfuatilia beki wa kushoto wa Sevilla Alberto Moreno (Daily Express), kocha wa Marekani Jurgen Klinsmann amesema amekataa 'ofa' kibao kutoka Ulaya, ikiwemo Galatasaray (Le Figaro), mshambuliaji wa Monaco, James (inatamkwa Hamez) Rodrigues, 23, amesisitiza kuwa anataka kuichezea Real Madrid, akisema ni juu ya rais wa klabu hiyo kufanya uamuzi (Marca), Lazar Markovic atafanya vipimo vya afya Liverpool Jumatatu, kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa euro milioni 25. Brendan Rodgers anataka kumchukua pia Wilfried Bony kuziba nafasi ya Luis Suarez (Daily Telegraph), boss wa Chelsea Jose Mourinho anataka kumchukua Sami Khedira. Arsenal walikuwa wakimtaka mchezaji huyo, lakini sasa wataanza kumfuatilia zaidi Lars Bender (Daily Mail), Liverpool huenda ikaingia Southampton tena, safari hii wakimtaka Jay Rodriguez kuchukua nafasi ya Iago Aspas (Daily Mail), Manchester United inakaribia kumsajili kiungo kutoka Chile, Arturo Vidal anayechezea Juventus. United wamekubaliana ada ya uhamisho ya euro milioni 40, na kuhama kwa Patrice Evra kwenda Juve (Marca), Juventus watamfuatilia Paulinho kutoka Tottenham iwapo watamuuza Arturo Vidal (Daily Express), Manchester United watakabiliwa na ushindani kutoka Barcelona kumsajili beki wa kati wa Borussia Dortmund Mats Hummels. Luis Enrique anamtaka Hummels baada ya mazungumzo ya kumsajili Marquinhos kuvunjika (Daily Star). Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho. Uhamisho wowote ukithibitishwa nitakufahamisha. Kesho tukijaaliwa-Cheers!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni