Mtoto Devota Malole
aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilosa kufuatia mama
yake kumtesa kwa kumfungia ndani na kumlaza chini kwa muda wa miaka
mitano amehamishiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada
ya afya yake kiafya kubadilika.
Mganga
mkuu wa hospitali ya wilaya ya kilosa Dr Shedrack Mponzi amesema
wamelazimika kumuhamishia mtoto huyo katika hospital ya rufaa ya mkoa wa
Morogoro baada ya hali yake kuwa mbaya na uchunguzi wa awali umebaini
anamagonjwa mbalimbali ikiwemo utapia mlo kwa kukosa lishe ambapo katika
hospitali ya mkoa wa morogoro waandishi wetu wameshuhudia madaktari
wakifanya kila juhudi za vipimo na matibabu.
Wasamaria
wema wamejitokeza katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kumjulia hali
mtoto Devota ambapo mbunge wa jimbo la Morogoro Abdul Azizi Abood
amewataka maafisa ustawi wa jamii kuacha kulala na badala yake
watekeleze wajibu wao ipasavyo kuwasaidia watoto wanaoteseka .
Nae
mfanyabiashara wa kampuni ya mabasi ya Alsaidi Omari Alsaidy ameahidi
kugharamia matibabu ya mtoto huyo hata kama italazimika kupelekwa nje ya
nchi kwa matibabu ili kunusuru maisha yake.
Tupe maoni yako hapo Chini..!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni