Jumatano, 25 Septemba 2013
Serikali Imesema Imejiandaa Vya Kutosha Kukabiliana Na Tatizo La Uhaba Wa Chakula Nchini
Waziri mkuu Mh Mizengo Pinda amesema serikali imejiandaa vya kutosha kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula nchini kwa kuendelea kujenga uwezo wa kujiwekea akiba ya chakula kwa kununua mazao toka kwa wakulima msimu wa mavuno na kuyahifadhi kwenye maghala ya taifa .
Akizungumza baada ya kutembelea ghala ya chakula kanda ya kasikazini lililoko jijini Arusha Mh Pinda amesema ili kuhakikisha kuwa lengo hilo linatimia serikali imeamua kuishirikisha sekta binafsi vikiwemo vikundi vya wananchi katika ununuzi na uwekaji wa akiba ya kuhusu hatua iliyofikiwa katika zoezi la ununuzi wa chakula naibu waziri wa chakula na ushirika Mh Adam malima amesema hali sio mbaya na lengo lililowekwa limefikiwa kwa asilimia kubwa.
Wakizungumzia hali ya upungufu wa chakula katika mkoa wa Arusha ambao nimiongoni mwa iliyoko kwenye tishio la njaa mkuu wa mkoa huo bw Magesa Mulongo na wakala wa usagishaji na usambazaji wa unga bw Philemoni Molel wamesema changamoto bado na kubwa na jitihada zaidi zinahitajika ikiwemo ya kuelimisha jamii na kuondoa urasimu katika suala zima la usindikaji na usambazaji wa chakula .
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni