Waumini wakipandishwa kwenye difenda.
Inadaiwa kuwa waumini wa kanisa hilo lenye jengo la ghorofa moja
walikuwa katika mgogoro uliotokana na madai ya ubadhilifu wa fedha,
hivyo kuwafanya kugawana sehemu za kufanyia ibada, kundi moja likisali
chini na jingine juu, kila moja likiwa na mchungaji wake, ambao ndiyo
waliokuwa wakiongoza mzozo huo.Ghafla, kundi lililokuwa likisali chini likaamua kuwafungia milango wale wa juu na kuwafanya kuendesha ibada yao nje, chini ya mwembe kwa siku kadhaa kabla ya kuamua kuvamia kanisani ili nao wasali kama wenzao, ambao walikataliwa na hivyo timbwili kubwa kuanza.
Askari wakiwa na silaha.
Wakiwa na fimbo na mawe, waumini hao wa makundi yote mawili walileta
tafrani kubwa kabla ya wasamaria wema kutoa taarifa Polisi ambao
walifika eneo la tukio na kujaribu kutuliza ghasia lakini bila
mafanikio, hadi walipoamua kutumia mabomu ya kutoa machozi na kufanikiwa
kudhibiti vurugu hizo zilizosababisha mtu mmoja kujeruhiwa, sambamba na
kuwakamata waumini 29 ambao walishikiliwa katika kituo cha polisi
Oyesterbay jijini Dar es Salaam.
Waumini chini ya ulinzi.
Habari ambazo hazikuweza kuthibitishwa mara moja zinasema chanzo cha
mgogoro huo ni ubadhilifu wa fedha za kanisa, baada ya kugundulika kuwa
nyumba moja iliyonunuliwa, ilipewa thamani kubwa ya pesa ambazo
zilishatolewa, lakini mwenye nyumba alikataa kutoa hati akitaka
kumaliziwa fedha zake, jambo lililowashangaza waumini ambao walihoji.Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hatua za kisheria zitafuata baada ya uchunguzi kukamilika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni