Aliyekuwa Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana nchini Afrika kusini Desmond Tutu ameingilia kati mjadala kuhusu kuwasaidia wanaotaka kujitoa uhai,akisema kuwa anaunga mkono haki ya wale wanaougua kupitia kiasi kuamua kujitoa uhai kwa heshima.
Katika ripoti yake ilioandikwa katika gazeti moja la Uingereza la Observer ,kiongozi huyo wa dini aliyestaafu amesema kuwa sheria zinazowazuia watu kusaidiwa kujitoa uhai zinazua maswali mengi kuhusu hali ya maisha na kuhusu vile watu wanavyotumia fedha ili kuongeza kipindi cha maisha yao.
Matamshi yake yanajiri wakati ambapo bunge la Uingereza linaandaa kujadili mswada wa kusaidiwa kujitoa uhai baadaye wiki hii.
Bwana Tutu pia ametaka sheria za Afrika kusini kuangaziwa upya kuhusu kusaidiwa kujitoa uhai.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni