Staa
wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kusema kuwa ushosti
wake na Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu, uliorudishwa hivi karibuni
baada ya kuwekana sawa ni wa kinafiki huku akidai Wema ni kigeugeu.
Akizungumza
kwa kujiamini mbele ya waandishi wetu, juzi Jumatano pande wa Mikocheni
jijini Dar es Salaam, Kajala alisema: “Wema ni mnafiki kabisa.
Upatanisho wetu ni wa uongo. Mimi moyoni nimeondoa kinyongo lakini
mwenzangu naona kama bado ana donge moyoni.”
Kajala
alisema hayo alipoulizwa na Risasi Jumamosi, sababu ya kutoonekana
kwenye tukio la futari lililofanyika nyumbani kwa mama mzazi wa Mbongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ambaye ni mkwe wa shosti
wake huyo.
Katika
tukio hilo, mama Diamond alifanyiwa sapraizi ya nguvu alipokabidhiwa
gari kali aina ya Toyota Lexus Harrier kama zawadi ya bethidei yake,
ambayo ilitolewa na meneja wa Diamond, Babu Tale kwa niaba ya
mwanamuziki huyo ambaye alikuwa safarini nchini Marekani.
“Tunakubaliana
kuwa kitu kimoja lakini mwenzangu anaonekana ana kinyongo. Hebu
angalia, anawezaje kuacha kunialika kwenye shughuli muhimu kama ile kama
kweli tumepatana? Mbona amealika watu wengi lakini mimi ameniacha? Wema
aache unafiki bwana.
“Mbaya
zaidi, hivi juzi tu ameweka picha ya msichana mmoja anayekaa China,
huyu mdada anaitwa Sabrina, niliwahi kugomabana naye, lakini yeye
amemuweka Instagram na kumwandikia maneno kibao ya kumsifia akim-wish
happy birthday, hapo si kama ananisimanga? Wema si mkweli,” alisema Kajala.
Akizungumzia ishu hiyo, siku ya tukio Wema alisema: “Ukiniuliza kuhusu Kajala kutokuwepo hapa, kwa kweli utakuwa kama unanichanganya tu maana leo sijashika simu muda mrefu sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni