Takriban watu 50, wameuawa
katika shambulizi la bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari katika soko
moja lenye shughuli nyingi , katika mkoa wa Paktika, Mashariki mwa
Afghanstan.
Soko lilikuwa na idadi kubwa ya watu wakati wa shambulizi lilipofanyika. Mwandishi wa BBC anasema kuwa mkoa wa Paktika ni ngome ya wapiganaji wa mtandao wa Haqqani na hushuhudia mashambulizi ya mara kwa mara.
Hakuna kundi lililokiri kufanya shambulizi hilo.
Awali polisi walisema kuwa wanaume wawili waliokuwa wakimfanyia kazi Rais anayeodnoka mamlakani Hamid Karzai wameuawa katika shambulizi lengine la bomu mjini Kabul.
Bomu hilo linalokisiwa kutegwa kando ya barabara lililipuka karibu na gari ambalo wawili hao walikuwa wakisafiria kwenda kazini .
Kundi la Taliban limekiri kuhusika na shambulizi hilo ambalo pia liliwajeruhi watu wengine watano
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni