.

Jumatano, 16 Julai 2014

Israel yawataka wakaazi wa vijiji 3 katika ukanda wa Gaza kuondoka

Wapelestina wa  miji ya Zeitoun, Shoujaiya na Beit Lahiya wametakiwa kuondoka katika nyumba zao na kuelekea mjini Gaza.
Wapelestina wa miji ya Zeitoun, Shoujaiya na Beit Lahiya wametakiwa kuondoka katika nyumba zao na kuelekea mjini Gaza.
REUTERS/Mohammed Salem

Na bongonewz255.blogspot.com
Jeshi la Israel limetangaza jumatanu wiki hii kwamba limewatolea wito wakaazi 100.000 kaskazini mwa ukanda wa Gaza kuondoka katika nyumba zao, baada ya kuahidi kuongezea mashambulizi siku moja baada ya kukwama kwa pendekezo la Misri la kusitisha mapigano.

“Takriban watu 100.000 wamepata ujumbe wa kuondoka wa kuondoka katika nyumba zao, kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi.
Wito huo kuhusu wakaazi wa Zeitoun, Shoujaiya na Beit Lahiya, wameupata kupitia sauti ziliyorikodiwa kwa sim, jumbe za sim na nyaraka ziliyosambazwa, jeshi limethibitisha katika tangazo lake.
Waandishi wa shirika la habari la Ufaransa la AFP wameshuhudia nyaraka hizo zikisambazwa katioka mji wa Zeitoun, kusini mashariki mwa mji wa Gaza.
Kwa mujibu wa jeshi la Israel, Licha ya pendekezo la kusitisha, kundi la Hamas na makundi mengine ya kigaidi yaliendelea kurusha makombora, ambayo mengi yalikua yakirushwa kutokea maeneo hayo matatu.
“Kwa usalama wenu, muliombwa kuondoka katika nyumba zenu haraka iwezekanavyo na kuelekea mjini Gaza kabla ya saa kumi na moja alfajiri saa za kimataifa jumatano wiki hii, jeshi limeendelea kusema, huku likibaini kwamba halitaki kufanyia vibaya wakaazi wa miji hio mitatu.
Ujumbe kama huo ulitolewa katika mji wa Beit Lahiya, na kupelekea watu 17.000kuomba hifadhi katika shule zinazodhaminiwa na Umoja wa Mataifa.
Israel imeendesha takriban mashambulizi 1.500, ambayo yamesababisha vifo vya watu 200 katika ukanda wa Gaza tangu Julai 8. Israel imebaini kwamba imeendesha mashambulizi hayo kwa lengo la kujaribu kukomesha kitendo cha Hamas cha kurusha makombora katika aridhi ya Israel.
Wakati huo huo, maelfu ya makombora yalirushwa katika aridhi ya Israel na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
tags: Palestina - Israeli - Hamas - Benjamin Netanyahu - Mahmoud Abbas

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni