Staa
wa kike anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki na filamu
nchini, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ amewatolea uvivu wasanii
wenzake kwa kuifumua tasnia hiyo kuwa asilimia kubwa ya
wasanii ni washirikina na wanalogana….
Msanii
huyo amewashutumu baadhi ya wasanii Bongo kuwa hawawezi
kufanya jambo lolote muhimu bila kufanya ushirikina na wengine
hawapendi kuona wenzao wakitoka kimaisha…..
Madaha
amefikia hatua ya kufumua ushu hiyo kwa madai kuwa hata
kufilisika kwake ghafla kumetokea baada ya aliyekuwa mpenzi
wake raia wa Kenya Joe Kairuki kupunguza nguvu ya kumsaidia
kisanii na kwamba ilitokana na rafiki zake kumpiga juju….
“Wasanii
wenzangu wameniloga.Walikuwa wanaona donge sana Joe alipokuwa
akinisaidia.Kiukweli wameniporomosha kabisa.Nilienda kwa mtaalamu
akanithibitishia hili.Hata hivyo nimepata mfadhili mwingine.Siwezi
kumtaja wasije wakanipiga kipapai tena,” alifunguka staa huyo wa wimbo wa Summer Tyme.
Alisema
ushirikina umeifanya tasnia ya sanaa kudumaa kwa kiasi kikubwa
na kwamba imani hiyo imesababishwa na wsanii wasio na elimu….
“Wasanii
wachawi wapo wengi tu.Yaani unamuona msichana mzuri au mvulana
mtanashati msanii kumbe anakesha kwa waganga.
“Wengi
wanasafiri sana kwenda mikoani kuloga wenzao.Sanaa imejaa
uchuro mtupu. Kama si kuelemewa na ushirikina basi tungekuwa
mbali sana.
“Ushirikina umesababisha pia fitina, majungu na visilani miongoni mwa wasanii. Hatupendani kwa sabab ya mioyo ya kichawi,” Alisema Baby Madaha
“Ushirikina umesababisha pia fitina, majungu na visilani miongoni mwa wasanii. Hatupendani kwa sabab ya mioyo ya kichawi,” Alisema Baby Madaha
Tupe maoni yako hapo Chini..!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni