Uongozi wa Yanga umesema Mwenyekiti wa Kamati ya ujezi wa jengo la
Mafia, Ridhiwani Kikwete siyo mwanachama wa klabu hiyo kwa kuwa hajalipa
ada yake kwa miezi sita mfululizo.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na
kusainiwa na Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto ilieleza kitendo cha
Ridhiwani kupinga hatua ya Wajumbe wa Bodi ya Udhamini na wanachama wa
Yanga kwa pamoja kumuongezea muda wa mwaka mmoja, mwenyekiti wao, Yusuf
Manji hayana uzito kwa kuwa siyo mwanachama.
“Ridhwani Kikwete hajalipa ada
zake za uanachama kwa miezi zaidi ya 6 mfululizo na kwa mujibu wa Katiba
ya Yanga ibara ya 13 kipengele cha pili ambacho kinasema kuwa endapo
mwanachama hajalipa ada yake kwa muda wa zaidi ya miezi sita mfululizo
atakuwa amekoma kuwa mwanachama wa Yanga.”
“Maoni aliyoyatoa hayana uzito wa mwanachama wa Yanga, labda alikuwa akitimiza haki yake ya kutoa maoni kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaamini kama angekuwa ni Mwanachama hai wa Yanga angetoa maoni yake kwenye Mkutano wa dharura wa Wanachama uliofanyika Juni Mosi. Pia angeweza kutoa kwenye kitabu cha maoni ya kupinga maazimio ya Mkutano huo kilichowekwa hapa klabuni kuanzia Juni 23 hadi 27, hakuna aliyesaini zaidi ya mwenyekiti, Manji.
“Niwakumbushe wanachama wa Yanga sehemu ya kuchangia maoni yao ni kwenye vikao vya Wanachama na siyo kwenye vyombo vya habari, wasitafute umaarufu kwa njia za kubomoa kuliko kujenga wala wasiwadhalilishe waliojitosa kwa hali na mali kuisaidia Yanga kuwa bora kama Mama Fatma Karume wenye historia ndefu Yanga, tunaona ni sawa na udhalilishaji kwake, kwa kweli inasikitisha sana.
Taarifa hiyo ya Yanga imekuja ikiwa ni siku moja baadaya Ridhiwani
kukaririwa na gazeti hili akisema haridhishwi na mambo ya migogoro ya
kikatiba yanayoendelea ndani ya Yanga.
Tupe maoni yako hapo Chini..!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni