WIKI iliyopita tuliona jinsi fangasi wanavyoambukiza na kusababisha madhara mbalimbali sehemu za siri.
Leo
tunakwenda mbele zaidi kwa kuangazia akina mama wenye ujauzito ambao
hupata fangasi hawa kutokana na kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini
na kupungua kwa kinga ya mwili.
Hata hivyo, ieleweke kuwa si kila mjamzito hupatwa na maambukizi haya ya fangasi wa Candida albicans.
Matumizi
ya dawa za kupanga uzazi maarufu kama vidonge vya majira huweza
kusababisha mtu kukumbwa na maambukizi ya fangasi hawa.
Lakini pia
wale wenye upungufu wa kinga mwilini (HIV/AIDS) nao wana hatari ya
kupata magonjwa sugu kama kisukari, saratani aina yoyote ile, ugonjwa
aina ya mononucleosis na nk.Wengine wanaopata maradhi ni wale waliopata
matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy) kutokana na sababu
mbalimbali au matibabu ya kusaidia kushika mimba kwa wale wenye matatizo
ya uzazi.
Wenye utapiamlo (malnutrition) nao wanaweza kupata tatizo hili.
Wengine
wanaoweza kupata ugonjwa huu ni wale wenye tabia ya kuvaa nguo au
mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri kama nguo za kuogelea (swim
wear), chupi zilizotengenezwa kwa kitambaa aina ya nailon au zinazobana
sana nk.
Lakini wale
wanaojamiiana kwa njia ya kawaida kufanya kitendo hicho kupitia njia ya
haja kubwa (anal sex) au matumizi ya vilainishi vyenye glycerin wakati
wa kufanya tendo la ndoa wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya
maradhi haya.
UCHUNGUZI NA VIPIMO
Kabla
ya vipimo vya uchunguzi, mgonjwa atafanyiwa vipimo vya uchunguzi wa
uke kitaalamu huitwa per Vaginal Examination (PV exam) kuona kama kuna
uvimbe wowote ndani ya utupu huo au kama ana maumivu wakati wa
kujamiiana.
Daktari
ataangalia kama kuna uchafu wowote unaotoka, wingi wake, rangi yake,
harufu yake, uzito wake na aina ya uchafu unaotoka kama ni sahihi
kutokana na maelezo ya mgonjwa.
Kwa kifupi
daktari ataangalia mambo mengi kama vile kuna uvimbe wowote wa tezi za
sehemu ya siri yaani mitoki, shingo ya kizazi, bartholin glands nk.
Ataangalia sehemu ya haja kubwa kama kuna skin tags, bawasiri
(haemorrhoids) nk. Inashauriwa kuwa kabla ya kufanya vipimo, daktari
amjulishe mgonjwa aina ya kipimo, lengo lake na jinsi kitakavyofanyika
ili kumuandaa kisaikolojia.
Daktari
anaweza kuchukua kipimo na kuotesha kwenye maabara ili kuangalia aina ya
uoto huo kama ni wa fangasi aina ya Candida albicans, ama la, atafanya
kipimo cha mkojo (Urinalysis), na cha ugonjwa wa kisukari, HIV/AIDS,
ugonjwa wa kuvimba tezi la koo (goiter) na kadhalika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni