Jana Nov 21, Diamond amesikika kwenye show ya XXL
ambapo amezungumzia mambo mengi, baadhi ya yale aliyoyazungumzia ni
pamoja na story zilizoenea mitandaoni kwamba mahusiano ya msanii huyo na
Wema yameisha pamoja na story ambayo imetokana na kuenea kwa picha
mitandaoni za msanii huyo na Zari the Boss Lady kutoka Uganda.
Hii ni sehemu ya mahojiano aliyofanya Diamond kwenye XXL:
Adam Mchomvu :”…Nataka
kujua ile vibe ya Fiesta that day, story zilikuja ooh Diamond kazomewa..
kazomewa kazomewa..na vitu kama vile, sijapata chance ya kukusikia wewe
una kipi cha kuzungumzia kuhusiana na that situation..?“
Diamond :- “… Siku zile
kwangu ilikuwa kama mchezo, unajua muziki ushakuwa kama sio fani tena,
ushakuwa kama siasa.. So, lazima uichukulie hivyo wewe mwenyewe kama
msanii ujue una control vipi kwa sababu sio mara ya kwanza vitu kama
hivyo vishatokea Maisha.. Maisha yalitupwa mpaka na mayai viza kabisa..
Ni vitu ambavyo vikitokea naonaga kama ni kawaida…“
B 12 :-“…Kwa hiyo ukweli uko wapi kati yako wewe na Wema Sepetu?…”
Diamond :- “…Kuna vitu vitu
fulani nadhani kuvizungumza sio vizuri… Lakini ikifikia kuvizungumzia
vinazungumziwa… Uzuri wa mahusiano yetu ni kwamba kila mtu anafahamu…
Haijafikia kuweka wazi ndio maana ninapoulizwa inakuwa ni swali gumu
kulijibu.. “
B 12 :- “.. Ni gumu kwa upande wako lakini yeye yuko tayari kuzungumza kwamba it’s over kati yangu mi’ na Diamond…“
Diamond :- “… Sijui…“
B 12 :- “…Hii ngoma kama
umemzungumzia yeye direct hivi… watu wamekuza akili zao zikaenda mbali
zaidi kimawazo lakini, kwamba inawezekana ile singo umemwimbia yeye hivi
kwamba bado unamzimia japokuwa bado kama kakutosa hivi…“
Diamond : “.. Waswahili
wanasema ‘A’ na ‘B’ yote majibu, halafu ukisikiliza ile nyimbo kama
kweli mtu mwenye ufahamu wako, kweli kabisa hauwezi kuwa na maswali
mengi …“
Kuhusiana na mahusiano yake na Zari the Boss Lady, Diamond amejibu hivi:
Diamond :- “.. Zari ni
rafiki yangu tu, alipokuja hapa mimi ndio nilikuwa mwenyeji wake
Tanzania na kama mimi ndiyo mwenyeji sikutaka kuleta roho za kibaguzi,
unajua hata alipokuja Davido pia ilibidi awe na mimi karibu ili hata
kesho na kesho kutwa mimi nikiwa Nigeria basi Davido anipokee hivyo
hivyo…“
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni